Gamba Jipya
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 401
- 80
Tumeona wenyekiti wa vyama vyenye ushawishi mkubwa vya CDM na CUF kupeleka wenyeviti wao katika kampeni za ubunge jimbo la Igunga zinazoendelea hivi sasa.
Kutokana na tathmini na taarifa kadhaa za kiutafiti imebainika kuwa vyama vyenye ushawishi mkubwa jimboni hapo ni CCM na CDM na ijulikane kuwa mnano tarehe 25 ya mwezi huu CDM wanampango wa kuingiza silaha zao za mwisho za maangamizo kama vile, Sugu,Wenje,Mnyika,Mdee,Kiwia,Lema n.k hawa ni watu wenye ushawishi mkubwa sana kwa vijana kitu ambacho CCM hatuna vijana wenye ushawishi wa kiasi hiki,
Je ni wakati muafaka sasa wa mwenyekiti wetu ambaye ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana na wazee kuingia Igunga na kumalizia mashambulizi, wasawasi wangu ni pale matokeo ya uchaguzi yakaonekana tumeangushwa je umaarufu wa mwenyekiti wetu na chama kwa ujumla utakuwa kwenye hali gani.
Je ni wakati muhimu sasa wa kuomba nguvu za mwenyekiti?
Kikwete ni mjanja sana kitu chochote ambacho anaamini ataumbuka hagusi, kwa mfano wakati alipoombwa ashiriki midaharo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alikataa katakata kwasababu anaufahamu uwezo wake vizuri sana tena tokea anasoma chuo, yanini akubali kutwangwa maswali na watu ambao anaamini kabisa wako juu sana kifikra si ni kujiumbua tuu? Kwasasa kikwete anaweza kuwa ni Rais asiye na mvuto kuliko Rais yeyote kwa Africa unategemea anaweza kujitokeza mbele za watu kumnadi mtu? au unadhani chama kilikosea kumtuma Mkapa aende Igunga.Hata saidia. Siku hizi hana mvuto, hana ushawishi.
Mkuu mwenyekiti ndio kwanza kenda za New York kujipoza...Mwenzake Karzai wa Afghanstan karudi nyumbani baada ya rais wa zamani kuuawa, kaahirisha kabisa mkutano wa UN hali JK watu zaidi ya 1000 wamekufa maji hakwenda hata Pemba kuwapa pole kaishia Unguja mara huyooo New York - siku ya maombolezi Pemba katuma wajumbe.
Nape mwenyewe anawapelekesha mputa huyo mwenyekiti si atawainamisha magwanda kabisa
Mwita25 mambo vip?mbona leo unatumia id hii au baada ya kujibu uharo sakata la dc igunga na kuumbuka?Nape mwenyewe anawapelekesha mputa huyo mwenyekiti si atawainamisha magwanda kabisa
Tumeona wenyekiti wa vyama vyenye ushawishi mkubwa vya CDM na CUF kupeleka wenyeviti wao katika kampeni za ubunge jimbo la Igunga zinazoendelea hivi sasa.
Kutokana na tathmini na taarifa kadhaa za kiutafiti imebainika kuwa vyama vyenye ushawishi mkubwa jimboni hapo ni CCM na CDM na ijulikane kuwa mnano tarehe 25 ya mwezi huu CDM wanampango wa kuingiza silaha zao za mwisho za maangamizo kama vile, Sugu,Wenje,Mnyika,Mdee,Kiwia,Lema n.k hawa ni watu wenye ushawishi mkubwa sana kwa vijana kitu ambacho CCM hatuna vijana wenye ushawishi wa kiasi hiki,
Je ni wakati muafaka sasa wa mwenyekiti wetu ambaye ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana na wazee kuingia Igunga na kumalizia mashambulizi, wasawasi wangu ni pale matokeo ya uchaguzi yakaonekana tumeangushwa je umaarufu wa mwenyekiti wetu na chama kwa ujumla utakuwa kwenye hali gani.
Je ni wakati muhimu sasa wa kuomba nguvu za mwenyekiti?
Je ni wakati muafaka sasa wa mwenyekiti wetu ambaye ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana na wazee kuingia Igunga na kumalizia mashambulizi, wasiwasi wangu ni pale matokeo ya uchaguzi yakaonekana tumeangushwa je umaarufu wa mwenyekiti wetu na chama kwa ujumla utakuwa kwenye hali gani.
Je ni wakati muhimu sasa wa kuomba nguvu za mwenyekiti?
Nape mwenyewe anawapelekesha mputa huyo mwenyekiti si atawainamisha magwanda kabisa