Ushauri wangu wa bure kwa Zitto Zuberi Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu wa bure kwa Zitto Zuberi Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Apr 21, 2012.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Habari yako Mheshimiwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mahesabu ya umma, nakuandikia waraka huu kwa kuwa mimi ni mmoja wa huo umma ambao unasimamia mahesabu yetu. Nimefatilia hoja uliyoiwasilisha bungeni michango ya wabunge na hitimisho la hoja yako.

  Uliazimia kukusanya sahihi 70 kutoka kwa wabunge ili bunge liweze kupata firsa ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae waziri wetu mkuu (mtoto wa mkulima) ambae siku zote huwa hana majibu ya moja kwa moja zaidi ya kusema mimi naona mimi nadhani mimi naona tusubiri mimi mimi mimi mimi........................... nadhani wewe pamoja na umma wa Watanzania tumechoshwa na hizo "mimi nadhani" ila naona wingu mbele ya hoja yako (vifungu) na hasa mtafsiri vifungu (spika).  Wewe kama Mwenyekiti wa kamati na sio makamu wa mwenyekiti wa cdm ulitoa hoja kuwa wabunge wajipime lakini hawakujipima bali wameenda kushinikizwa kwenye kikao cha chama bila kujua hii nchi sio ya ccm wala sio ya chama chochote! wamefanya hivyo ili wewe uonekane kituko!

  Ushauri wangu.

  Kabla ya kuwasilisha sahihi 70 omba mwongozo kutoka kwa spika wa kuitishwa bunge la dharura baada ya siku kumi na nne kwa ajili ya maslahi ya umma pili ukiona hilo limewekewa zengwe omba mwongozo wa nini kifanyike kupiga kura ya kutokuwa na imani na spika naamini Sitta angekuwepo mambo yangeenda vizuri hata vifungu vingetenguliwa kwa maslahi ya Taifa.
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kumbe gongo inasaidia mkuu...
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii process iko sawa sawia labda tu ifike spika aamuue kwa ubabe tu kwamba haijadiliwi kwa kuwa Katiba inampa nguvu ya kukubali ama kukataa. Inasema akiona kama inafaa basi hoja itakujadiliwa na kura kupigwa. Lakini kwa jinsi nionavyo hoja itakubaliwa na spika kwa sababu Zitto atajikita kwenye ibara ya 52 (1) na spika hatakuwa na pakutokea. Wasiwasi wangu ni kwamba wabunge wa CCM hawatapiga kura ya kutokuwa na imani na PM hivyo ile 50%+1 haitapatikana. Pamoja na hayo ujumbe mpana na wenye mwangwi mkubwa utakuwa umefika kwenye mikono ya serikali.
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa hapo kwenye red akiona haifai Zitto aombe mwongozo wa kumng'oa mama kwa sababu yeye ni kikwazo kwa maamuzi yanayo favor maslahi ya umma.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,172
  Trophy Points: 280
  Mkuu Sokomoko, Zitto sio M/Kiti wa Kamati ya Kudumu ya Mahesabu ya Umma bali ni Mahesabu ya Mashirika ya Umma!.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Mkuu,
  Spika akikataa, cdm tunapiga kambi jimboni kwake. Wabunge wa ccm wakikataa, chopa aliyopewa Lema itafanya kazi kama wakati wa kampeni! Nakuhakikishia kiazi walichowekewa mdomoni na Zitto ni cha moto sana na hakimezeki wala hakifai kutema!
   
Loading...