Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,978
- 5,025
Ukitaka sherehe ujipange sawa sawa.
Hakikisha una pesa ya kutosha kuchukua gharama za sherehe pale Mambo yanapoenda tofauti.
Vinginevyo utajikuta unawachukia watu kisa hawajakuchangia wakati sio lazima. Kuna watu wananuniana humu mijini kisa mwingine hakuchanga mchango wa sherehe.!!
Ndoa/send-off sio dharula kwamba isipofanyika kuna mtu atakufa. Tujipange ili tusiingie kwenye ndoa na mikopo kisa siku moja. Sio kila uliyesoma naye/unayefanya naye kazi/ uliyenaye group moja umhesabie Kama ni pesa yako ya sherehe.
Watu Wana Mambo mbali mbali humu duniani. Nakumbuka wakati naoa niliamua kufungia ndoa nyumbani waliko wazazi. Hii ilipunguza gharama za kuwalaza wazazi na ndugu hotelini ugenini.!! Pia nilihakikisha mfuko uko sawa ndio nikaanzisha mchakato. Kamati ilifanya kazi yake lakini sikuwa na shaka na hofu ya kuanza kukopa ili sherehe ifanyike. Na huko kijijini Mambo ni rahisi tu. Bajeti ndogo sana inakutoa na tukio linafanikiwa.
Tujipange jamani ukiona bajeti ngumu jua watu waliko wanalia na ukata wa pesa.