Ushauri wenu ni muhimu members

kalua 89

Member
Sep 22, 2020
54
30
Kwa uwezo wa aliye juu ni imani yangu kuwa wote tuko salama.

Wakuu nimekuwa member kwa miaka kadhaa sasa japo sikuwa nimejisajili lkn nimekuwa nikisoma mada mbalimbali za wadau na ukweli ni kwamba nimejifunza na kuyajua mengi kupitia JF.

Sasa nije kwenye mada, nimesoma diploma ya mambo ya natural sciences miaka 5 iliyopita. Baada ya msoto wa muda huo wote bila kupata ajira na ushindani wa ajira kuwa mkubwa kulingana na kipindi tulichopo kwa hii miaka 5 sasa wazo la kurudi shule ndo lipo kichwani mwangu ila changamoto ni kozi gani nitaenda kusoma ili kukidhi au kuendana na soko la ajira katika nchi yetu kwa sasa.

Japo navutiwa sana na speech ya Rais Magufuli kwamba serikali imejenga vituo vya afya zaidi ya 60 na hospital kadhaa na lengo ni kufikia kuwa na hospitali kila wilaya ifikapo 2025 hivyo nikafikiria kuwa sehemu pekee pakuponea ni kwenda kusoma kozi zinazohusiana na afya lkn kulingana na vigezo nilivyonavyo kozi pekee ninayoweza kusoma kwenye kiwango cha shahada ni Biotechnology & Laboratory Sciences.

Sasa wakuu naombeni ushauri wenu juu ya hii kozi kwenye upande wa afya kama ina soko au nikaanze upya kwa kwenda kusoma diploma nyingine kwenye mambo ya afya? Na ni kozi ipi ambayo ina soko kwenye afya ukianza na Crinical Medicine, Medical Laboratory, Pharmacy nk.

Natanguliza shukrani wakuu ila ushauri wowote hata nje ya hayo niliyoyasema pia utapokelewa.
 
Back
Top Bottom