Shabiby yatajwa kuwa kampuni bora ya usafiri wa Mabasi nchini

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wadau poleni kwa majukumu ya kila siku. Kwa mujibu wa utafiti wa kina, Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Line ndiyo watoa huduma bora nchini.

Shabiby Line yenye huduma ya usafiri kwa madaraja ya kawada hadi VVIP wamepewa Tuzo ya Watoa Huduma Bora Tanzania (kwa usafirishaji kwa njia ya mabasi) ikiwa ni mara ya pili kwa miaka miwili mfululizo, 2021-2022.

Sanjari na hilo, Shabiby imetajwa kuwa ni kampuni ya mabasi isiyokuwa na migogoro ya ukiukwaji wa maelekezo na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) tofauti na baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa yakifanya kinyume na makubaliano ya maelekezo.

Tuzo hiyo waliyopewa Shabiby Line imetolewa na Consumer Choice Award Africa 2022. Pia ni kampuni isiyokuwa na migogoro na Taboa. Mmiliki wake ni msikivu na anayejali na kusimamia biashara yake vizuri. Hajawahi kuitwa kwenye vikao vya kuonywa vya mamlaka husika kama Taboa na Latra.

Baadhi ya watu waliyozungumza na mtandao huu wamesema ni kweli katika ubora wa usafirishaji kwa njia ya mabasi nchini, Shabiby Line wako vizuri sana.

Wakati huohuo, hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) ilisitisha leseni ya kutoa huduma ya usafiri kwa mabasi 22 kwa kosa la kuingilia mfumo wa kufuatilia mwenendo wa usafiri wa magari.

Katika adhabu hiyo, Kampuni ya Shabiby Line haikuguswa kutokana na uongozi wake kuwa makini na maelekezo ya Taboa na Serikali-TAARIFA HII NIMEIPATA KATIKA MAMLAKA YA UHAKIKA.
Shabiby-Line-Bus.jpg
 
Dodoma Arusha.....machame waliishika hii njia ila siku hizi wameanza kuboa wanakata tiketi zaidi uwezo wa gari hasa kwa Safari za jioni dodoma to Arusha
 
Back
Top Bottom