Ushauri wenu muhimu sana, maana nnakoelekea siko.

Ushauri wenu muhimu sana, maana nnakoelekea siko.

Samboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2011
Posts
5,417
Reaction score
8,047
Heshima kwenu,
Nina hali ya upweke wa hali ya juu sana umenitawala kwa kipindi cha miezi ya hivi karibuni,
Muda wote nawaza tuu mambo ya ajabuajabu,
Nina watoto watatu na mwanamke ninaeishinae na wawili wa nje ila huyo mmoja mama yake nimemkatia tu mawasiliano ghafla mwezi wa 3 huu sipokei wala kujibu sms zake, huyo mwingine tunawasiliana mara chache sana,
Akili yangu inanitaka kuishi peke yangu tu kitu ambacho kimenifanya nianze kuwapotezea ndugu zangu wakiwepo wazazi pia, nikiona simu au sms zao hata km ni salamu tu nakasirika kupita maelezo,

Natamani kuikimbia familia kiujumla au nimtafutie mke wangu sababu nimfukuze na watoto, hapa tuna mwezi haziishi siku 2 sijamfokea ovyo kitu ambacho hata yeye analalamika nimebadilika,
Kupitia hali hii nimelazimika kulipa tena kodi ya miezi sita wakati mwezi wa 7 ilkua tuhamie kwenye nyumba yetu ambayo ilishakamilika kila kitu na hilo limesabisha mke kutonielewa maana sina sababu za msingi.
Saa ingine nawaza niiuze ili nimkere tuu wife, gari nimelificha kwa jamaa angu nikamdangaya kuna jamaa alikua akinidai nikemwachia kupunguza deni.

Nawaza tu nikae chumba changu kimoja nijifungie huko niishi mahali ambapo hamna ndugu wala jamaa anaenifahamu
Kuna saa nakaa mahali nawaza tu jinsi ya kutekeleza huo mpango wangu, lkn saa ingine hali inakua kawaida nabaki tu nashangaa kwanini nawaza ujinga huo na kuupuuzia lkn kadri siku zinavyozidi hiyo hali inazidi na naanza kutekeleza moja baada la jingine,

Hatuna historia ya ugomvi mi na mke wangu, nikiwa nae najiuliza kwanini namuwazia mabaya wakati hatujagombana, watoto kiujumla nmeanza kuwachukia kwa mbali, sichezinao tena, naweza fika home wakanisalimia nikiingia ndani wao wanakaa sebuleni wananisubiri(ndio ilkua kawaida yetu) na mimi nakaa ndani hadi wakienda kulala ndio natoka ndani.

Hapa nimeanza kuandika tangu saa 12 asubuhi najiwa na hali kutotaka ushauri napotezea, kila nikiandika kidogo naacha,

Nahisi kabisa kuna roho ya ukatili inaninyemelea kwa kasi sana, ninavyojijua na ninavyowaza haviendani kabisa,
Ushauri wenu muhimu sana wakuu natokaje hapa na hii hali ya kuwaza kua mpweke tu mda wote.
 
Pole sana, kama mkeo ni mama wa nyumbani mtafutie ajira au biashara aendeleze familia pindi utakapo kufa. Kuna roho ya umauti inakunyemelea na mkeo ndo ataeiendesha familia yako. Ukishamuacha mkeo kwenye halikauki ya kuiendeleza familia basi tafuta chumba change kupanga ila kabla tafuta kazi mahali pengine na usiwaambie hata wafanyakazi wenzio kisha hamia chumba chako, kazi mpya na simu zako ziache nyumbani kwa mkeo maana yake unanunua line mpya na utakuwa na mawasiliano na utaowataka ama laah usiwe na simu kabisa.

Dalili za kuikimbia familia, maisha yamekuwa magumu kiasi kwamba ukifikiria ada za watoto kuwa kuwatunza wazazi chakula nyumbani umeme maji vote wewe hata wewe hujinafasi.

Na ukifanikiwa kukaa chumba chako utajiua humalizi mwaka huu.

Tina yako au poa yako, jiulize ni kitu gani ukifanya kinakupa tabasamu furaha na amani ya moyo....

Chukua hata mkopo safiri kwenda mahali unapotamani kwenda fikia hotel hudumiwa tuma pesa nafsi yako ifurahi. Actually you need a leave out of home but not alone.

All the best.
 
pole njoo huku nilipo kwa muda ukirudi utakua sawa hyo ni athari ya kukaa muda mrefu bilashughuli ya kufanya na kutokua na marafiki wapya
 
Sio dalili nzuri hizo, kama hutojiua ili ukakae kaburini peke yako basi kuna athari ukaizuru familia yako ili ubaki peke yako,unahitaji ushauri wahi kwa wataalamu kabla mambo hayajawa mabaya zaidi, pia Jenga tabia ya kuwa unamshirikisha Mungu katika mambo yako mengi ili akufungue kutoka katika hiyo minyororo ya shetani ulikonasa kwa sasa!!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Israel asha mark Sura yako anasubiri kubofya kitufe cha DELETE
 
Yawezekana kuna kitu kinakunyima amani ndiyo maana wafikiria yote hayo.
Jaribu kutafuta mzizi wa tatizo

Usiwe unakaa pekeyako muda mrefu maadam umeshajua kinachokusumbua ni upweke jaribu kukaa na watu/mtu wako wa karibu.
Ongea nao,waeleze yanayokusibu,wakati mwingine kuongea ni tiba.

Kwa hali uliyofikia si nzuri maana waweza fanya jambo ukaja jutia baadae.
Tafuta daktari wa saikolojia waweza pata ufumbuzi.

Mshirikishe Mungu wako.
 
UNA JINI MKUU, NENDA KASOMEWE ARAKA, USICHEZE NA FAMILIA, FAMILIA WAZAZI NA UKOO WAKO NI MUHIM SANA
 
Pole sana, kama mkeo ni mama wa nyumbani mtafutie ajira au biashara aendeleze familia pindi utakapo kufa. Kuna roho ya umauti inakunyemelea na mkeo ndo ataeiendesha familia yako. Ukishamuacha mkeo kwenye halikauki ya kuiendeleza familia basi tafuta chumba change kupanga ila kabla tafuta kazi mahali pengine na usiwaambie hata wafanyakazi wenzio kisha hamia chumba chako, kazi mpya na simu zako ziache nyumbani kwa mkeo maana yake unanunua line mpya na utakuwa na mawasiliano na utaowataka ama laah usiwe na simu kabisa.

Dalili za kuikimbia familia, maisha yamekuwa magumu kiasi kwamba ukifikiria ada za watoto kuwa kuwatunza wazazi chakula nyumbani umeme maji vote wewe hata wewe hujinafasi.

Na ukifanikiwa kukaa chumba chako utajiua humalizi mwaka huu.

Tina yako au poa yako, jiulize ni kitu gani ukifanya kinakupa tabasamu furaha na amani ya moyo....

Chukua hata mkopo safiri kwenda mahali unapotamani kwenda fikia hotel hudumiwa tuma pesa nafsi yako ifurahi. Actually you need a leave out of home but not alone.

All the best.
Mke wangu nimemfungulia biashara siku nyingi tu sio mama wa nyumbani,

Maisha niliyonayo kiujumla sio mabaya ni ya kawaida tu, nna maduka mawili ya mtaani moja ndio yupo wife na mimi nafanya kazi,

Kiukweli sioni ninachokiihitaji ili niwe na furaha zaidi ni kuwaza kua peke yangu lkn najiuliza kwanini nifanye hivyo? Ili iweje? Sipati jibu na hapo ndio nashindwa kuelewa kwanini nawaza hivi ilhali sipati furaha.

Kuchukua mkopo kwa kweli hapana, wala sina shida ya hela kiasi kwamba siwezi kwenda jificha mahali nkatumia, yaani natamani tu nifanye kitu cha kushangaza ndani familia yangu, ndio maana sijawaza kuondoka tu bila kufanya chochote.

Asante kwa ushauri, natamani sana hii hali initoke ila nahisi kila leo ndio inazidi kuota mizizi
 
Back
Top Bottom