Ushauri wana jf! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wana jf!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Mar 31, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuna jamaa yangu best sana tangu primary!tulipotezana kwa mda baada ya yeye kuendelea na masomo.Baadae nilisikia yupo Uganda anafanya biashara kwa mda mrefu.Baada ya kitambo cha miaka kazaa aliamua kuachana na ubachera(single) na kutafuta mchumba.Njia aliyotumia ilikuwa ni kuchati kwenye mitandao si mda mrefu akafamiana na binti mmoja mkazi wa Nyamagana mjini mwanza.Binti huyu ni mwalimu.Awali binti alimwambia jamaa kuwa alikuwa na mahusiano na jamaa furani ila baada ya miaka kazaa walipotezana kwa sababu ya majukum ya hapa na pale.Inshu ni kwamba jamaa alidoo na huyo binti baada ya kukutana hawakutumia mpira.Tangu hapo walikuwa marafiki sana mpaka wakaamua kufunga ndoa.Cha ajabu jamaa yangu anakataa mtoto kuwa si wakwake kuwa ametwishwa mzigo.Baada ya kumliza kwa undani zaidi alisema kuwa alikutana na huyo binti kimwili tar 6 April 2010 na mtoto amezaliwa tar 27december2010.Kwa maelezo yake jamaa anasema kuwa binti alishamueleza kuwa anaingia mwezini kati ya hizi tarehe kila mwezi 25,27,29,au 1.Sasa jamaa ameamua kumkataa kwa kudai kuwa mtoto si wake kwa kuwa siku na tareh haviendani kwa mtoto kuzaliwa.Wana jf ushaurii tafadhali
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Labda ni premature.Alivyoenda kavu alikua anategemea nini?Alafu kama walikuta april wamepata wapi muda wa kujuana vizuri mpaka kuoana?
   
 3. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Kwa nini umekosa uaminifu huo
  kama walidu tarehe 6 April na aliona period tarehe 25 March kwa nini anasema tarehe haziendani
  Mtoto ni wake aache ukora
  Hii tabia ya kukataa watoto inazidi wanaume acheni hizo watoto wakishakuwa wakubwa
  ndio mnawataka
   
 4. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Mpz Lizzy
  Walifahamiana kwenye mtandao walipokutana april ilikuwa kumaliza game
   
 5. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asanteni kwa ushauri yeye anadai walijuana kwenye mtandao!kikubwa zaidi anasema kuwa siku yaani miezi tisa kama wanavyodai hazijatimia zingetimia january 6 au ikawa mbele zaidi!
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hiyo nimeona mami...ila hakutaka kujuana live hata kidogo?Alafu kama wameoana akiwa tayari na mimba iweje akatae mtoto sasa hivi?Maana ukienda hosp unaweza kujua muda ina muda gani kwahiyo wanaweza kukadiria hata tar!Yani hawa wanaume wa hivi wana mambo...STAREHE NDIO...MAJUKUMU HAPANA!
   
 7. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Black woman yeye anavyodai ni kuwa tarehe hizo ameambiwa na mke wake baada ya kuoana hapo awali alikuwa hajui chochote kuhusu piliod maana jamaa mda mrefu anakuwa Uganda hivyo ni kuja na kuondoka anaweza kukata miezi kama sita had saba bila kuja tz wakati mwingine huwa anaelekea Ulaya kwa mda mrefu bila kurudi nyumbani
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hamjawahi kusikia neno premature au njiti kwa lugha yetu?
   
 9. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dada Lizzy Swali kubwa ambalo linamsumbua kichwani kila ninapompa ushauri ni kwamba kuwa jamaa anasema kuwa mtu anaweza kuingia tarehe 25march na akapata mimba tarehe 06 april!hilo ndo swali kila kukicha nikimshauri hakubali
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kama hamtaki mtoto kwa sababu zingine aseme, wengine wanatamani sana hao watoto na kuwahangaikia.
  Ila habari ya kujifanya anajua mzunguko wa period wa huyo dada kama vile anaenda yeye mwezini aache..kwanza anajua ni mzunguko mrefu au mfupi?anajua mzunguko unaweza kutofautiana kwa sababu kadhaa? alivyofanya kavu alitegemea ametoa mapovu?pia kubeba mimba anajua ni wiki ngapi?na kwamba inaweza isitimie miezi 9...Pheew! hayuko tayari kimalezi na aache sababu za kijinga!!
   
 11. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana Belinda kwa ushauri wako nitamfikishia jamaa yangu ujumbe huu!maana anakuwa mbishi ka nini!
   
 12. F

  Fay2011 Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi si akapime DNA ili awe na uhakika kama mtoto ni wake ama la! Hata hivyo kitanda hakizai haramu huyo mtoto amtunze tu whether wake au sio wake kwani tayari ameshazaliwa ndani ya ndoa yake.
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  sio lazima mimba ifikishe miezi 9. lakini kama wasiwasi umezidi si akapime DNA?
   
 14. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyo kesha mchoka huyo mama hivyo anatafuta tu sababu za kuachana naye,hana lolote hivyo vingine ni visingizio tu
   
 15. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  jamani mimi sioni tatizo ni nini hapa,
  mwende mkapime DNA,mmalize hicho kizungumkuti!
   
 16. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  punguza jazba kidogo BJ,
  Upo poa lakini?
   
 17. e

  ejogo JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama mama aliingia kwenye moon tarehe 25 march na akakutana na jamaa tarehe sita April, kimahesabu ni possible kupata mimba. lets say anableed kwa 5 days, maana yake mpaka tarehe 30, then kunakuwa na siku kama 5 hapo zipo powa tu, maana yake ni mpaka tarehe 4 April. then kuanzia siku ya 11 mara nyingi haishauriwi kudo kavukavu kama hamna lengo la kufanya uumbaji, that's to say kuanzia tarehe 5 april. na kama wali do tarehe 6 April maana yake ni siku ya 12. so mathematically ni likely kuwa uumbaji ulifanyika. Biologically, yai la mama hushuka siku ya 14 kwa mzunguko wa kawaida, siku ya 15 kwa mzunguko mrefu, na siku ya 13 kwa mzunguko mfupi. Sperm zinauwezo wa kuishi mpaka masaa 36. So, ukichukulia kimahesabu na kibiologia, kwa tarehe hiyo ni likely kuwa uumbaji ulifanyika.

  Ukipigia hesabu siku ya kuzaliwa mtoto mara nyingi jumlisha siku 14 au toa siku 14(expected date + - 14). ukienda kimahesabu hayo huyo mtoto naona amezakiwa mwake kabisa.

  Kama kuna more doubts wakafanye DNA test.
   
 18. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Bacha niaje?powa nimepunguza, si unajua jamaa anabisha kama vile DNA imemhakikishia mtoto si wake? angetumia kinga je ingekuwaje??
  Powa, enjoy your weekend mkuu...tc
   
 19. RR

  RR JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Mtoto anazaliwa kati majuma 38 (kuanzia aprili 6 hadi desemba 27) hadi majuma 42 wakati mwingine.
  Kiutalaamu inawezekana kabisa mtoto ni huyo jamaa...mahesabu ya tarehe na muda wa ujauzito yanatoa nafasi kubwa sana kwamba mtoto ni wa jamaa, labda kama kuna mashaka mengine....kuondoa mashala apime DNA (ila ina madhara ya muda mrefu sana ikiwa itathibitika mtoto ni wa jamaa).

  ....source
   
 20. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyo kaka aache ushamba, kama kweli ana nia ya kujua mtoto wa nani si kuna DNA, akapime. Unless hana hela, niko tayari hata kuchanga ili ukweli ujulikane. wanaume siku hizi wamezidi sana kutwa wangu wangu kukatika bila Condoma end of the day unaanza kufanya hesabu za kipuuzi, siku za mwenzio anazijuaje? Ama kweli ushamba hauna kwao kwa huyo mkaka nafikiri umeota mizizi.

  Ole wako wewe mama kama umemsakizia mwenzio unaumbuka. DNA yaja hiyo!
   
Loading...