mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 917
- 1,997
Waswahili wanasema "Msafiri Kafiri" na "kuku mgeni hakosi kamba mguuni". Hii misemo yote inaelezea tabu na adha unayoweza kukutana nayo ukiwa safarini au ugenini.
Leo nimetafakari juu ya homa ya MGUNDA iliyoibuka Mkoa wa Lindi, nikakumbuka kisa nilichowahi kusimuliwa na marehemu Mjomba wangu mwaka 1995. Mjomba alimuoa shangazi mtu wa Nyasa, Ruvuma. Sasa walipofunga ndoa baada ya miezi kadhaa akampeleka shangazi kijijini Masasi kusalimia wakweze.
Huko ndio kisa mkasa kikaibuka Bwana. Walifika usiku usiku, asubuhi na mapema, Mama mkwe akamuuliza shangazi kama anakula Kima. Shangazi akajibu hana shida anapenda sana kima. Baba mkwe alitoka Nae Asubuhi na mapema na bunduki yake kwenda porini. Mjomba na Shangazi nao wakaondoka kwenda kusalimia ndugu na jamaa pale kijijini. Waliporudi mchana wamekuta mama mkwe anababua nyama ya nyani/kima kwenye moto.
Mchana kufika ukapikwa ugali kwa nyani/kima. Unaambiwa kichwa cha nyani na meno yake yupo kwenye supu kaletwa mkekani. Unaambiwa shangazi kuona ile mboga akatapika hapo hapo mkekani kwa kichefuchefu. Ikabidi Mjomba awaambie kuwa huyu hali nyama ya nyani. Mama mkwe akajitetea mbona nimemuuliza asubuhi kama anakula Kima akanijibu anakula. Shangazi ndio akafafanua kuwa alijua nyama ya kusaga hakudhani kama kima ni nyani
Kusini bana kunalika vyakula vya ajabu sana, ukinusurika labda uwe Muislamu au Mkristo kwelikweli ndio hutokula hivyo vyakula vya ajabu. Nadhani serikali inawajibika kupeleka miradi ya ng'ombe, mbuzi na kuku kwa wingiiii ili kuwezesha wananchi kupata vitoweo muruwaa