zito nakushauri urudi ccm na ukagombee ubunge kwa kupitia huko au vyama nipya vilivyoanzishwa na ccm kwa ajili ya kuikabili chadema ambavyo ni chauma ,adc na vingine wanavyovijua wao. nasema hayo sababu nyingi lakini nitasema chache.
1.wakati viongozi wa juu wote wa chadema wanapambana kwa kutumia m4c zito haujaonekana hata kwenye mkutano mmoja ikiwa kama ni kutotaka kutamka maneno ya kuwaudhi waliokutuma kuichafua chadema.
2.zito unapopeleka hoja yoyote bungeni inakuwa ya kujijenga binafsi na si kwa maslahi ya wanyonge wengi na wabunge wa upinzani hususani chama chako na hii ni pamoja na kutokutoka nje ya ukumbi wa bunge pale chadema wanapofanya hivyo kwa maslahi ya chama chao.
3.umejisifu sana kuwa wewe ni muadilifu na unao uwezo wa kuwa rais wa nchi 2015 kwa hili umekosea maana njia uliyoitumia ni mbovu sana maana kuna vikao vya chama ambavyo ungevitumia kueleza hoja yako lakini kwa kutumia waandishi wa habari na bunge na vijana wako wa kigoma halitakusaidia kufika huko maana nyuma yake inaoonekana kuna baraka za bwana mkubwa ili muivuruge chadema.
4.taarifa zisizo rasmi zinaonyesha urafiki wako wa karibu na jakaya na ridhiwani ni mashaka makubwa sana maana hakuna sehemu yoyote ambayo umemlaumu rais wa nchi kwa udhaifu wake bali amekutumia kumdhalilisha waziri mkuu kwa maslahi ya ikulu na si kwa upinzani unaposema serikali haiko makini bado unaficha kumtaja jakaya moja kwa moja sababu ya agenda zenu za siri ambazo wana ccm na wanachadema wengi wameliona.
Umeingizwa kwenye orodha ya wala rushwa wabunge kwa makusudi tu kuichafua chadema na si vinginevyo na hili unalijua vizuri.sidhani kama kupitia chadema utafanikiwa ndoto zako maana chadema wako makini ndio maana hakuna kiongozi wa juu wa chama aliyejibu hoja zako za kuutaka uraisi kiurahisi ushauri wangu kwako utangaze adharani kujiunga kwako na kundi la shibuda nakutakia safari njema.m4c daima.
Huyu angeweza kupuuzwa, lakini kwa mapesa aliyokusanya toka ndani na nje ya nchi ili kutimiza ndoto zake, huyu si hatari kwa CDM tu, ni hatari kwa ustawi wa taifa hili. Hawa wanaompa mapesa toka nje wana malengo gani? Atawarushiaje mapesa yao? Think twice.zito ana kiburi kwa kufikiri wale bongoflavour wake watampeleka ikulu unahitaji baraka za chama sio za kikwete
Zito hakuwahi kuwa mwanachama wa ccm, hivyo kusema arudi ccm si sahihi ni bora ungesema ahamie ccm,
Sisi sote ni watanzania hivyo kutofautiana ki-itikadi hakutenganishi utanzania wetu, si dhambi kuwa na urafiki na mtu eti kisa hamko chama kimoja.
Zito bado ni Mwanasiasa safi na makini pale Chadema.
simjibii mwanasiasa Zitto Kabwe, bali najaribu kuelezea jinsi ninavyoona!
Tatatizo liko hivi (nafikiri) Zitto anataka kuendelea mbele katika siasa lakini tatizo anatoka familia ya kimaskini kama watz wengi tulivvyo, na ukweli ni kwamba kama huna pesa hakuna mafanikio katika siasa, huo ndio ukweli wenyewe! Sasa swali linakuja atapata wapi pesa? Kuna mawili aidha mtu au kikundi cha watu kimpe ili afanikishe azma yake ya kisiasa au yeye
mwenyewe atafute, lakini atafute wapi kwao sio matajiri?
Kwa hiyo njia pekee na raisi iliyobaki kuzunguka huko huko serikalini kwa watu wa CCm kufanya nao dili na mwishowe kupata pesa ambayo sasa anaweza kuitumia kukamilisha mipango yake ya kisiasa, lakini hiyo haiji bure ina bei pia na bei yake ndio kama hiyo anayoilipa sasa , na huu ni mwanzo mengi yatakuja kwa maana piga ua garagaza anahitaji PESA kama anataka kutimiza azma ya kusonga mbele kisiasa!
Mwanzoni nilidhani una nia kweli ya kumshauri zito ila baada ya post hii naanza kutilia shaka kama nia yako ilikuwa ni kumshauri zito au ulitaka kupima upepo kama imani ya watu imepotea kwa zito.Zitto hasemwi ovyo ovyo isipokuwa wanajua Zitto ndiye kiungo kikubwa cha pande mbili za mtazamo kitikadi ndani ya Chadema. Navyoamini mimi, ktk swala la Uchaguzi mkuu na utawala -chama cha CCM huchukulia hili kama wako vitani na ndio maana wanasema - Ushindi wa Uchaguzi mkuu utapatikana kwa njia yoyote ile..Na siku zote CCM hutafuta sehemu inayoweza kukiyumbisha chama mbadala cha Upinzani kwa kutafuta their weakest point of entry..Hivyo wakaona mahala ambapo wanaweza penyeza ngome ya Chadema ni Zitto. Ndio maana Zitto alipewa wenyekiti wa kamati ya JK kuhusu madini wakati uleee, Mnyika akaja juu sana kupinga uteuzi ule kinyume cha matakwa ya chama, lakini kwa furaha kubwa Zitto akaingia mzima mzima. Toka pale CCM wakamkamata na kuhakikisha anaambukizwa gonjwa la upinzani wowote ndani ya Chadema dhidi yake ni kwa sababu yeye Muislaam..
I know all these things toka vijiwe vya mujini, tena walimpa Zitto hadi mafaili ya kina Mbowe na viongozi wengine waliopokea rushwa ama kuwa upande wa kina RA na EL kumpitisha JK uchaguzi wa 2005. Vitu vingine vilitungwa kuhakikisha Zitto anaweka mashaka ktk dhamira ya viongozi wake. Na wala sii kosa lake tu, uongozi wa Chadema pia kwa kuelewa hivyo walianza kumtenga, kutomwamini maana mtu yeyote anayefanya kazi na serikali wakati hakuna makubaliano ya Bipartisan ina maana yuko upande wa pili..
Sijui kama unakumbuka Senator Joe Lieberman wa Marekani, huyu alikuwa Presidential material alipokuwa Democratic lakini kutokana na msimamo wake wa ndumila kuwili, alianza kutengwa akajikuta pekee na kila siku hakosekani CCN kwa kashfa na misimamo yake, mwisho ilifikia kuhama chama na leo hii kabakia senator tu ambaye hana mbele wala nyuma..Hivi ndivyo siasa inavyoweza kukujenga ama kukubomoa.
Mambo yote hyanayohusiana na Zitto yametengenezwa na CCM ili wanaCHadema mzidi kukosa matumaini naye na kwa kufanya hivyo mtagawanyika. Zitto ana watu wanaomwamini sana na ambao wanajua fika kwamba ndani ya Chadema kuna mtandao vile vile.. Na tumeyaona mengi hapa JF jinsi Zitto anavyosakamwa na WanaChadema wenyewe. Kuna makundi ndani ya chama na pengine naweza kusema kwamba tunaweka sana matumaini kwa Dr.Slaa wakati ikifika 2015, sidhani kama kiafya na Umri, atakuwa na nguvu kama za jana na leo - simwombei mabaya lakini nasema what if?.....
Let's say kwa hali ambayo haikutegemewa Dr.Slaa hatagombea Urais - Je, tuna chaguo gani jingine -Ni Tundu Lissu? Mbowe? Mnyika? au Prof. Safari?....Na kwa nini jina la Zitto lisiwepo?
Zitto anapakazwa sana kwa malengo na hasa wabunge ambao wanapokea posho ilihali Zitto ndiye sababu ya kukatwa ongezeko..Zitto na Makamba wana maadui wengi tu muhimu ni wao kufahamu makosa yao kama vijana mnaowategemea kesho.
Hapa ndipo panaponishangaza mimi....yaani watu wa ccm wote wanamsapoti Zitto. kazi kweli kweliThe journey to the presidency is not an easy one, there are rivers to xross and mountains to climb; some rivers with crocodiles and hippos...but for ambitious ones, it is worth a journey to pursue....Go ZZK! Go
Huu ni upepo tu na utapita!
ananunuliwa kama akina mrema na wenzake
Bora umemwongelea kwani intia kinyaa.Hivi alipofikia alitumia sh. Ngapi? Azma yake ipi hiyo?Umasikini wake ndio unamponza ajipime na walionazo?sasa ya nini kununua magari ya kifahari.simjibii mwanasiasa Zitto Kabwe, bali najaribu kuelezea jinsi ninavyoona!
Tatatizo liko hivi (nafikiri) Zitto anataka kuendelea mbele katika siasa lakini tatizo anatoka familia ya kimaskini kama watz wengi tulivvyo, na ukweli ni kwamba kama huna pesa hakuna mafanikio katika siasa, huo ndio ukweli wenyewe! Sasa swali linakuja atapata wapi pesa? Kuna mawili aidha mtu au kikundi cha watu kimpe ili afanikishe azma yake ya kisiasa au yeye mwenyewe atafute, lakini atafute wapi kwao sio matajiri?
Kwa hiyo njia pekee na raisi iliyobaki kuzunguka huko huko serikalini kwa watu wa CCm kufanya nao dili na mwishowe kupata pesa ambayo sasa anaweza kuitumia kukamilisha mipango yake ya kisiasa, lakini hiyo haiji bure ina bei pia na bei yake ndio kama hiyo anayoilipa sasa , na huu ni mwanzo mengi yatakuja kwa maana piga ua garagaza anahitaji PESA kama anataka kutimiza azma ya kusonga mbele kisiasa!
Kijana huyu mnafiki sijapata kuona......kweheri zitto ulitaka kuwafanya watz mambumbu eeee sasa misifa yako utaona mwisho wako pia