Ushauri wangu wa bure kwa Zitto Kabwe na CHADEMA

nyakim

Member
Jan 27, 2015
68
26
KUHUSU KINACHOJILI MITANDAONI KUHUSU ZITTO.
Nimekuwa nikifuatilia japo si mda wote maoni ya wadau mbalimbali
mtandaoni kuhusu kinachojili hususani hatima ya zito kisiasa, na hatima ya
ubunge. kweli dunia imejaa watu wa aina zote, kuna watu wana huruma
ila hawana ufahamu, kuna watu wana ufahamu ila hawana ujasili wa
kuelezea wanachokifahamu, kuna watu wana imani flani ila wanaogopa
kuonyesha wanachokiamini, kuna wenye imani na itikadi na wanaweka wazi
bila kujali kinachofuata baada ya kueleza imani yao.
Kwa haraka sana huwezi kujua kilicho ndani ya moyo wa mwanadamu
mpaka afanye tendo flani, maana KIMTOKACHO MTU NDICHO KIUJAZACHO
MOYO WAKE, HIVYO KWA MATUNDA YAO MTAWATAMBUA. Binafsi
nampongeza sana kamanda Albert Msando kwa ujasili wake wa kusimama na
kutetea kile anachoamini. JAPO AMEONEKANA KUSIMAMIA MGUU MMOJA
WA UTAALAMU WA SHERIA AMEACHA AU AMESAHAU SKILLS OF CONFLICTS
RESOLUTIONS. MAANA KUNA MENGI KWA UKARIBU WAKE NA ZITTO
ANGESHAURI NA YAKAFANYIWA KAZI KWAN ZITTO ANA IMANI KUBWA
KWAKE, hii ingesaidia kuliko kutoa matamko wakati huu.
Binafsi simfahamu ZITTO kwa undani sana ila namfahamu kama
anavyofahamika kwa watanzania wengine, historia ya CHADEMA NI NDEFU
SANA KULIKO HISTORIA YA ZITTO. Nyuma ya mafanikio ya ZITTO ipo CDM
na nyuma ya mafanikio ya CDM yupo zitto kwa sehemu kubwa pia. Hivo sio
busara tosha kusimama kumbeza ZITTO na kushangilia kuondoka kwake.
Ni sahihi kumwacha zitto aondoke kama no way out ila si muhimu sana
kushangilia kuondoka kwake, kwa maana kumvumilia kwa miaka yote hiyo
kuanzia around 2008 mpk leo inatosha kuonyesha kwamba umuhimu wake
ulikuwa ni mkubwa ndani ya CDM, na kwa TZ kwa ujumla ila when he has
to die let him die no way, SIO BUSARA KUSEMA ZITTO AKITWENGWA NA
CHADEMA, CHADEMA ITATETELEKA. Hii ni miongoni mwa kauli za kipuuzi na
kipumbavu sana nilizowahi kukutana nazo. Leo MESSI asimame na kusema
bila yeye hakuna BARCELONA!!!! Hata mashabiki wake watamshangaa, Mi
naamini kuna watu CDM imewagharimu kuliko zitto na bado wameendelea
kujiona wa kawaida ndani ya CDM, na pengine hawajala tunda lolote toka
CDM zaidi ya kubaki na matumaini ya ukombozi unaokuja. kuna watu
wengi wametoa mali na hata majumba yao yanatumika kama ofisi za
CHAMA ila wako cool mpk leo na hawatangazi.
Kuna watu kama MEDARD MTUNGI, mzee huyu inasemekana amefirisika na
mpk sasa amepooza yote ni kwa ku devote maisha yake yote kwa CDM,
kuna watu wamefukuzwa shule hususani vyuo na wengine kufukuzwa kazi
kwa kusikika tu wanaipenda CDM, wengine wametishiwa kuwa sio raia wa
TZ kisa wanajihusisha na CDM, kuna waliopoteza wazazi, wapenzi na hata
watoto kwa sababu ya CDM. Kwa hayo tu utagundua no one IS THE BEST
IN CDM FAMILY. Bali kila mtu ana umuhimu wake anapokuwa mahali pake.
Kuna kauli nyingi ZITTO alizitoa wakati wa bunge la katiba especially
kuhusiana na UKAWA, ila juzi wakati anawasilisha report ya PAC kuhusu
ESCROW alisema alikuwa amewa miss ndugu zake wa UKAWA, every human
being became sympathetic with that statement, I being inclusive.
Juzi wakati waandishi wanamuhoji, kwa macho yangu NILIMUONA ZITTO
AKILENGWA NA MACHOZI KITU KILICHONIFANYA NITOKWE NA MACHOZI
GHAFLA. Sikulia kwa kuwa zitto kafukuzwa CDM bali nililia kwa uchungu
nikimwangalia SHETANI aliyejipanga kuyaharibu maisha na ramani ya zitto
ktk ulimwengu wa siasa, Binafsi nikasema wakati huu zitto anawahitaji
washauri wazuri kuliko wakati mwingine. Mana nilimhurumia ZITTO asiye
na mke kama nijuavyo, asiye na mama kama mshauri wa karibu,
nilimhurumia zaidi.
Wakati mmoja kipindi cha ule waraka wa siri nilimwandikia zitto ujumbe
nikasema"ZITTO KUNA VIJANA WENGI WENYE UWEZO ZAIDI YAKO HAPA TZ
ILA HAWAJAPEWA NAFASI KAMA ULIYONAYO WASIMAME HAPO ULIPO
WANGEFANYA MAKUBWA PENGINE ZAIDI YAKO". Sikumaanisha kwamba zitto
hafai kwa wakati ule ila nililenga kumwambia asijisahau ashike vema alicho
nacho asije mtu akamnyanganya mkononi mwake. leo hii tunamwona mtu
kama HUMPHREY POLEPOLE, binafsi sikuwahi kumwona kabla ya mchakato
wa katiba, leo Dunia imejua kuna kijana anaitwa POLEPOLE maana amepata
pa kusimama, tumemjua JUSSA na wengine, SIKUWAHI KUMJUA VIZURI
SALUM MWALIMU kama ana uwezo kiasi hiki kabla hajashika nafasi ya naibu
katibu mkuu, hivo bado naamini kuwa kuna vijana wengi bora wakipata
nafasi tutawaona.
Kwa mantiki hii zitto alipaswa kuendelea kuwa mnenyekevu na kuridhika na
kidogo alichokuwa anakipata kama wabunge wengine, huku mungu
akiendelea kumwinua taratibu angejikuta anayafikia mambo makubwa mno
bila kutokwa na jasho. Wakati ungefika zto angejikuta anapewa uwenyekiti
wa CHAMA pengine hata bila kuwa na mpinzani, na pengine angejikuta
anagombea u rais kwa kuombwa na si kulazimisha na kuumana kama
wafanyavyo MAGAMBA. Lakini haikuwa vile na hakuweza kuheshimu
SENIORITY aliweza kufanya kila alichotaka. SEMA KWELI HUWEZI KUJENGA
KWA KUBOMOA, zitto hakupaswa kuhubiri mambo ya ukanda, ukabila wala
udini mambo yanayohubiriwa na wapuuzi wa CCM.
Binafsi nadiriki kuamini kwamba hata kama matumizi ya ruzuku
yasingekuwa clear, zitto alikuwa na nafasi ya kukisahihisha CHAMA kwa
vikao vya ndani na si kutumia nafasi ya PAC kukidhalilisha chama
unachotaka uwe mkt wake. Na hili ni kwa sababu matumaini ya watz
kukomolewa kutoka mikononi mwa shetani mweusi (CCM) yako nyuma ya
CDM, si nyuma ya mtu mmoja kama zto au yeyote, na watz wamejenga
matumaini haya kutokana na kazi ya utetezi inayofanywa na chama na si
mtu mmoja na wala walio wengi hawajui kitu kuhusu katiba wala kanuni
za chama, hvo haikuwa busara kuwafanya watz wapoteze matumaini ktk
wakati ambao utungu wa kuzaa mabadiliko uko kwenye peak.
SASA baada ya yote hayo chama kama taasisi kina utaratibu wake wa
kushughulikia mambo yanayokihusu, UTARATIBU AMBAO ZITTO ANAUFAHAMU
VIZURI. Zto hakuutaka tena huo utaratibu ili utumike kuyashughulikia
mambo yake na chama aliamua kwenda MAHAKAMANI kukishitaki chama,
akivunja kanuni za CHAMA waziwazi. CHADEMA haijawahi kumpeleka zitto
mahakamani bali ilitaka vikao vya kawaida vya ndani vitumike
kulishughulikia jambo hili kama ambavyo zitto ameshiliki vikao hvo
kuwashughulikia wengine, THIS MEANS THERE WAS NOTHING MORE SPECIAL
TO ZITTO IN COMPARISON WITH OTHER CDM MEMBERS. Na sasa zitto
ameshindwa kesi aloifungua yeye mwenyewe. Na kilichoelezwa na LISSU ni
tafsiri ya kanuni za chama katika mazingira husika.
Sasa zimesikika kauli nyingi juu ya jambo hili, nyingine zikishangaza zaidi
hususani zinazotolewa na mashetani weusi (MA CCM) nimeona kauli za kina
mwigulu na wengine, SWALI NI JE NINI CDM WALIFANYA BAADA YA CCM
KUMTIMUA MANSOUR???? wanaweza kumchukua zitto kama wanamtaka.
Kwa upande wangu mimi kama mwanachama hai wa CHADEMA nikipewa
nafasi naweza kushauri kwa paragraph hii moja kama ifuatavyo.
Kwanza ni dhairi nawapongeza wanasheria wa chama, TUNDU A.M.LISSU,
JOHN MALLYA, PETER KIBATALA na wengine wamefanya kazi kubwa na ya
maana, Naipongeza kurugenzi ya ulinzi na idara ya USALAMA ya CHADEMA,
kweli wakati huu tunahitaji kuilinda CDM kuliko nyakati zote zilizowahi
kuwepo. NA TUTAKILINDA HIKI CHAMA HATA KWA DAMU YETU AU UHAI
WETU WENYEWE. BECAUSE ITS OUR ONLY REMAINING HOPE. SASA kwa
kuwa wakati huu jambo la zitto limeshika hatamu kwenye vyombo vya
habari na mijadala ya hapa na pale hata vijiweni, ni vema chama kikajikita
kwenye program zake za kawaida na ku keep attention ya kwenda kushika
dola oktoba mwaka huu. Kusema kweli watanzania hawako interested na
kumskia zito au yeyote wanahitaji kuongezewa matumaini juu ya ukombozi
ambao tyr wameuchungulia kwa mbali unaokuja mapema mwaka huu.
WENGI tunatambua mwisho wa hili bunge ni jul 2, 2015.ALMOST miezi
mitatu tu mbele, KAMA CHAMA NAAMINI KWA ZITTO KUWA MBUNGE KWA
MIEZI MITATU ILIYOBAKI HAKITOPUNGUKIWA NA CHOCHOTE, NA BADO
AKIFUKUZWA UBUNGE KESHO HAKUNA KITU CHA ZIADA KITAONGEZEKA KWA
CHAMA. Nasema hivi kwa kutambua kuwa yako mambo mengi ambayo ni YA
MUHIMU KWA TAIFA ANAYOPASWA KUYAFANYA NA KUYAMALIZIA ZITTO
AMBAYO NI LAZIMA AYAFANYE AKIWA MBUNGE NA KATU HAWEZI
KUYAFANYA AKIWA NJE YA UBUNGE. PIA NAAMINI CHAMA KITAKUWA NA
JUKUMU JINGINE LA KUZUNGUKA KUWAELEZEA WATANZANIA ILI WAELEWE
KINACHOJILI JUU YA ZITTO NA CHADEMA KITU AMBACHO NADRIKI KUKIITA
MNYUKANO USIOKUWA PRODUCTIVE.
Pia inafahamika kuwa tanzania inawahitaji watanzania wenye uelewa wa
kati na wa chini katika kuwa sehemu ya mabadiliko ktk nchi hii, hawa ni
watu ambao hawahitaji kuchanganywa wakati huu, na hawahitaji
kuhubiriwa harufu ya migogoro kwa wakati huu muhimu. Hawa ni watu
wasioijua katiba wala kanuni, bali wakimwona ZITTO, LEMA, LISSU, MBOWE
AU YEYOTE wameiona CHADEMA.
HIVO MIMI NAAMINI CHAMA KINAWEZA KUENDELEA NA MAMBO MENGINE
HATA BILA KUANDIKA BARUA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI AVULIWE UBUNGE,
KWA LOGIC YA NO GAIN NO PAIN OUT OF THAT. Naamini kwamba hili ni
fundisho tosha kwa wanachama na wabunge waliobaki na hata wale wajao,
kwamba lazima waheshimu kanuni na taratibu za chama. Hivyo mimi
naomba chama kisiendeleze hatua za kumvua ubunge kama ni somo zitto
kalipata.
USHAURI WANGU KWA ZITTO.
Zitto ni mtu muhimu sana katika kizazi hiki na MUNGU kamjalia uwezo wa
kipekee katika nyanja za kisiasa na hata kukubalika kwa watu. ZITTO
anahitaji kujitafakari upya katika vigezo vya kizalendo. ZITTO anapaswa
kutambua kuwa watz hawana hamu na malumbano kwa wakati huu, si
vizuri kuendelea kujiona bora kuliko wengine, bali atambue watz ni bora
kuliko yeye na ndio maana wanamtumikisha,(maana wamemchagua awe
mtumishi wao), na kweli kwa kiasi kikubwa zitto amekuwa si mbunge wa
kigoma kaskazini tu BALI MBUNGE WA WATANZANI, mfano wa kuigwa.
Juzi nilimskia akiwaambia waandishi wa habari kwa masikio yangu kwamba
"MIMI NI MWANASIASA WA TOFAUTI SIDILI NA WATU NADILI NA ISSUES,
AKAONGEZA KWAMBA MIMI HUWEZI KUNIFANANISHA NA WABUNGE
WENGINE". kauli hii sikuipenda inawafanya hata wabunge wengine
kumwona vibaya.
Hivo ZITTO anapaswa kutulia na kufanya SIASA akitaka kueleweka kwa
watanzania asimame kidete na apambane na CCM ili uzalendo wake
uthibitike, sidhani kama itakuwa busara ZITTO kuendelea kuisema vibaya
CDM au viongozi wake, UKIZINGATIA CHADEMA SI TATIZO KWA
WATANZANIA BALI NI NEEMA
 
...zito angekuwa chama dume wangesha muua, cheki orodha ya viongozi wao waliouwawa vifo vya ajabu, sumu, kupotelea marekani na wengine wengi...
 
CDM upuuzi na ni laaana kwa Tanzania ukabila na udini uliokidhiri naipa ccm miaka 20 mingine ya kuitawala tz upinzani bado saana tz
 
Back
Top Bottom