Ushawahi lala njiani baada ya gari kuharibika?

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,491
Mimi leo inanikuta, naelekea Korogwe sasa hivi ndio kwanza tupo Bagamoyo gari imeharibika mara mbili.

Hapa watu hawajafuturu, chakula chetu ni mmbu maana wametuzunguka.

Makonda wanatengeneza gari, wanatupa matumaini ila hii ngoma naona kabisa hatuchomoi,.

Kushuka kutafuta gari nyingine ni mtihani sababu nina mizigo mikubwa.
 
 
[emoji28][emoji28] ndio mbona ulifika mbali sana
 
Ilikuwa Mpanda sumbawanga, enzi za summry daah tulikwama siku 2,, jion yake tukatoka ilaa nilipatagaa kademu nikakadinyia humohumo kwa bus coz watu wengi waliondok na magari mengine, so tukabaki kama abiria 6 tuu basi zimaa [emoji2]
 
Yaani nyie msipomtaja Makonda 🙂 hamridhiki kwa maongezi yenu finyu, siyo!??? Haya sasa Mh kaongeza mawe, semeni lingine.
 
Wami, ngoma ilifeli kupanda mlima, ilikula mzigo wa kutosha, buti tuu ilikula kama tani 3 za tiles...
Ukitoka wami kuna ka mji kwa kwanza sijui panaitwaje pale, ndio tulienda kutafuta msosi, tukakuta samaki ndio wanakaangwa, ikabidi wawe mlo kamili.

Pia msamvu kwenda ifakara, ile sehemu yenye daraja kubwa ambapo ukiimaliza tuu unaanza barabara ya vumbi(kwa kipindi kile sijui sasa) nahisi ni daraja la mto ruaha. Maeneo yale nayo nishapindua..
 
Mara kibao tu paleee Mwenge ila kamata hizi mbili, gari yangu ya kwanza kirkuu, nikiwa na mapara chichi kuelekea Mbezi Beach, gari likapata pancha na hela ya ziada sina halafu jioni, nili lala pale victoria.

ya pili ni paleee kwa azizi Ally, rejeta ilifumuka ghafla nikalala pale siku mbili!! nakula kwa ma ntilie
 
Kilombero hapo,siku hizi kuna lami inajengwa kutoka Ruaha kwenda Ifakara
 
Ilikuwa Mpanda sumbawanga, enzi za summry daah tulikwama siku 2,, jion yake tukatoka ilaa nilipatagaa kademu nikakadinyia humohumo kwa bus coz watu wengi waliondok na magari mengine, so tukabaki kama abiria 6 tuu basi zimaa [emoji2]
Mara ya mwisho umepima HIV status lini?
 
Mwaka 97 siku hiyo ndio nilijua pesa haimalizi shida zote.
Tulikuwa na pesa but hamna chakula cha kununua. Kuna abiria alikuwa na dagaa ametoka kununua ziwa nyasa huko Ukisi alituokoa sana yule.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…