Ushauri wangu kwa serikali ya Jiji la Mwanza

Ushauri wangu kwa serikali ya Jiji la Mwanza

Unawaongelea jiji gani hawa hawa wa mwanza? Ambao wameshindwa walau kulipa fidia maeneo yaliyowazi wakapanga mji na wakauza viwanja kwa faida kubwa tu, waje wapate pesa ya kuwalipa hao waliokwisha jenga? Labda muwekezaji mwenyewe ahamue kuwaondoa mmoja mmoja yeye mwenyewe lakini sio jiji, nikuulize mara ya mwisho umesikia jiji wanauza viwanja Vilivyopangwa na kupimwa ni lini, Watu wamestaarabika kuna wanaohitaji sehemu zilizopangwa vyema lakini hazipo, Badala ya kuhangaika na hao ni vyema wangeenda maeneo kama Sawa, Lwanima, Isebanda na huko usagara na kisesa wakalipa fidia maeneo yaliyowazi wapange wapime ili mji usiendelee kujengwa kiholela
Hiki ni kipimo tosha bila kupepesa kope kuwa serikali tuliyonayo madarakani haiwajibiki kwa wananchi wake inavyotakiwa na ni aibu kubwa kama taifa kuendelea kuongozwa namna hii pasipo kuwa na future ya baadaye.
 
Inasikitisha sana hii miji yetu Nyerere wa miaka ya 70 aliweza kupanga vijiji vya ujamaa na vikawa na taswila nzuli tu na vikaeleweka huku ni Sehemu za mashamba huku ni Makazi na kule ni kufuga, Sie serikari inamuachia mwananchi ajipange mwenyewe na baadae ndio wanakuja kufanya upimaji shilikishi ambao unasaidia zaidi kupata hati na sio kupanga miji.Suala la mipangomiji Serikari ilichukue kwa uzito tusiporekebisha leo huko mbeleni hatutaweza maana thamani ya ardhi itakua tayali imeongezeka sana
 
Hivi ulisbajiuliza hizi nyumba watanzania wanazojenga miaka hii kama zingejengwa maeneo yaliyopangwa miji yetu ingependezaje? Watanzania wanajitafuta na wanajipenda mtu anaweka nyumba kweli Msauzi unasimama juu, chakusikitisha nyumba inazoofishwa na eneo ,Shagala bagala huyu kageukia kulia mwingine kushoto,alikoweka choo mwenzio we ndo sebule ipo huko, barabara mita 3 au 2 nguzo humo humo, mabomba ya maji na wakati mwingine zinageuzwa mifereji na mamlaka hazishtuki wala nini
 
Umasikini siyo sifa ya kujivunia achana na huo ujinga dunia nzima inatambua kuna madaraja na katu hatulingani, kwahiyo kama ni masikini ndiyo uruhusu Tanzania nzima iwe na mwonekano wa dhiki ya mabanda kila mahali?

Isitoshe hapa nawaongelea hao hao wanyonge hili wapate fidia wakaishi maisha yanayofaa huku wakiachia maeneo promising kwa ajili ya watu wenye uwezo mkubwa kuwekeza na pesa inayopatikana hapo ndiyo itakayorudi kwa mnyonge huyo huyo kumboreshea miundombinu.
Usiite mawazo ya wenzio ujinga maana waweza jikuta we ndio mjinga, kuwa makini mkuu!!
Nikirudi kwenye hoja, hilo unaloshauri kwa serikali yako ni gumu sanaaa, hata mdau mmoja hapo amesema iwapo mamlaka ya jiji yenyewe tu haina viwanja vizuri vilivyopimwa na kuwekewa mipango elekezi vipi wataweza kulipa fidia za watu????
Unalazimishaje sehemu ambazo watu wamezi develop kwa miaka kibao kuganga njaa zao kipindi ambacho hata hao matajiri hawana A wala B, wazo ni zuri ila wangeanza walau kwenda maeneo ambayo bado wana uwezo wa kuyaendeleza na wakayauza kwa watu wenye uchumi unaousema!!!
Kingine pia ukifuatilia miaka kadhaa nyuma kulikua na mipango kama hiyo ya kuuza maeneo yaliyopimwa na kutayarishwa na mipango miji lakini ajabu watumishi wa jiji mamlaka za viwanja na watumishi wengine wenye nafasi ndio waliokua wanaambulia nafasi hizo ambapo kiuhalisia wafanyakazi hao zinapokoma au kushuka kwa kipato katika ajira zao maeneo waliyayachukua hugeuka kuwa ya kawaida tu kinyume na matarajio, iambie serikali yako vizuri wanapoamua kuuza viwanja hasa hivyo vyenye hadhi ya watu fulani basi iwe ni watu wenye hadhi hiyo kweli ndio wanunue ili kukamilisha taswira ambayo wewe na serikali mnaiwaza!!!
Kama unapataka capripoint kaongee na mtu umuhamishe achana kuisakizia serikali ambayo kiwanja cha bure wameshindwa acha hiyo fidia
 
Hata wapanga mipango na watoa maamuzi wa jiji la Mwanza nawao ni bule tu hususani hao madiwani, Watu na exposure zao na ziara zote za kujifunza kwenye miji mingine wanaenda kujenga vitu vya ajabu pale nera, mmeshindwa kuiga hata pale coco Beach walivyotengeneza Vibanda vya wale wauza chakula na mihogo, hivyo vibanda na hapo ni mbele ya mji hamjisikii aibu kwanini msitumie wataalam wakatengeneza mandhali nzuli wakachanganya na hivyo vibanda
 
Back
Top Bottom