segere
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 539
- 262
Tumeacha kwa sababu zisizokuwa na msingi sikuona sababu ya yeye kuniacha kama kweli ananipenda lakini! Lakin ckutaman aniache
kama alikuacha kwa sababu tu alipata binti mwingine sidhani kama una sababu za kuendelea kumng'ang'ania kwani kumbuka wakati atapogeukia kwako huyo mwingine naye ataumia, hivyo kwa moyo wa upole mwache aende tu na zaidi endelea kumwombea akafanikiwe huko aliko. Kwa upande wako naamini utaweza kupita kipindi hiki na hatimaye siku za usoni utaingia kwenye mahusiano mapya na tena matamu zaidi ya haya yalopita ambayo huna budi kuyapa kisogo, na ashukuriwe Mungu aliweka macho mbele na sio kisogoni, lakini kabla hujaingia kwenye mahusiano mapya jaribu kurekebisha mambo kadha wa kadha, pitia mipango yako na ile iliyo ya msingi ikamilishe kabisa kisha ndo uanze kutazama namna gani utaingia tena kwenye hili game ambalo halinaga sare, huku ni kufungwa au kufunga..