Ushawahi kukuta nyumba kama danguro……….!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushawahi kukuta nyumba kama danguro……….!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 2, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna nyumba ambazo ukiangalia maisha ya wanaoishi ndani ya nyumba hizo huwezi kuzitofautisha na danguro. Hebu fikiria nyumba ambazo watoto wa kike wanaingiza marafiki zao wa kiume na kufanya nao mapenzi humo, iwe mchana au usiku. Watoto wa kiume nao ni kama hao dada zao nao huja na wanawake zao na kufanya nao mapenzi humohumo ndani ya nyumba.

  Lakini hata baba naye akipata mwanamke wa kupitisha naye usiku hujivinjari naye ndani ya nyumba hiyo hiyo. Kama ni mama, akiibua buzi lake huko atokako atakuja nalo na kufanya nalo mapenzi humo humo ndani ya nyumba ya familia huku watoto wakishuhudia. Aibu gani hii!Mara nyingi tabia hizi hujitokeza zaidi katika nyumba za mzazi mmoja. Inawezekana wazazi wameachana au mmoja amefariki, au huyo mzazi anaishi na watoto ambao alizaa kila kona na kuwakusanya hao viumbe wake na kuamua kuishi nao.

  Kwa sababu, kila mtoto amelelewa kivyake huko alikotoka au kwa sababu, baada ya mzazi mmoja kufariki au kuachana, aliyebaki na watoto alishindwa kuwalea vema na sasa wamegeuka nunda halisi.
  Sisemi nyumba zote zenye mzazi mmoja zinakuwa hivyo, hapana. Naogopa nitasakamwa. Nazungumzia zile nyumba za mzazi mmoja ambapo mzazi huyo kwa bahati mbaya au kwa hiyari yake bila kujua ameiharibu familia kimaadili.

  Bila shaka mtakuwa mnazijua familia za aina hiyo, angalau moja.
  Nyumba hizi ni kama nyumba ambazo ni mtaa humohumo ndani ya nyumba. Huyu anaingiza mtu wake chumba hiki na yule anaingiza mtu wake chumba kile. Kama kwamba ni watu majirani tu wanaoishi mtaa mmoja na hakuna mwenye haki ya kuuliza kuhusu maisha ya ndani ya mwingine. Kama baba au mama anafanya hivyo mbele ya watoto, unadhani atathubutu vipi kumkemea mtoto? Tena mtoto mwenyewe ameshaanza kuvuta bangi au kubwia ‘unga,' thubutu!
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  M-bado
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  sidhani kama ipo kwa tz yetu.
   
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mtambuzi! Haya bana,no comment.
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Sitaki hata fikiria the agony of reality..... Ni mbaya!
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Dingi, uko sawa! Niliwahi pata hgeli, baada ya miezi 2 akawa kachangamka haswaa. Siku ya off yake ya jumapili akasema anaenda kwa dadake wapi sijui. Saa moja usiku ananipigia,'dada, samahani naomba nirudi kesho manake bado niko kwa dada na naona giza lishaingia'. Nilijibu kitu kimoja tu, ukilala kwa dada yako, kesho kabla ya saa mbili uwe umeshakuja kuchukua vitu vyako! Nyumba yangu sio mzinga wa nyuki unaingia na kutoka utakavyo. Tunapanga ratiba na tunazifuatilia kuzikeleza.
  Huwa nashangaa sana watu wanaolala kwa 'watu' (sio wapenzi wao, ieleweke), ni kama kutoheshimu nyumba yako kama danguro!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nahisi labda wewe unaishi ughaibuni, kama ungekuwa unaishi hapa Bongo usingesema hayo
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mzee mwenzangu sijui mimi nina bahati mbaya, maana nimewahi kuzishuhudia familia za aina hiyo zaidi ya tano, ni aibu kwa kweli.
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  AshaDii, heshima kwako.
  Kusema kweli maisha ya aina hiyo ni aibu kubwa na inatia kinyaa. Mimi nimewahi kuishi maeneo ya Mwananyamala na Buguruni miaka ya 90. hayo niliyoyaeleza ni mambo ambayo niliyashuhudia na sio kuelezwa. kwangu mimi mtu niliyetokea kanda ya Mashariki ilikuwa ni jambo la kushangaza kidogo, ingawa kwa wenyeji wa pale hilo lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa.
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  "Nyumba yangu sio mzinga wa nyuki unaingia na kutoka utakavyo."
  Hilo neno limenifanya nicheke.....................Mwanangu una visa wewe!
  Kuna jambo ambalo pia sikulizungumza kwenye uzi huu, nalo ni hili la ma-house girl wetu, kuna baadhi yao ukitoka na mkeo au mumeo kwenda kazini, nao huigeuza nyumba kuwa danguro, utakuta wauza mchicha, wauza samaki na wenye kuuza bucha humalizia shida zao humo, ili dada aweze kupata discount ya bidhaa ili kupata cha juu kwa ajili ya kununulia skin jinzi.
   
 11. c

  christer Senior Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kidogo yanitokee kwangu wadogo zangu wakike(graduates)walianza kutoka na kurudi wapendavyo nisipo kuwepo hata dada hawamuagi . nika pachimba nikasema asiyependa kufata masharti mlango uko wazi nampa namba ya dalali. sasa kila mtu adabu na utiii.
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi nimejikaza nikapanga ka nyumba kangu kana bedroom mbili kuna ndugu zangu watoto wa mauncle na mamamdogo wapo chuo wengine sijui wapo wapi wakaja wakataka kufanya makazi nikawatoa baruti,ningekubali tungekuwa 7 eti
  nikawaambia kwangu sio hosteli
  watu si wangeona ni danguro jamani?
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hahaha, kama visa ntakuwa nimerithi kwako!
  Hgeli wangu ana clear instructions, hana ruhusa ya kupata mgeni bila clearance yangu, na ni lazima niwepo! Jumapili yote ni off day, na kama ana mgonjwa tunafanya utaratibu aende tena na ma-hotpot ya misosi kabisa!
  My maid doesn't shop for me, no!! So hakuna mchuuzi anaeniletea kitu na kuna limit ya access ya nyumbani kwangu! Naenda sokoni mwenyewe sana akibahatisha chumvi iishe na nisijue ndo atanunua dukani!
  Hayo maisha ya kama danguro ni sign ya disorganised life! Kuna dada alitelekezwa na celebrity flani, jamaa kaenda ng'ambo kamuacha na binti, sasa hivi she is in form 3 nadhani. Kila siku mama anarudi na 'uncle' na kumuambia mwanae 'muambie uncle asante, ndo kakulipia ada. Babako wala hajali, anauza jina tu!'. Nikikaangalia kale kabinti, nachoka manake lazma ataishia mulemule, kama ma-uncles hawatamuwahi! Sad indeed!
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ofcoz kama hakukuwa na sababu nzuri ya kuja kubanana nao hapo ulikuwa sahihi. Lakini danguro haina maana ya kuishi watu wengi sehemu moja. Danguro ni nyumba isiyo na nidhamu, at least machoni pa watu. Inahusika na umalaya na ubadilishaji wa wenza bila kujali.
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  daaah nyumba moja wasichana saba ukizingatia tunarudi usiku sometimes hadi saa kumi usiku watu wasingetuelewa nakwambia
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mie visa vyangu huwa wanarithi watoto wa kiume tu, sasa sijui wewe hiyo mirathi umeipataje.............!? LOL
  Naomba nikupongeze kwa namna ulivyoweza kukopi na kupesti tabia zangu, si unajua wakati nawalea nilikuwa nawashikisha adabu na henzirani pale mnapotoka nje ya mstari. nilikuwa sina mchezo na ndio maana mmekuwa na adabu na hishma mpaka ukubwani.

  Kuna jirani yangu watoto wake wa kike hawa adabu kabisa, unaweza kukuta usiku wazazi wamelala wao wako nje kibarazani eti wanapiga stori na washkaji zao, kumbe wanafanya Malabuku viambazani mwa uzio wetu, tukiamka asubuhi tunakuta vifanyio kila kona. kuna siku huyu mdogo wako Ngina aliniuliza ni nani anatupa vile vifanyio pale nje kwetu nikamwambia ni watoto wa majirani wasio na staha na miili yao. lakini alipotaka kujua zaidi, maana Ngina haishi udadisi nikamkata kalma na kumtaka akajifungie chumbani kwake afanye home work.
   
 17. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mi nshaona kitu hiki jamani, nyumba wanaishi brothers and sisters. Kaka mkubwa kaoa, wengine hawajaolewa. Dada analeta bwanake daily na wakaka pia wanaleta mademu zao daily, na hao mademu wanapika na kupakua. acha hayo, wanapeana zamu kufanya ngono, yani nyumba ni kweli inakuwa danguro!
   
 18. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  We kaka acha tu, hata kusema nashindwa. Kifupi nimetimua mischana yote. Ukiwabana njia hii, wanabuni nyingine almradi tu walete mijanaume yao nyumbani kwako, waiweke sitting room kwako waipikie chai na chakula, walale nayo vyumba ambavyo havifungwi. Usiku pia usipoangalia mijanaume inapenyezwa inalala hapo hapo, we watoka asubuhi unakimbia kuwahi foleni unaacha njemba limelala ndani huna habari. Ama usiku wadhani wamelala wote wapo ndani, kumbe kuna walioisharuka hawamo wanarudi alfajiri. Hiki kizazi cha www.com mie hamu sina. Hata la kuongeza nimekosa.
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Terms and conditions ndo zinapoapply sasa. Lazma kila anaechelewa kurudi home aseme anachelewa wapi na kwa nini. Unless ni shuleni. Kurudi saa kumi alfajiri once in a while sio mbaya na itolewe taarifa pia. Ila ungehitaji matron,lol! Anytime u need my service holla me, nadhani wasiofit wataondoka wenyeewe!
  Self discipline ni muhimu kwenye maisha bana!
   
 20. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Heshima yako baba,hizi nyumba zawezekana zikawepo kbs,
  Dah!hii habari imenikumbusha nyumba moja niliishuhudia maisha yake hata sijui ndio ndanguro au nn?

  Kuna shost wangu alikuja huku kikazi ili kubana hela akafikia kwa shangazi yake baada ya siku 2 akapata homa akawa ameshinda nyumban kumbe pale kuna wadada 3,wawili wana watoto 2 kila mmoja na huyo shangazi na ndugu wengine 2 wadada,nikawa nimeenda kumjulia hali kwa mda wa nusu saa niliokuwa pale nikagundua haya;

  Ile nyumba haipikwi kila mtu anajitegemea au anajipikia,mwingine akinunu sukari mwingine vitafunwa akizuba kidogo mwenzie keshaviiba,huku mama analalamika sabun yake kuna mtu kachukua,yani hapo wanaishikm cjui km nn ni vurugu kuibiana,mpaka viatu mwingine anatoka navo,watoto wanapigana mama zao wanagombana wanatukanana matusi ya ajabu,yani nilihis kuchanganyikiwa,

  Ikabidi nimuulize shost anaishije pale akasema naye anashangaa kwani huwa anatoka asubuhi na kurudi usiku yale hakuwahi kuyaona mie nikamwambia najihic siko sawa narudi zangu kwangu akaingia ndan na kuchukua kibegi chake akaaga tukaondoka naye,yaan nilibaki na mshangao na kutoelewa km kuna familia za maisha ya vile!!!
   
Loading...