Ushauri wangu kwa Balozi Sirro

Idofu

Senior Member
Oct 24, 2022
108
187
Ni kuwa ni bora Uchutame, Serikali nzima wanajua nini kilitokea kwenye kwenye Mfuko wa Kufa na Kuzikana,na pia ni nini kilitokea kwenye Mfuko wa Tuzo na Tozo!!

Ni kuwa mpaka Mh.Rais anakuondoa kwenye nafasi yako alikuwa amejiridhisha kwa kile kilichotokea!!

Vile vile,umedanganya kuwa ulimtuma DCI afanye uchunguzi kitu ambacho sio kweli,ulichomfanya ni kumchukua Ofisa aitwaye ACP Nyakulinga kutoka kwenye Ofisi yako ya IGP na kumtuma aende akakamate watendaji wa Mfuko Zanzibar na kuwapeleka Mahakamani, na hizo kesi zote hakuna kinachoendelea tangu zilivyofunguliwa January, 2022.

Huyu Nyakulinga,wasiomjua ni kuwa aliondolewa na Rais JPM kutoka katika Ofisi ya Financial Crime Unit,baada ya malalamiko mengi ya rushwa katika Ofisi hiyo.

Kikubwa kinachokupa jeuri ni baada ya kumtorosha Mtendaji Mkuu wa huo Mfuko, ambaye alikuwa ndio mhusika Mkuu wa Kazi zote za kila Siku za Mfuko na aliondoka na documents zote, na hata CAG alivyokuja kukagua hakupata hata document Moja ya mfuko tangu ulivyoanzishwa.

Ushauri wangu ni huu, utulie, zile Kesi za Zanzibar zinakutaka ufike Mahakamani utoe ushahidi Kama Mlezi wa Mfuko.

Usimchokoze Mh. Rais, kitu ambacho alishakisahau!
 
Kwa hiyo Tanzania ukiiba au kukosea unawajibishwa kwa kupelekwa kwingine ukaibe pia si kuchukuliwa hatua na kurudisha ulichoiba. No wonder TZ ni ...
 
Kwa hiyo Tanzania ukiiba au kukosea unawajibishwa kwa kupelekwa kwingine ukaibe pia si kuchukuliwa hatua na kurudisha ulichoiba.
No wonder TZ ni ...
Ulifuatilia kwa kina,hicho Kipindi alikilipia,na kikubwa ni kuonyesha kutokubaliana na maamuzi ya Mh.Rais!!

Yeye alishastaafu na kuagwa rasmi ndani PT!! Uliona wapi mstaafu anafanyiwa interview ya namna ile!!

amwache IGP Mpya afanye Kazi,aache kumwingiza kwenye Mambo ambayo yeye aliyaboronga akiwa kwenye kiti!!
 
Sema wewe mtoa Mada kuwa KAMBA YAKO ILIKUWA FUPI MNO NA ILIKUWA INAKURUHUSU AT 45 DEGREES ONLY
 
Sema wewe mtoa Mada kuwa KAMBA YAKO ILIKUWA FUPI MNO NA ILIKUWA INAKURUHUSU AT 45 DEGREES ONLY
Ndio maana,wengine tunashangaa alivyosema yeye alikuwa Muadilifu!!

Muadilifu gani anaweza kujenga nyumba kwenye kila mkoa?,hizo fedha alimezipata wapi?
 
Sema wewe mtoa Mada kuwa KAMBA YAKO ILIKUWA FUPI MNO NA ILIKUWA INAKURUHUSU AT 45 DEGREES ONLY
Sio kana Kwamba tunamuonea hapana,amejichanganya alivyosema yeye ni Muadilifu,tunaomjua tunashangaa amepata wapi kiburi na uajasiri wa kuzungumza hayo?

Ona hii kwanza hapo chini,hapa ni Mkoa wa Kusini Unguja,alivyoingia tu wakafufua akaunti iliyofungwa na kuiba fedha zote hizo!!,hii akaunti fedha zote hizo 900M zimeliwa na zilikuwa zinaingizwa kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Wahusika wakuu akiwa yeye Sirro,Meneja Mkuu wa Mfuko ambaye ametoroshwa,Makamishna wote waliopita Zanzibar Kati ya Mwaka 2018-2021,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kati ya 2018-2021.

Walichofanya Sasa walipoona Mambo yamekuwa mabaya,wakawakamata wale Askari wadogo ambao walikuwa Signatory na wakawafukuza Kazi na kuwapeleka Mahakamani,lengo likiwa ni kuficha dhambi zao na kwa kuwa hao Askari hawana mtetezi basi ndio imetoka hiyo.

Ndio maana tunaomfahamu,tunashangaa huo uadilifu ameutoa wapi?,na ina Maana Mh.Rais alikosea kumtoa kwenye cheo chake Cha awali?

IMG-20230523-WA0054.jpg
 
Ni kuwa ni bora Uchutame, Serikali nzima wanajua nini kilitokea kwenye kwenye Mfuko wa Kufa na Kuzikana,na pia ni nini kilitokea kwenye Mfuko wa Tuzo na Tozo!!

Ni kuwa mpaka Mh.Rais anakuondoa kwenye nafasi yako alikuwa amejiridhisha kwa kile kilichotokea!!

Vile vile,umedanganya kuwa ulimtuma DCI afanye uchunguzi kitu ambacho sio kweli,ulichomfanya ni kumchukua Ofisa aitwaye ACP Nyakulinga kutoka kwenye Ofisi yako ya IGP na kumtuma aende akakamate watendaji wa Mfuko Zanzibar na kuwapeleka Mahakamani, na hizo kesi zote hakuna kinachoendelea tangu zilivyofunguliwa January, 2022.

Huyu Nyakulinga,wasiomjua ni kuwa aliondolewa na Rais JPM kutoka katika Ofisi ya Financial Crime Unit,baada ya malalamiko mengi ya rushwa katika Ofisi hiyo.

Kikubwa kinachokupa jeuri ni baada ya kumtorosha Mtendaji Mkuu wa huo Mfuko, ambaye alikuwa ndio mhusika Mkuu wa Kazi zote za kila Siku za Mfuko na aliondoka na documents zote, na hata CAG alivyokuja kukagua hakupata hata document Moja ya mfuko tangu ulivyoanzishwa.

Ushauri wangu ni huu, utulie, zile Kesi za Zanzibar zinakutaka ufike Mahakamani utoe ushahidi Kama Mlezi wa Mfuko.

Usimchokoze Mh. Rais, kitu ambacho alishakisahau!
Kumekuchaaaa !!!

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom