Habari zenu wandugu..
kuna wifi yangu nimeona jina lake ameitwa kwenye interview tarehe 7 huko dar wizara ya afya na ustawi wa jamii..Ndo kwanza amejifungua jana tena kwa kisu sasa jamani naombeni kuuliza anawezaje kuipata haki yake ya kufanya hiyo interview kwa baadae maana kwa hali aliyonayo hataweza kwenda kwa tarehe hiyo.je kuna namna yeyote ataweza kusaidika au ndo imetoka hana lake...Namuonea huruma jaman huenda ni bahat yake maana amefight sana kutafuta hata kuitwa kwenye interview sasa naona kama tumaini halipo naogopa hata kumwambia maana naona atapata presha akijua hatokwenda.
wenye uzoefu jamani nisaidieni angalao nimtie moyo.
Mi nafikiri ana haki ya kusikilizwa na kupangiwa siku nyingine kutokana na hali aliyonayo, cha msingi tafuta namna ya kuwasiliana na watu wa utumishi kuona namna watakavyoweza kumsaidia, wao ndio wanaweza kukupa jibu sahihi.
7 june, nyuzi atakuwa ametoa kama hayupo mbali sana na dar aje kuna dada yangu aliitwa interview ya oral ana wiki toka ajifungue nae kisu sababu ni dar akaenda na amepata kazi, alianza kazi mtoto ana mwezi mmoja