Ushindani: Je, Ni Lazima Kumshinda Mwingine?

Ushindani: Je, Ni Lazima Kumshinda Mwingine?

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
911
Reaction score
792
Shule zilitufundisha kushindana. Kujua umefaulu na hivyo ufurahi kwa kiwango gani ilikuwa lazima ujue kwanza umekuwa wa ngapi kwenye orodha ya mwalimu. Thamani ya alama zako ilitegemea alama walizopata wengine.

Nyumbani, tulikokulia, nako maelekezo mengi yalilenga kutulinganisha na wenzetu. Kila jambo jema lilikuwa na lugha ya ulinganisho.
‘Umeona mwenzako?’
‘Fanya kama nanihii.’
‘Wenzako wote wanaweza.’

Matokeo yake ushindani umekuwa sehemu ya maisha yetu. Hata ukiulizwa unaendeleaje, unajibu, ‘Tunapambana!’ Kila wakati inakuwa kama furaha yako inategemea umewashinda wangapi.

Kipimo cha bidii na uwezo wako kinakuwa uwezo wa kushindwa kwa wengine. Unajiona unaweza kwa vile wengine hawawezi. Unajiona mzuri kwa vile ‘una kitu’ ambacho wengine wote hawana. Tatizo la kushindana sana ni kufika mahali unashindana hadi na kivuli chako mwenyewe na huridhiki.

Kadri unavyokua, maisha yanakufundisha kumbe kila mtu ana hatua zake, kwa vigezo vyake na kwa majira yake. Unaweza kabisa kufanya kikawa kizuri na ukakifurahia bila kumshinda yeyote. Unaweza kuwa hodari bila kumfanya mwenzako akaonekana dhaifu. Ukifika hapo utafanya vitu vikubwa kwa utulivu, bila mashindano na utapata matokeo makubwa bila kuumiza hisia za mtu.
 
Back
Top Bottom