Ushauri wenu kwangu nifanyeje juu ya huyu dada.

Ushauri wenu kwangu nifanyeje juu ya huyu dada.

Mudundo

Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
38
Reaction score
9
Vipi wadau? Naomba ushauri wenu. Nilianzisha uhusiano na dada mmoja ambaye nilipomtongoza alinijibu kuwa hana mpenzi wala rafiki wa kiume. Basi tukahidiana kuwa tusifanye mapenzi mpaka tuoane kwasababu tuanze kujipanga kwanza na tumuogope MUNGU. Dada huyo nilimsaidia kwa mapana na marefu hata alikuwa hana simu nikamnunulia ilimradi tusalimiane. Nilimpeleka hadi kwa wazazi wangu iliwajue kuwa niko na mchumba ni yeye. Ilifika takrban miazi kumi na moja hivi. Hivi juzi kila nikimpigia simu naambiwa mteja hapatikani kwa sasa! Basi nilimjaribu kumpigia lakini simpati kwa simu. Mara nikapigiwa simu na jamaa akaniambia hii namba nimepewa na CLARIS. Halafu jina hilo ni la huyo mchumba wangu, lakini sikutilia maanani sana kwa sababu wenye majina kama hayo ni wengi sana. Lakini nikimpigia simu huyo demu wangu si mpati. Ndo nilipomvutia waya huyo jamaa nikamwambia hebu mpe simu huyo CLARIS ni mjue ni yupi. Alipompa hiyo simu, nikasikia hiyo sauti ni ya huyo mchumba wangu! Akaniambia mimi tayari nimeshakwisha kuolewa tayari! Hapo nikaanza kughafilika juu yake nikawa simuelewi. SASA NAOMBA USHAURI WENU NIFANYEJE JUU YAKE.
 
Kuna la kufanya tena wakati ashakuwa mke wa mtu? Hata kama hajaolewa, inaonyesha hakutaki tena.. Achana nae usije weka "kabang" yako rehani...
 
We nawe...
Haya kamlazimishe kuwa na wewe basi.
 
hivi siku hizi watu hawaelewi ama ni wabishi .....? ushaambiwa kaolewa tayari afu unakuja kuuliza ufanyeje....?....ni kwamba umeshindwa kabisa kujua kwamba hapo huna chako tena.......endelea na maisha yako.....
 
Mkuu kuna uzi nmeanzisha jana kua nataka kuoa mzungu,watu hawakunielewa,..:wanawake wa kiswahili mi mapimbi na waliojaa tamaa na wasio kua na future,huyo dasa achana nae hakufai tena.
 
Keshaolewa haina shida...cha kufanya ni kumwita mume wake shemej.
 
Imekula kwako mazima, ulikosea kutii masharti hasa la kupiga mujengo, yani kitaa unaitwa ----.
 
Shukuru MUNGU hilo limepita,anza maisha mapya ukiendelea kumuomba MUNGU akupe aliyewako.Mithali 16:4a na Mithali 19:14
 
Ulikuja pekee yako hapa Duniani kaka, kwann umlilie mtu ambae hayuko tayari kukulilia? ?? Get Busy Fanya Yako maisha yasonge,
Mademu ni Urithi tuliopewa na Mwenyezi Mungu so ww kama vp tafuta mwingine kaka
 
Yaani we unakaa na mwanamke mwaka hujatia saini wala kupiga muhuri!!!

Mwache aende kwa wanaume, we unadhani hawa viumbe hawana genye, au kwa sababu hawasemi wazi wazi? Sasa we unadhani huyo jamaa alikuwa anamshangaa akisubiri ndoa? Pole lakini ndio ujifunze,hawa wanawake zetu wanaanza mapenzi na miaka 12 we unamkuta kashakunwa vya kutosha unaleta story za tusubiri mpaka ndoa, atakubali tu asije onekana muhuni lakini deep down inside anasema kwaheri.
 
Mwambie hivi, NILIKUPENDA SANA LAKINI MUMEO KAKUPENDA ZAIDI..
Namwomba Mungu anipe nguvu nikusahau kabisa.
Happy new year Happy new love
CLARIS.
Halafu ubadili line.
^^
 
Mwambie ulipata mgao Wa escrow uko vzr atakuja faster
 
Ambacho huelew kitu gani wakat ushaambiwa ameolewa tayari
 
acha kujitoa ufaham kijana. Inamaana hapo hujaelewa alichokwambia au?
Kubaliana na matokeo,, mbona wanawake wapo wengi tu?

Halafu siku nyingne usikimbilie kupeleka wanawake nyumban eti unamtambulisha, wanawake wenyew hawaelewek unajiaibisha bure,,
 
Ashaolewa bas tafuta wa kwako huyo hakuumbwa mkae wote. Ni aina mojawapo ya usaliti na wala usimfanyie lolote baya huwezi jua Mungu kakuepusha na nini. Anza upya tafuta mke mwingne oa
 
Haina kwere hommie...move on...(if its real btw)
 
Ahsanten wadau sasa naona kichwa changu kimetulia kwa ushauri wenu. Nitamuomba MUNGU anipe wangu.
 
Tafuta mwingne na wewe wanawake wengi hivii au mdomo mzito??
 
Back
Top Bottom