Ushauri Wangu kwa Wakongo (DRC)

tutaongea mengi,ukweli ni kwamba vita ya Congo,niyakufitinishwa na majirani,kibaya zaidi wanaofaulisha hizo fitina ni wacongo wenyewe,namaanisha ndani ya Congo kuna wa Congo wasaliti,wa Congo wanao wauza wa Congo wenzao kwa tamaa zao binafsi na maslahi yao binafsi,lakini swali lakujiuliza ni hili je kwa nn usaliti huu umekuwa sugu ndani ya ardhi ya Congo,jibu ni hili uzalendo wa wacongo ulishazikwa kitambo tangu enzi za mobutu seseseko,hivyo Congo ina generation ambayo neno uzalendo halimo ,yaani kisayansi ile Gene ya uzalendo haimo.ni kweli Congo ina viongozi lakini ni viongozi wa sio na uzalendo na ardhi yao,ni kweli Congo ina Wana nchi wazee kwa vijana lakini ni wananchi wasio na uzalendo na ardhi yao,ni kweli congo ina jeshi lakini ni jeshi lisilo na uzalendo na ardhi yao,ni kweli congo ina polisi lakini ni polisi wasio na uzalendo na nchi yao.hakuna nchi ambayo huwa haifitiniwi lakini tunaona linapokuja kwenye suala la nchi wananchi,viongozi na jeshi huweka tofauti zao pembeni na kuwa na sauti moja,kiongozi akisema adui na apigweee,wananchi na jeshi lote huitikia apigweee tena kwa kumaanisha kutoka moyoni wakiwa na Nia moja na ari moja ,na sio apigweeee ya mdomoni hapana.hata wapalestine tunawaona wanavyopambana kwa pamoja hata Kama bado hawaja fanikiwa lakini dunia nzima inaona wapalestine wanavyo waumiza vichwa waisrael,na hata Kama ukisimama useme wapalestine hawana uzalendo watu watakushangaa Sana,hii ni tofauti kwa ndg zangu wacongo.tatizo la congo limekuwa la muda mrefu Sana,lakini ni wao wacongo wenyewe wamekubali na kuridhika na yote. Ukweli ni kwamba wakongo kwa pamoja wakisema sasa basi inatosha,wanauwezo wa kumpiga adui yao nakumtoa nje ya mipaka,wanauwezo wa kumpiga hata wakaingia ndani ya mipaka ya adui na kumpiga,inawezekana kwa wacongo lakini ikiwa hawata geuka nyuma na kuviwazia vilivyo nyuma yao.kurudisha heshima ya kongo inahitaji sadaka ,sadaka ya kujitoa ,wacongo wa sasa wanahitaji kujitoa sadaka ili kutengeneza congo mpya yenye heshma kwa kizazi na kizazi kijacho.
 
Kinacho waumiza wakongo ni mali yao iliyo ardhini dunia hii yote teknoligia haiwez kwenda bila kongo!!!

Nawasilisha
 
Maoni mazuri
 

Extra wapo Congo nyingine
 
Mkuu Sio Kongo tu niseme Afrika kwa ujumla tulishakubali kuwa meza ya kuchezewa chess na first world hakuna namna ya kushauri kitu ilishakuwa more than too late yani mtu anakuwa mkubwa AU wakati nchini kwake ni afadhali ya shida.Inachekesha
 
Exta nusica hawatoki DRC bali congo brazaville
 
Tusikimbilie kulaumu mataifa ya nje,hata mataifa yaliyoizunguka baadhi yameifanya Congo kuwa hapa ilipo,wamejawa uroho tamaa iliyopitiliza,hata sisi ni wabaya sana Tena Sana,Kuna baadhi ya nchi zinaendesha hata nchi zao kwa uwepo wa Congo,tunabaki kulaumu mataifa ya nje yanafaidika yanagombanisha na maneno chungu nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…