Gwappo Mwakatobe
R I P
- Nov 22, 2019
- 1,796
- 2,345
Bongo unafanya unayowashauri wa kongo
Nimekuelewa Sana ndugu. Huwa nakusikia ktk kipindi cha maoni cha radio DW.
🤣🤣🤣🤣Kila siku Wakongo wanatumia midomo yao kuimba nyimbo za "nakupenda Cherie;
na lingi mwasi kitoko na ngai."
Nadhani tungetumia vizuri fursa ya ujirani na uwepo wa maliasili zao kwa maendeleo ya nchi yetu. Hao Wakongo waendelee tu kutuburudisha na Ma soukouss yao.
Haiwezekani Mabeberu wa Kichina, Kimarekani, Kibeligiji, Kifaransa, Rwanda na Uganda wanafaidi, halafu eti sisi tunashangaa tu.
Ile nchi, fujo zote zilizopo hapo, ni makundi mbalimbali ya wakongo wenyewe ambapo hupenyezewa lupia kutoka nchi za ng'ambo ili tu nchi hizo ziendelee Kuiba utajiri wa wacongomani!
Ili kudhibiti, kunahitajika kuwepo jeshi la kizalendo la Wa Congo wenyewe, na linalojua kunusa ili kuwanyang'anya siraha hao waasi ambao wamejikita hata ndani ya jeshi
Nitakifuatilia.Shukrani sana! Jumamosi kesho kutwa, saa 7 mchana baada ya habari za kimataifa, utanisikia na wenzangu wa Kampala na Kinshasa tukichambua uenyekiti wa Tshisekedi kupitia DW.
DW wanajiunga na FM Radios nyingi hapa nchini. Afrika tuna safari ndefu na ngumu endapo sisi Waafrika wote na AU hatutajipanga upya.
[emoji120][emoji120][emoji120]Nitakifuatilia.
Inaonekana wewe kwenye mambo ya siasa hasa za DRC, ni mweupe kabisa!!mzozo wa congo asilimia kubwa si wao kwa wao ndani ya nchi, mfano, congo mashariki ndiko kwenye shida hasa kivu ya kasikazini, Goma, beni ambako ni mpakani mwa uganda, Rwanda, na maeneo kidogo ya huku kivu ya kusini, maeneo ya FIZI, ITOMBWE, na BARAKA, lakini ukiwa ktk jiji la UVIRA hayo mapigano unayasikia kama unavyoyasikia ukiwa TZ, shida kubwa ni RWANDA, kupitia wanyamulenge, hasa huku kivu kusini, pamoja na kasikazini.Rais Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa DRC amepata uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), wakati nchini kwake bado kunawaka moto na ebola imerudi. Je, atayamudu matatizo ya Afrika nzima ikiwa kwake bado kugumu!? Wakongo msaidieni Rais Tshisekedi...
Inaonekana wewe kwenye mambo ya siasa hasa za DRC, ni mweupe kabisa!!mzozo wa congo asilimia kubwa si wao kwa wao ndani ya nchi, mfano, congo mashariki ndiko kwenye shida hasa kivu ya kasikazini...
Mkuu kwanza ungeenda sikiza LOSAMBO ya EXTRA MUSICA kisha ungerekebisha kauri yako
si sahihi kusema wanaimba mapenzi hawaiimbii nchi yao
zipo nyimbo nyingi sana tangu miaka ya kina LUAMBO MIKIADI hadi enzi za kina KABASELE YAMPANYA
Nimekutajia LOSAMBO sababu ni maarufu
Ila wewe uliipenda sebene na midundo ya musica yake ukasahau ujumbe mzito uliopo humo ndani ya mashahiri ya hiyo nyimbo
ambapo humo utazisikia sauti zenye huzuni Mwingi na zenye UCHUNGU mkubwa na nchi yao za kina IBAMBI OKOMBI ROGATIEN na kundi nzima la EXTRA MUSICA wakiimbia nchi yao jinsi maswaibu inayoyapata kiasi wanamuomba MUNGU mpk wanamtaja kwa jina la ALLAH
awaunganishe wacongo
awape NGUVU wapambane kuikomboa nchi yao
Hiyo ni moja kati ya nyimbo nyingi tu mkuu hvyo swala la kuimba washaimba sanaaa
Hvyo nyimbo pekee hazitoshi
CONGO inahitajika apatikane KIONGOZI mzarendo asiyesimikwa na mabeberu mwenye uchungu na nchi yake wanacongo wenzake
Akawaunganisha wakawa wamoja wakaijenga nchi yao
Asikwambie mtu
WACONGO wanapata TABU
Wanateseka mno ndani ya nchi yao
Tangu enzi za KING LEOPORD mpk kesho wacongo wanaishi kwa mateso mno katika ARDHI yao ambayo imebarikiwa kila aina ya neema si madini mito misitu na ARDHI yenye rutuba na eneo pana
TATA NZAMBE YOKA LOSAMBO YA BANA YA LE CONGO
PESA NGUYA PAPA
PO TULUKA LA VIE
Kuna Watu Vichwani mwenu mmejaza Usaha tu. Hivi Nchi kuwa na Machafuko ndiyo Kigezo cha Kutengwa?Rais Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa DRC amepata uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), wakati nchini kwake bado kunawaka moto na ebola imerudi. Je, atayamudu matatizo ya Afrika nzima ikiwa kwake bado kugumu!? Wakongo msaidieni Rais Tshisekedi...