Ushauri wako ni muhimu sana hapa...

Ushauri wako ni muhimu sana hapa...

Ihwa jnr

Member
Joined
Feb 4, 2014
Posts
19
Reaction score
14
Natumai mko salama wapendwa katika Bwana na mnaendelea vyema na shugHuli zenu za kila siku na ujenzi wa taifa hili.

Nimehitimu stashahada ya ualimu katika chuo kimoja hapa nchini,kwa bahati mbaya nilifeli vipindi viwili yaani Curriculum na PE (Phsical Education) hivyo sikuweza kuajiriwa ingawa sikufeli vile vipindi vya kufundisha darasani.

Baada ya hapo ilinibidi nitafute kazi kwenye hizi taasisi binafsi na kufanikiwa ambako nimefanya kazi kwa takribani miaka miwili na baada ya mambo kuwa mengi na kama mnavyojua kazi hizi za sekta binafsi ilinibidi niache kazi...

Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijiendeleza katika chuo kimoja hapa Dar nasoma Diploma ya mambo IT huku nikijaribu kutafuta kazi ya kufanya ingawa nayo ni ngumu kupata...

Haja yangu kwenu ni kuomba ushauri,Je naweza tokana vipi na hii hali ya ukosefu wa ajira au naweza fanya nini kuepukana na hii hali ninayokumbana nayo kwa sasa
 
Kuondokana na hali ngumu ni issue ila kuipunguza inawezekana:

Si una experience ya kufundisha tayari?tafuta center hizi za kureseat wanaita qt sijui,zipo nyiingi siku hizi as ujuavyo dv 5 wanaongezeka kila mwaka na huko hawazingatii sana ubora wa waalim kwa nahisi watakubeba

We mwenyewe unaweza kujitaftia wanafunzi ukawa unawapiga tuition unapata vijisent

Vishule uchwara vipi vingivingi huko nako jaribu.........................taka nini tena kijana
 
Natumai mko salama wapendwa katika Bwana na mnaendelea vyema na shugHuli zenu za kila siku na ujenzi wa taifa hili,Nimehitimu stashahada ya ualimu katika chuo kimoja hapa nchini,kwa bahati mbaya nilifeli vipindi viwili yaani Curriculum na PE (Phsical Education) hivyo sikuweza kuajiriwa ingawa sikufeli vile vipindi vya kufundisha darasani,Baada ya hapo ilinibidi nitafute kazi kwenye hizi taasisi binafsi na kufanikiwa ambako nimefanya kazi kwa takribani miaka miwili na baada ya mambo kuwa mengi na kama mnavyojua kazi hizi za sekta binafsi ilinibidi niache kazi...

Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijiendeleza katika chuo kimoja hapa Dar nasoma Diploma ya mambo IT huku nikijaribu kutafuta kazi ya kufanya ingawa nayo ni ngumu kupata...

Haja yangu kwenu ni kuomba ushauri,Je naweza tokana vipi na hii hali ya ukosefu wa ajira au naweza fanya nini kuepukana na hii hali ninayokumbana nayo kwa sasa


Mkuu uzoefu wako wa kufundisha ni mtaji toshaa saana, hapa mjini na tena hesabu kuwa wewe ni tajiri baada ya miaka 2 hapo baadae. Hebu jitangaze kuwa unafundisha tusheni na utapata wanafunzi wengi sana kwani wazazi wengi wanahangaika kutafuta walimu wa tusheni.Anzia mtaani kwako unakoishi. Kama huna eneo la kufundishia, nakushauri utafute yale mabanda ya kuoneshea mpira halafu ingia nao ubia wa kutumia hilo banda mida ambayo hawaoneshi mpira.
 
Tafuta jamaa wa teachers junction wao wamemwaga nafasi za shule mbalimbali hapo dsm no yao ya simu ni 0753810857 watakusaidia.
 
Walimu walokwenda kufanya interview leo 08,04,2014.
Reminant tabata,Zabikha Islamic Kinyerezi na Centennial Seminary.
Mungu awaongoze.

Kwa wale wa kesho interview ya Agape High School iko pale pale pamoja na ya Reminant.
Jitahdi kufika kabla ya saa tatu.
Mungu atuongoze kwa kila jambo
0753-810857
 
nenda chuo ukakilie masomo yako acha uvivu la sivyo utaendelea kuteseka na kuwa kuli huku unayonafasi ya kumaliza tatizo na kupata ajira ya kudumu. Achana na kufundisha sasa toka mjini rudi chuo umalizie viporo utapangiwa shule direct,acha uvivu nenda shule haraka,ungekuwa mdogo wangu,ningekupatia makofi mawili tu,utie akili,acha uvivu wewe.
 
Back
Top Bottom