saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,131
- 6,130
Hao Sauli lao speed, kuna hii kampuni inaitwa Maning Nice inafanya biashara sehemu nyingi nchini. Nataka nizungumzie haya mabasi yake yanayotoka Tunduru kuja Dar Es Salaam. Haya mabasi yananyanyasa sana abiria. Kwanza kifungua kinywa ni mpaka saa 8 ukifika Nangurukuru. Watu wengine wana matatizo ya vidonda vya tumbo, hivi kuanzia Mangaka, Masasi mpaka Mtama hakuna hoteli? kwanini watu washinde njaa mpaka saa 8? Safari ni adhabu? Tatizo la pili hawajali na wanadharau sheria za nchi na maelekezo ya viongozi wa serikali. Magari yanaishia Temeke mwisho badala ya stendi kuu ya mabasi ya mikoani km sheria inavyoelekeza na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ametoa agizo kwamba mabasi yote yashushe na kupakia abiria stendi kuu ya mabasi tu na si sehemu nyingine wao wamepuuza. Hawa wamenunua serikali kupitia jeshi la polisi. Wamenitesa sana napakia mizigo kwenye daladala baadaye usafiri wa mizigo kuingia stendi maana nilikuwa niunganishe safari kwenda mkoa mwingine. Serikali ifuatilie kampuni hii, lazima wanatoa rushwa kuwanyanyasa wananchi waliolipia usafiri husikaWakuu habari,
Ningependa kuishauri SUMATRA wawaite na kuwashauri wamiliki/madereva wa mabasi ya SAULI kuwa kusifiwa barabarani kwa ubingwa wao wa kukimbia speed kubwa na kuovertake bila mpangilio siku moja kutagharimu maisha ya abiria wasio na hatia.
Ushauri wangu ni huo kwenu SUMATRA msije sema hamkuambiwa.