Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,675
Tukitaka jiji la Mwanza liwe bora kimwonekano lakini pia liongeze thamani ya ardhi na uwekezaji ambao utachangia mapato basi hatuna budi kuanza na ile mitaa ya daraja la juu na daraja la kati ambapo ni rahisi mno kufanya marekebisho kuliko ile ndoto ya mchana ya kuibadili mabatini kuwa real estate.
Mwanza ni tofauti na miji mingine mikubwa ambapo watu wenye kipato kikubwa uishi katika mazingira yanayowafaa peke yao pasipo changanyikeni.
Ile tunayojivunia nayo kama Capripoint waweza fikiri pengine ni mtaa kweli wa madon ila ukipata nafasi ya kuuona upande wake wa pili wenye umaskini wa kutupwa kule tunapaita Capripoint idara ya maji huwezi kuamini kama ndiyo huo huo mtaa mmoja.Kuna slums kule za washashi na wajaluo Ilemela ikasome.
Bwiru nako ukishika ile njia lilipo kanisa la AIC ukanyoosha ukielekea mwaloni, ukauvuka mwalo alafu ukaanza kupandisha kuelekea juu kuna slums za ajabu sana kule za ndugu zangu wasukuma hata baiskeli kuipitisha ni kazi.
Kwa ujumla Ilemela iko vizuri kuanzia kona ya kwenda Igombe kuzunguka mpaka Tunza na kurudi RFA kote huko pako njema kabisa.
Tatizo la Ilemela liko ile mitaa ya mahakama na kule juu milimani lakini nako hakuna slums choka mbaya sana kama zile za Capripoint na Bwiru.
Kipi kifanyike kukamilisha uzuri wa Capripoint na Bwiru.
Serikali ikawalipe fidia wamiliki wa zile slums kwa awamu kulingana na uwezo wao wa mfuko kisha mabanda yale yavunjwe na kisha serikali iuze viwanja kwa faida kubwa.
Serikali ikimaliza hapo ihamie eneo la Bugando mtaa wa miembeni kuna slums za kufa mtu lakini wale jamaa wakilipwa fidia wakaliacha wazi lile eneo serikali inaweza kuliuza kwa faida kubwa sana tu.