ChickMagnet
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 2,702
- 3,553
Jamani wakuu nahitaji kununua flat tv iwe kati ya sony bravia sumsung au LG inchi 32 anaejua bei zake anisadie au anejua duka lolote linalouza original kwa hapa dsm.
Nenda kariakoo kabla hujafika round about pale kuna duka la Samsung ,
Authorised dealer.
Sasa wakuu nitawezaje kutambua kama ni clone au original
Sai distributors, wapo stendi ya daladala za kwenda Mbagala, mtaa wa Msimbazi,. ni Authorised dealers/services wa SAMSUNG, .... TV 32'' SERIES 4 YENYE KING'AMUZI NI TSH.750,000, BILA KING'AMUZI NI TSH 700,000.... HIZI NI BEI WANAZOANZIA HUWA WANASHUKA KWA MNUNUAJI WA KWELI. SERIES 5 KAMA HIVYO NI TSH 950,000 NA TSH.900,000. NA MODEL WALIZO NAZO NI UA32H4100AK; NA UA32H5100AK. KAZI KWAKO KAKA.
Sony Bravia ni habari nyingine.
Sijakuelewa mkuu zinakua na king'amuzi gani? Halafu series 4 ndo inakuaje na 5 inakuaje mkuu?
Mkuu niliinunua hiyo TV 2012 JULY pale mlimani city juzi imebuma...
ilianza kujigawa Kati yaani chini inaonesha rangi ya kijani juu blue Mara mda mwingine rangi yote inavurugika kabisa in short ni kero tu nimejaribu mafundi wee wapi nimeamua iweka kando tu...
Nikiangalia ung'aavu wake upoje?
Sijaelewa vizuri hapa hebu weka clear mkuu
Ukilinganisha na samsung ipi inakuwa clear sana?
Jamani wakuu nahitaji kununua flat tv iwe kati ya sony bravia sumsung au LG inchi 32 anaejua bei zake anisadie au anejua duka lolote linalouza original kwa hapa DSM.
Aisee, mi niliona jamaa ndo anauza bei cheap, kumbe zipo cheap zaidi ya hiyo, 490000 kwa samsung LEd series 4 zinauzwa wapi kiongozi? Nielekeze nami niwaelekeze wenginesajo
Mbona bado bei yake iko juu TV kama hiyohiyo inauzwa sh 490000/ inch 42 inauzwa sh laki tisa na sitini elfu inch52 inauzwa sh milioni moja na laki mbili.
kiukweli sijawahi kutumia smart tv but nikisoma kwenye mitandao features zake huwa naona kuwa hizo ni Tv classic sana, very smartSmart TV ndo kitu cha ukweli nilikwenda sehemu fulani hivi kunga dish nikaipata nilitamani niendelee kukaa pale niliiungia wireles internet kutoka kwenye kasmartphone kangu nikaanza kukimbizana nayo JF.
Kwanza mwenye nayo alikuwa hajui kama ina mambo makubwa kama hayo asikwambie mtu yaani umekaa kwenye sofa lako na rimot yake iko kama mouse ya wireles mambo ya youtube na mengineyo mengi ni wewe tu na bando la kutosha.
Aisee, mi niliona jamaa ndo anauza bei cheap, kumbe zipo cheap zaidi ya hiyo, 490000 kwa samsung LEd series 4 zinauzwa wapi kiongozi? Nielekeze nami niwaelekeze wengine
kiukweli sijawahi kutumia smart tv but nikisoma kwenye mitandao features zake huwa naona kuwa hizo ni Tv classic sana, very smart