Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu

Private Pasua kichwa sanaaa,niliacha kazi private mshahara 1m nikaenda serikalin mshahara laki 5 napata baada ya miez sita mwajir kapata mapigo mengii sahv mshahara unalipwa kwa mbinde kwa waliobak na umepunguzwa sababu hali sio nzuri na kupata tarehe 55 au 60 kawaida

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Baki kwenye uhasibu. Somea CPA. Timiza ndoto zako.
 
Ushauru wangu

Fanya kazi hapo private lkn fungua biashara yako binafsi haraka sana.
 
Uhasibu unakupa fursa yakukutana na watu wenye pesa na waliofanikiwa, ila uwalimu unakukutanisha na watu wenye msongo wa mawazo na waliokata tamaa.Sasa ni wewe uamue,uwe karibu na anayenukia pafyumu au uwe karibu na anayenukia jasho.
 
Ushauru wangu

Fanya kazi hapo private lkn fungua biashara yako binafsi haraka sana.
Haraka sana eti????[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Miezi sita 1.5 mil kama una familia sio hela ya kudhani itabadilisha maisha yako mzee yani na vile private wanakuwa busy na kazii utajikutaa unamaliza miezi sita huna hata mia na Omba sana wakuongeze mkatabaa..
 
Best comment ever, Kuna wengine wanakushauri uendelee hapo wakati wao Ni watumishi wa serikali na hawataki kuachia nafasi, mkuu nenda serikalini hizo private company unafanya mwez mmoja unatukuzwa au kampun inafilisika naww ndo serikalin huwei Tena ingia kwa sabab ulishachaguliwa uka kataa nafasi.
 
Lakini mtoa mada amesema kuna option ya kuongeza mkataba
 
Maisha yana mengi anaweza pia kufa kabla ya kupokea kiinua mgongo.
 
Mkuu fanya hivi nenda kwenye ualimu serikalini kaa mwaka mmoja ukisha thibitishwa kazini ka wilikilishe cheti chako cha uhasibu na uombe kubadilishwa muundo utafanyiwa re categorization kuwa mhasibu Kuna uhaba wa wahasibu kwny halmshauri nyingi achana na iyo kazi ya mtu binafsi job security ni 0
 
Lakini mtoa mada amesema kuna option ya kuongeza mkataba
Yaan ijulikane kwamba kazi yangu sio ya leo wala kesho ni miaka na miaka nikiperfom vzr nitaedelea nayo mpaka hata nistaaf. Na walivyonichukua moja ya swali wameniambia hatutaki ambae tunamuajiei leo kesho anaondoka. Tunataka mtu wa kukaa mda mrefu. So ni mm tu.
 
Kaka hiyo 1.5 nimeanza nayo tu. Huko mbele mambo mazuri sana. Sio kwamba ni fixed salary. Noo baada ya probation nitapewa contract nyingine na salary nyingine
 
Kama ni jinsia ke nenda ualimu, kama ni jinsia me baki uhasibu.

By the way kama ushakusanya mtaji kiasi ambao unaweza kuanzisha biashara kwa sasa nenda ualimu huku unasimamia biz au mradi wako.
 
Kama ni jinsia ke nenda ualimu, kama ni jinsia me baki uhasibu.

By the way kama ushakusanya mtaji kiasi ambao unaweza kuanzisha biashara kwa sasa nenda ualimu huku unasimamia biz au mradi wako.
Mimi ni Me. Nashukuru kwa ushauri wako
 
Nina malengo makubwa sana na ninachotaka ni capital nifanye mambo yangu binafsi baadae kidogo
Sikushauri uende kwenye ualimu .

Utakuja jutia baadae[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kaka mm nipo single. Matumizi yangu hata hiyo 500k haiishi, sinywi pombe wala sina madem. Ila nendelea kupata shauri mbalimbali then before 14 days kuisha nitakuwa nimepata jawabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…