OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Waziri wa Habari, Paulo Makonda ameonesha nia nzuri ya kutaka Tanzania ifahamike kimataifa. Hata hivyo utaratibu aliouzungumza ili Tanzania iandikwe aljazeera, CNN na maeneo mengine ina walakini, na hapa nitoe mawazo yangu kwenye kutimiza hilo.
Suala la sisi kuandikwa kimataifa halifanyiki sana kwa kuwa tunawatu wachache waliokwenye taasisi za kimataifa. Je tunafanyaje kwanza kuhakikisha watu hawa wanaenda kimataifa na kuwa connected ili nasi tupate kuwatumia katika kuleta picha nzuri ya nchi yetu.
Nitoe mfano wa Kenya ambayo ina watu wengi kimataifa na mnaona jinsi Kenya inafanya vizuri hadi watu wengi wanajua vitu vingi vipo kwao. Larry Madowo, sikosoi kazi yake, anafanya vizuri lakini mliona akiripoti matatizo ya Kenya? Suala ni kwamba ukiwa na watu kama Larry ni rahisi kupata story nzuri za nchi yako kwenye maeneo hayo ya kimataifa. Larry mbali na kufanya kazi sana Kenya 2019–2020 alipata Knight-Bagehot Fellows huko Columbia University. Hapo alipata kuwa correspondent wa media outlets kubwa.
Serikali za Pakistan na South Korea kwa ushahidi nilio nao wanashirikiana na Marekani ili watu wao waende kupata exposure huko na zinawafanya waende mbali. Serikali ya Tanzania haitoi hela ili watu waende mbali. Mfano Tanzania kulikuwa na Fulbright program ambayo inafadhiliwa na Marekani. Hii program huchukua mtu mmoja hadi wawili kila mwaka kwenda kujifunza vitu tofauti tofauti Marekani. Lakini nchi nyingine utakuta zinatoa watu hadi 10 kwa kila mwaka kwa kuwa nchi zao zinatoa hela kwa hizo program ili watu wao wawe wengi.
Maana yangu ni kuwa, badala ya kulazimisha watu wabaki Tanzania, tukomae na suala la watu kupata hizi exchange programs ili kuongeza representation kimataifa. Mfano, Badala ya Samia scholarship kupeleka wanafunzi Arusha, tuwapeleke vyuo vya Marekani au Ulaya ambako watakuwa more exposed.
Kuna MicroMasters program inatolewa na wataalamu wa kubwa wa data huko MIT. Kila course inalipiwa $250, na inabidi usome course 4 ilikupata MicroMasters. Ukiangalia pale Brazil inatoa hela kwa watu wake ili wasome bure badala ya kulipa hela hiyo. Lakini kwa Africa, lazima upambane kupata hela ya kusoma, hebu fikiria ulipe $1250 ili kupata micromasters, ambayo ni milioni zaidi ya mbili kwa fedha za Tz. Lakini ile masters inawapeleka watu sehemu kubwa sana.
Mfano wa fellowship kwa ajili ya kusoma
So, nitoe wito kwa Makonda kwamba kama anafikiria kuleta picha nzuri ya Tanzania nje ya Tanzania. Asiwaze kwamba unaweza kupeleka Press release kwa editors ili waandike habari yako. Ila tukiwa na watu wengi kimataifa watasaidia katika kufanya hizo press releases ziwe stories strategically.
Nawasilisha.