BansenBurner
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 6,809
- 5,779
Hapo nimeelewa kitu mkuu hilo ni tatizo kwa baadhi ya TV za Samsung.kuwa makini na maduka ya pale stand na yale maduka madogomadogo.. wanauza samsung na LG. ambazo ni clone.
Bora ununue TCL au Singsung kwa bei poa sio mbaya. mimi nimetumia singsung Led haijaniangusha kabisa.
kuna TV za samsung clone huwezi kutambua kama ni feki tatizo lake kubwa hazina audio output.
Nimeamua kuachana na TV-chogo.... nataka kununua flat screen... wadau wenye kuzijua vizuri... je! aina gani ni nzuri? kwa hapa Arusha zinapatikana duka gani? bei yake tafadhali?
Mkuu niliinunua hiyo TV 2012 JULY pale mlimani city juzi imebuma...
ilianza kujigawa Kati yaani chini inaonesha rangi ya kijani juu blue Mara mda mwingine rangi yote inavurugika kabisa in short ni kero tu nimejaribu mafundi wee wapi nimeamua iweka kando tu...
Basi hili ni tatizo la TV's za Sony, nakumbuka nilipata nayo tabu enzi za Sony Wega!!
Kumbe hawajarekebisha tatizo hilo, lilinitesa sana? Baada ya hapo ndiyo nikapata mzuka wa kupenda vitu used, haya basi sihami kwenye JVC yangu mtumba!! Kitu kipo clear mi nawashangaa mnasema mara LED mara Plasma hata siwaelewi mi najua kitu flat nchi 34 hahahaaaa
Hiyo JVC ulipata wapi na kwa bei gani mkuu??
Ni kastory karefu kidogo ila ni hivi nilikuwa na hela mfukoni kama 1.2 m!! Lengo nipate TV original nikawa nazunguka tuu hapo Dar mara Kariakoo, Samora, Mwenge hata sieleweki!!
Siku hiyo nilipita mitaa fulani ya Msimbazi, ukitoka hapo Uhuru keep left kama unaenda Msimbazi barabara ya pili (kama sijakosea) unakona kuelekea kushoto kuna maduka mengi tu ya Wapemba wanauza used electronics!!
Siku hiyo napita asubuhi sijui hata ninunue TV gani nikawakuta ndo wanashusha mzigo wao toka kwenye kilori! Nikaziona hizo TV za JVC zilikuwa tatu, kwa laki tano na ishirini!!
Nikazipenda nikajibebea, ilikuwa mwanzoni 2013!! Ipo clear sana na haijawahi kunisumbua kwa lolote
Sony bravia 42" kiboko yao alafu pata na home theater yake ya 13000watt hutoki nyumban kudadadeki.
Hzo zingine ni mbwembwe tu za sokon
Samsung hamna kitu yeboyebo tu
Mkuu umevuta yale majani ya mti ulilaaniwa?
Hakuna Home theater ya 13,000 Watts. !!π
Hata zile Speaker za Kupigia ndombolo ndani ya Stages hazijafika huko.
kuwa makini na maduka ya pale stand na yale maduka madogomadogo.. wanauza samsung na LG. ambazo ni clone.
Bora ununue TCL au Singsung kwa bei poa sio mbaya. mimi nimetumia singsung Led haijaniangusha kabisa.
kuna TV za samsung clone huwezi kutambua kama ni feki tatizo lake kubwa hazina audio output.
Kuepuka kuuziwa fake nenda kwa ma Agent wa Samsung wapo kariakoo mkabala na stand ya magari ya daladala yaendayo Gongo la mboto pia watembelee pia maagent wa Lg na Son wapo karibia kila mall za hapa bongo.Led na 3D zenye in built decoder na zenye kusaport Wireless keyboard ni nzuri zaidi