Ushauri wako ni muhimu katika hili

Joninho

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
559
611
Habari wadau wote wa JF ni matumaini yangu mko salama Kwa uwezo wake Mwenyezi mungu, heshima kwenu wote.

Naomba kuwasilisha swala hili mahali hapa kwani nafahamu humu Kuna watu walio yapitia mengi, hivyo wengi mnauzoefu wa maswala mengi.

Baada ya kuhitimu shahada yangu ya kwanza nili rejea nyumbani kama mjuavyo ajira ni ngumu sana Kwa wakati huu, hivyo mzazi wangu alinipatia shilingi milioni mbili nianzishe shughuli yoyote maeneo ya karibu na nyumbani, hasa ufugaji wa kuku wa nyama sababu mabanda yapo na kabla ya kwenda chuoni mwaka 2014 ndio kazi Nilifanya nilipo malizia kidato cha Sita wakati nasubiri majibu na ilikua ina nilipa na soko nilauhakika.

Ila baada ya sasa kupewa hii pesa niliwasiliana na rafiki angu nilie maliza nae chuo tuka shauriana kutafuta shamba maeneo ya Morogoro tukaanzishe kilimo cha umwagiliaji, yeye atoe shilingi laki 7 na mimi hivyo hivyo.

Hapo ilibidi ni mgusie mzee wangu azma yangu ya kwenda kufanya kilimo hakuonyesha kuniunga mkono ktk jambo hilo.

Naomba ushauri wenu ktk jambo hili wadau maana pesa yenyewe ndio hiyo hiyo.
 
Ila baada ya sasa kupewa hii pesa niliwasiliana na rafiki angu nilie maliza nae chuo tuka shauriana kutafuta shamba maeneo ya Morogoro tukaanzishe kilimo cha umwagiliaji, yeye atoe shilingi laki 7 na mimi hivyo hivyo,.
Hapo ilibidi ni mgusie mzee wangu azma yangu ya kwenda kufanya kilimo hakuonyesha kuniunga mkono ktk jambo hilo.
Naomba ushauri wenu ktk jambo hili wadau maana pesa yenyewe ndio hiyo hiyo.

Nijibu maswali haya kwanza

1. Unataka kulima nini?

2. Una mtu wa kuaminika ambaye atakuwa shamba full time Au nyie ndio mtakuwa mnakaa shamba?

3. Soko la zao lako umesha lijua? Unajua misimu ya hilo zao sokoni?

4. Mzee amekupa sababu zipi za kutokuunga mkono hili wazo lako?
 
Kwasababu Mzee amekupa pesa kwa malengo tofauti na kilimo, nakushauri no bora ufanye kile mabacho Mzee amekupea fedha for.....
Kumbuka huko uendapo unaenda kuanza moja kwamaana ya kwamba kujitegemea kwa kilakitu na pia, Mzee hatiweza kuona like unacho kifanya hata kama utapata hasara kwake haitokua rahisi kukuamini kwasababu hajaina kwa macho.
Pia usijaribu kuharibu uhusiano wako na Mzee wako, eti kwasababu ya rafiki ambae hata asingeweza kukukopesha hiyo milioni mbili.
Kaa nyumbani na fanya hicho ulicho kubaliana na Mzee, na hata ikitokea hasara Baba hawezi akakulaumu kwasababu ameona kwa macho.
Na kwakufanya kile mlicho kubaliana na Mzee inajenga imani na kufanya Baba aone kwamba u-mtiifu na mwenye kumuheahimu.
 
Wazazi wakati fulani wamekua chanzo cha kuwarudisha nyuma watoto wao kimaendeleo.

Chakukushauli ikiwa umejiridhisha kabisa kua moro kinakufaa Ongea naye kwa ustaarabu mwambie ,funguka tu kua mzee naenda kufanya maisha kwa ajili yetu sisi.

Mwambie tu akubarikie. Kama utaharibikiwa nabado ajue kua maishabyanaitaji kufanya mara tatu nyingi kshindwa ,mara nyingi zaidi kushinda.
 
Nijibu maswali haya kwanza

1. Unataka kulima nini?

2. Una mtu wa kuaminika ambaye atakuwa shamba full time Au nyie ndio mtakuwa mnakaa shamba?

3. Soko la zao lako umesha lijua? Unajua misimu ya hilo zao sokoni?

4. Mzee amekupa sababu zipi za kutokuunga mkono hili wazo lako?

1)kulima vitunguu mkuu
2)tutakua ni sisi wenyewe
3)soko bado sijalifahamu mkuu
Na msimu maeneo hayo unaanza mwezi wa nne
4)hakunipatia sababu mkuu alicho nieleza nikuwa ni fanye ufugaji sababu soko lipo la kutosha nasio kwenda kuanzisha jambo jipya mkuu.
 
Kwasababu Mzee amekupa pesa kwa malengo tofauti na kilimo, nakushauri no bora ufanye kile mabacho Mzee amekupea fedha for.....
Kumbuka huko uendapo unaenda kuanza moja kwamaana ya kwamba kujitegemea kwa kilakitu na pia, Mzee hatiweza kuona like unacho kifanya hata kama utapata hasara kwake haitokua rahisi kukuamini kwasababu hajaina kwa macho.
Pia usijaribu kuharibu uhusiano wako na Mzee wako, eti kwasababu ya rafiki ambae hata asingeweza kukukopesha hiyo milioni mbili.
Kaa nyumbani na fanya hicho ulicho kubaliana na Mzee, na hata ikitokea hasara Baba hawezi akakulaumu kwasababu ameona kwa macho.
Na kwakufanya kile mlicho kubaliana na Mzee inajenga imani na kufanya Baba aone kwamba u-mtiifu na mwenye kumuheahimu.
Sawa mkuu nimekuelewa.
 
Habari wadau wote wa JF ni matumaini yangu mko salama Kwa uwezo wake Mwenyezi mungu, heshima kwenu wote.

Naomba kuwasilisha swala hili mahali hapa kwani nafahamu humu Kuna watu walio yapitia mengi, hivyo wengi mnauzoefu wa maswala mengi.

Baada ya kuhitimu shahada yangu ya kwanza nili rejea nyumbani kama mjuavyo ajira ni ngumu sana Kwa wakati huu, hivyo mzazi wangu alinipatia shilingi milioni mbili nianzishe shughuli yoyote maeneo ya karibu na nyumbani, hasa ufugaji wa kuku wa nyama sababu mabanda yapo na kabla ya kwenda chuoni mwaka 2014 ndio kazi Nilifanya nilipo malizia kidato cha Sita wakati nasubiri majibu na ilikua ina nilipa na soko nilauhakika.

Ila baada ya sasa kupewa hii pesa niliwasiliana na rafiki angu nilie maliza nae chuo tuka shauriana kutafuta shamba maeneo ya Morogoro tukaanzishe kilimo cha umwagiliaji, yeye atoe shilingi laki 7 na mimi hivyo hivyo.

Hapo ilibidi ni mgusie mzee wangu azma yangu ya kwenda kufanya kilimo hakuonyesha kuniunga mkono ktk jambo hilo.

Naomba ushauri wenu ktk jambo hili wadau maana pesa yenyewe ndio hiyo hiyo.
wewe upo wapi kijana nikupe akili ya maisha?
 
Back
Top Bottom