ushauri wanajf.

Salanga

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
364
44
poleni sana kwa mgao wa umeme tusiojua mwisho wake. Mimi nna mpango wa kujenga nyumba miaka ijayo maeneo ya vikindu mkuranga pwani. na sasa nasoma huku nikikusanya pesa taratibu. napenda kuomba ushauri wa namna ya kuhifadhi pesa hizo. wazo langu ilikuwa ni kununua viwanja kadhaa halafu baadaye niviuze kwa kwa faida dheni nijenge ktk kiwanja changu nilicho nacho tayari. wazo jingine ni kufungua fixed account katika pesa za kigeni ktk benki ambayo ina riba kibwa zaidi hapo tz. tafadhali wanajf naomba mwazo yenu ni nitawaweza kufanikisha hili; je benki gani wanatoa riba kubwa na ktk sarafu ipi? je ongezeko la bei za viwanja dar na pwani linazidi riba zitolewazo na mabenki ktk fixed account? NAWASILISHA...
 
Go ahead, idea ya kufuatilia benki gani wanatoa interest nzuri kama ukiweka fixed deposit ni njema sana, mimi sijui but fuatilia via websites au face-to-face visit.
 
thamani ya ardhi inakua kuliko riba ya fixied account. hatari ya kiwanja ni pale papa msofe akikitamani kukifanyia u-tapeli, kuwa mwangalifu kwa kila unalolifanya utaongeza nafasi ya mafanikio.
 
Salanga una mawazo mazuri sana lakini unahitaji wataalamu wakushauri kuhusu mambo ya uwekezaji. Kwanza kitu cha kujiuliza unazo pesa kiasi gani za kuwekeza. Real estate ni mkombozi wako lakini unapaswa ujue mchezo wake. Pili huko unapotaka kununua kiwanja na kujenga nyumba ni sehemu ambayo utapata mapato kidogo sana kama utapangisha hiyo nyumba yako. Kwenye real estate location ni muhimu kama unazo hela nyingi nunua nyumba au kiwanja sehemu nzuri. Usiwekeze hela zako nyingi benki kwani mfumuko wa bei utazifanya pesa zako zisiwe na thamani. Mfano mwaka 1983 nilichonga kitanda kwa sh. 1,400.00 kama ningeziweka benki sasa hivi hata mkate ningeshindwa kununua acha kitanda. Kama unatafuta mbinu zaidi za kuwekeza pesa zako naomba tuwasiliane kwa simu namba 0755394701
 
Asanteni sana kwa mawzo yenu yanayotia moyo. Mtaalamu Charles na wengine Vikindu ni sehemu inayokua na inaitwa Vikindu Jesus town na mwanzilishi wa sehemu hiyo ambayo ilikuwa vchaka nyakati hizo. Nina taarifa za kujengwa kwa tawi la chuo cha SAUT kwa Dar, State university of Afrika na opportunity nyingine nyingi. Zaidi ya hayo wajanja kama akina Tibaigana waliwahi na kujenga hotel huko, huwezi amini ,pia kuna tetesi kuwa sehemu hiyo itaingizwa katika mkoa wa Dar, there is something there.now watch out.
 
Tunashukuru kwa taarifa kuhusu Vikindu. Ila acha kula riba, wekeza katika miradi utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom