Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

masai dada,

Nimesoma maoni ya wote humu, naona wameegemea upande mmoja. Wengi walotoa maoni inaonesha aidha ni akinamama wenzako au ni vijana ambao hawajaoa na kama wameoa basi ni ndoa changa kama yako ila bado kuonja subiri za ndoa kama unazokumbana nazo.

naomba nikuhakikishie kuwa hata kwa mumeo bado anaonja subiri na anakupenda, la sivyo alivyokupapasa isingesimama! Pili kuwa na mtoto was akati huo huo hana biological mother ndani ya nyumba hiyo ni mtihani kwetu hasa mbele ya mama wa kambo. Kulala naye anajitahidi kumweka karibu naye hasa mtoto wa Kike. Unatakiwa uwape Uhuru hata kama roho inakuuma.

ninavyojua wewe ni wa Mlimani (sijui kama ni sahihi), uzoefu wangu ni kuwa huwa mnajisemea tu ila sie vyasaka huwa tunaingiza kifuani na tunatafuta jinsi ya kuwarudi. Uloyasema mumeo anakupenda ila kuna vitabia asovipenda na una mdomo sana! Hivyo anakuchapa kwa vitendo (he is not exceptional, we normally discipline our lovers kwa njia hiyo Mwalimu Masai Dada). Tumeyapitia na bado wengine tunasukuma hivyo.
 
Pole masai dada, changamoto yako pamoja mimi ni mwanaume imefuta furaha yangu ya leo. Huwa najiuliza kama umepata mke anayeheshimu na kukujali unapata wapi kiburi cha kumliza? Mungu hatamwacha salama mtu wa aina hiyo na mda wowote mmeo atakupigia magoti maana Mungu huwa karibu na wamliliao.

Nakuomba usifikirie kusaliti pia usifikirie kulipiza bali mwachie Mungu. Kula na kipofu hakukuondolei heshima yako. Akihitaji penzi mpe maana ni haki ya ndoa, cheka nao walionuna au kukuumiza, cheka nao wanaocheka nawe. Kwa kuwa huu ni mwaka mpya Omba sana Mungu atende jambo katika familia yako na mtoto wa kufikia mpende sana kama mwanao.

Natamani sana Mungu akujibie na naamini atakujibia.

Wanaume tunaosoma uzi huu plz usimfanyie ukatili mwenza wako kisa anakupenda.

Huwa nampenda sana J wangu hatajutia kuwa nami.

Masai dada Mungu hajakuacha mpweke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
masai dada,

Pole kwa mapitio hayo ndugu yetu. Mwanaume akifikia hatua hiyo hakika lazima kuna kitu anajivunia kama mbadala, na hapo hata huruma na wewe hana tena. Nakuomba utunze nyaraka zako zote za huo mkopo uliochukua kwa ajili ya kusaidiana kujenga hiyo nyumba pia kusanya risiti zote za mapato ya hela zako kisha zi scan na uzitunze kwenye email yako au popote unapoona ni salama, ili siku ukiamua uwe huru na hayo manyanyaso basi kaombe shauri mahakamani mgawane hizo mali zenu.

Hii dunia imeumbwa ili tufurahie na ndoa zimekuja kama makubaliano ya kuheshimiana na kujaliana kiubinadamu ndani ya familia. Sasa kama mmoja wapo akikengeuka na akaamua kutesa hisia na moyo wa mwenzake basi hakuna haja tena ya kuendelea na makubaliano hayo. Nijuavyo mimi huyo mwanaume alipaswa akuheshimu sana,maana umejitoa mhanga kukopa hela kwa ajili ya maendeleo ya pamoja pili alipaswa akuheshimu maana tayari alishazaa kabla ya wewe kukuweka ndani na bado umemkubali mwanae.
 
Pole masai dada, changamoto yako pamoja mimi ni mwanaume imefuta furaha yangu ya leo. Huwa najiuliza kama umepata mke anayeheshimu na kukujali unapata wapi kiburi cha kumliza??? Mungu hatamwacha salama mtu wa aina hiyo na mda wowote mmeo atakupigia magoti maana Mungu huwa karibu na wamliliao.

Nakuomba usifikirie kusaliti pia usifikirie kulipiza bali mwachie Mungu. Kula na kipofu hakukuondolei heshima yako. Akihitaji penzi mpe maana ni haki ya ndoa, cheka nao walionuna au kukuumiza, cheka nao wanaocheka nawe. Kwa kuwa huu ni mwaka mpya Omba sana Mungu atende jambo katika familia yako na mtoto wa kufikia mpende sana kama mwanao.

Natamani sana Mungu akujibie na naamini atakujibia.

Wanaume tunaosoma uzi huu plz usimfanyie ukatili mwenza wako kisa anakupenda.

Huwa nampenda sana J wangu hatajutia kuwa nami.

Masai dada Mungu hajakuacha mpweke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu namuheshimu sana mume wangu
..ukija nyumbani most of tge time utanikuta jikoni nampikia sibweteki nazitafuta hela na mtoto wake ninampenda anajua hilo.
Nitamuangalia tunipo siku atahitaji msaada wangu
 
Pole kwa mapitio hayo ndugu yetu. Mwanaume akifikia hatua hiyo hakika lazima kuna kitu anajivunia kama mbadala, na hapo hata huruma na wewe hana tena. Nakuomba utunze nyaraka zako zote za huo mkopo uliochukua kwa ajili ya kusaidiana kujenga hiyo nyumba pia kusanya risiti zote za mapato ya hela zako kisha zi scan na uzitunze kwenye email yako au popote unapoona ni salama, ili siku ukiamua uwe huru na hayo manyanyaso basi kaombe shauri mahakamani mgawane hizo mali zenu. Hii dunia imeumbwa ili tufurahie na ndoa zimekuja kama makubaliano ya kuheshimiana na kujaliana kiubinadamu ndani ya familia. Sasa kama mmoja wapo akikengeuka na akaamua kutesa hisia na moyo wa mwenzake basi hakuna haja tena ya kuendelea na makubaliano hayo. Nijuavyo mimi huyo mwanaume alipaswa akuheshimu sana,maana umejitoa mhanga kukopa hela kwa ajili ya maendeleo ya pamoja pili alipaswa akuheshimu maana tayari alishazaa kabla ya wewe kukuweka ndani na bado umemkubali mwanae.
Kiasi cha hela ninachokipata kwa mwezi na sina pa kupata popote ni Mungu tu naona ananisogeza.
Roho inaniuma kwa kiwango kikubwa sana.
 
Pole saana mdada, si mtaalamu wa mambo hayo lakini common sense unanipa haya ya kusema.

1. Naona kuna kama hali ya mashindano, hata kama siyo moja Kwa moja basi hata hiyo ya wewe kudai fair treatment mwenzako analiona kama unashindana, sasa anakukomoa.

2. Huenda mama wa mtoto wa zamani ana mkono wake, au kuna mwanamke mwingine nje anamfanya asijisahau na akutreat vibaya, labda utaondoka mwenyewe. Inaweza ikawa hivi hivi tuu ujinga wake au hata kimazingara pia.

3. Ama kuna uwezekano ndugu zake flan hawakukubali, sasa nayeye amekuwa jinga jinga anayekosa ku analyse mambo.

4. He is short sighted, yaan ukute hapo umechangia ujenzi, na sasa huna hela huna ujanja, anajiona amefiiika, hajui kuwa hiyo nyumba siyo yake pekee.

Nini cha kufanya??

1. Huyo ni mumeo never give up on him, yaani weka akilini kwako kuwa kitakacho kutoa hapo labda roho itoke. Wewe ndo mtu wa kurekebisha yoote hayo. Hilo uwe nalo akilini.

2. Analyse Mali zote mlizochuma pamoja, ikiwepo na hiyo nyumba, register malalamiko official, iwe ustawi wa jamii, kikao cha ukoo, popote pale tafuta ushauri, yaani ijulikane kuwa mmejenga pamoja na kuwa mkopo wa mshahara wako unakatwa Kwa sababu ya Hilo, wazazi wako waliokusomesha wajue Hilo, mshenga ajue Hilo, yaani Kwa vyovyote vile ajue kabisa hicho anachojiaminisha ni ndoto. Mtoe upepo.
Usiogope vita kuongezeka lakin nakwambia akijua yote hayo atapunguza speed.

3. Ishi kwako bila kujali upendo wake, pika chakula, fanya majukumu yoote ya mke, omba hela za matumizi, ukinyimwa basi. Ila jishushe, usijinyenyekeze kiviile, itafika mpaka watoto wataona unanyanyaswa ila utafanyaje ndo zamu yako ya ups.

4. Punguza matumizi binafsi ili usiteseke Sana, kama unaweza kuishi na nywele fupi kata Tu, kwenye vikoba sijui kitchen party unaweza kujitoa au kujipunguza saaana, dunia haitakuelewa kirahisi lakn kwakuwa unajijua utakuwa na amani moyoni.


Ukiweza hayo japo for 4months utaona anajirudi mwenyewe. Ila ukiishi kama vile hayo anayokufanyia siyo kweli basi utateseka kisiri Siri Hadi utajikuta ume give up kirahisi.

Pole , nitaendelea hapa ama inbox

Note: hao watoto wote wanakutegemea uyakavyosimama wewe, bila wewe wanapotea wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Suna neno mkuu nimeuchukua ushauri wote
 
Daaaaahh umeongea kwa hisia Sana hadi nimeumia kwa kweli pole Sana Dada angu

Ninacho weza kukwambia ni kwamba huyo ni mmeo hivyo usifikilie kumsaliti ila fikilia kumuweka karbu Zaid na Zaid haijalishi itakugarimu kiasi gani kwauda wako na kwa hisia zako but hakikisha una fanikiwa katika hili


Unaweza kuomba nafasi ya kutoka out ukiwa wewe na yeye tu hapo nenda kamuoneshe jinsi gani una mpenda na hauko tayar kumpoteza mpe mapenzi kwa hisia za ndani Sana shoe him how worth he is then baada ya yote mwambie you need a peaceful life na yeye ndie mwenye peaceful life kwako hivyo asikuumize tena


Pia katika out yenu akiwa kwenye mudi nzuri ongea nae juu ya future yenu kuhusu mwanao na huyo na mwanae yule mwambie wote ni wake na wote wanajua yeye kama baba yao hakuna mwingine Zaid yake hivyo ni bora kujenga future sawa kwa wote




Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ndo solution..kwa binadamu wa kweli ukifuata hii njia lazima itamwingia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
masai dada,

Inaumiza ila kiukweli huyo mwanaume hakupendi na hana mpango wowote na wewe. Cha msingi fanya kila jitihada uanze kujikomboa ila kuanzia sasa na kuendelea jiondoe kabisa kuwa sehemu ya maisha yake. Upo uwezekano mapenzi yapo kwa mama wa mwanaye. Chukua hatua mapema sana na mwaka huu jitahidi uwaze na upambanie hilo moja la kijikomboa.
 
Huu usemi huwa unanichekesha..
Hivi ukipewa nafasi ya kuwa mwanamke unaweza kunyenyekea hata robo siku?
there is a difference,kuna mwanamke hata uwe mkorofi vipi huna uwezo wa kumpiga,utaanzia wapi labda uwe tahira,kuna mwanamke hata kumcheat tu unaumia sana n kujuta sana,sasa kwa lishankurumbembe kama wewe lazima utandikwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom