Ushauri: Wabunge wa chadema hemu mjitambue.

Ni wizara ngapi zimepita bungeni huku uwepo wa Lema haujulikani ulipo?

Ina maana huoni umuhimu wa Lema kuwa ndani ya bunge na kutoa mchango wake kwenye hizo wizara zilizo pita bila ya yeye kuwepo?

Wana Arusha mjini angalieni hasara mliyo pata kwa kumchagua huyo mbunge wenu Lema.

We hujapata tu Mume.
Naona full kupapatika
 
Ushauri wa mtoa mada ni mzuri sana. Chadema mnapaswa kuufanyia kazi. So, mnaiga kama wabunge wa ccm hawapo na nyie mnachomoka, mlipaswa kutulia bungeni hata kama wa ccm wamehepa. Msijilinganishe na ccm hata kama wanafanya opp.

ama kweli dunia hii mbuzi watu wengi
 
Hivi sasa bunge la bajeti linaendelea, bunge hili linahitaji umakini na ufanisi wa wabunge ili michango ya wabunge iwe yenye tija na kujenga wanapo ishauri serikali.

106dlxt.jpg
 

Ni vilaza tu ndio wataamini maelezo kwenye hii picha.

Mhe. Wassira akukaimu nafasi ya waziri mkuu, huu ni uongo wa wazi wazi.

Kuhusu kulala, huyu ni mwanaadamu bhana, kwa rundo la shughuli anazo zifanya kwa niaba ya watanzania na wingi wa majukumu kwenye wizara yake, hata ungekuwa wewe ungelala.

Bila shaka hayo maelezo kwenye picha yametolewa na Tanzania Daima, gazeti la udaku na upotoshaji nchini.
 
Kuhusu kulala, huyu ni mwanaadamu bhana, kwa rundo la shughuli anazo zifanya kwa niaba ya watanzania na wingi wa majukumu kwenye wizara yake, hata ungekuwa wewe ungelala.
Mbona JK halali na yeye ni kiguu na njia kila kukicha kama swala ni rundo la shughuli? Nenda kakojoe ukalale wewe gamba!
 
Na huyu pia ni shughukli nyingi za kuwahudumia wananchi zimemfanya kua hivi bungeni?
komba-auchapa-3.jpg
 
Hii hali ya wabunge wa CHADEMA kutumia muda wao mwingi kwenye majukwaa badala ya kuwawakilisha wananchi bungeni ina sikitisha mno.

Ifike wakati sasa wabunge wa CHADEMA wachague moja, kama ni bunge au majukwaa, kwani huwezi kutumikia vyote hivi kwa wakati mmoja.

Hivi sasa bunge la bajeti linaendelea, bunge hili linahitaji umakini na ufanisi wa wabunge ili michango ya wabunge iwe yenye tija na kujenga wanapo ishauri serikali.

Lakini cha kusikitisha wabunge wa CHADEMA wamekuwa 'bize' kwenye majukwaa, hii ina pelekea wabunge wa CHADEMA kukurupuka kuandaa hotuba mbovu na kusababisha gumzo mara kwa mara pindi wanapo ziwasilisha bungeni hotuba zao.

Hivi sasa wabunge wengi wa CHADEMA wamejikita kutetea wagombea udiwani walio wasimamisha kwenye kata zenye uchaguzi mdogo wa udiwani.

Nitoe rai kwa CHADEMA, ni wakati sasa chama chenu kikomae, inapaswa chama kiwaache wabunge watekeleze majukumu yao ya msingi pindi bunge linapo kuwa hai, na chama kiunde kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kampeni, hasa za chaguzi ndogo.
Hebu fikiria mtu kama Lema anaachwa atoe hotuba bila kuandikiwa.....mwishowe anaenda kuropoka tu
 
.

Ifike wakati sasa wabunge wa CHADEMA wachague moja, kama ni bunge au majukwaa, kwani huwezi kutumikia vyote hivi kwa wakati mmoja.

.
SIASA ni mkakati ndugu yangu!
Na nashukuru kwa sababu umetambua kwamba wabunge wa CHADEMA kama hawako BUNGENI basi watakuwa majukwaani!SASA ni zamu ya kutuambia NAFASI ZINAZOOONEKANA WAZI kwenye viti vya wabunge waCCM na CUF wao wanakuwa wapi!?
Sasa hivi ni kampeni za UDIWANI-sawa!Waziri Tizeba na Ngeleja wako kwenye kampeni wakipandikiza chuki na fitina na siyo Bungeni!
Juzi pale Arusha alikuwepo Devotha Likokola, Mwigulu Nchemba ndiye hashikiki kabisa. Ole Sendeka katoka juzi Arusha, Zambi katoka Mbozi juzi juzi tu, Lowassa yuko Makuyuni halafuu ulete mada za kipuuzi puuzi! Mie siungi mkono kutokuwemo bungeni ILA napinga kuwa nje ya bunge kwa ajili ya biashara kama wabunge wengi wa CCM wanavyofanya! CHADEMA endelea maana ukiona hvo mjue magamba washaanza kujutia tamko lao kwamba VYAMA VYA UPINZANI NI VYA MSIMU!
 
CHADEMA si mbadala wa CCM? fanyeni tofauti na CCM basi, maelezo yako yana ashiria kuwa kila lifanywalo na CCM basi CHADEMA mnaiga.
Kuiga si ajabu ILA kunahitajika innovations kwa kile uigacho!
HUONI Mbunge uliyempigia kura (MWIGULU NCHEMBA) kwamba anawaiga akina MAO TSE TUNG?!
Itafikia hatua mtatuambia hata chama kuwa na mwenyekiti na Katibu ni kuiiga CCM!
Mtatwambia kutoa kadi za uanachama, kujenga ofisi,kuzindua matawi, kuwa na bendera, kufanya mikutano ya kisiasa, kupiga kura kura vyote ni kuiiga CCM kisa tu CCM ndicho chama kikongwe nchini!
Kama hayo ndiyo mawazo yako BASI tuisifu CCM kwa ubunifu wake japo IMESHINDWA kubuni namna ya kutumia RASILIMALI WATU NA ASILI KUTUONDOLEA UMASKINI, KUINUA ELIMU NA HUDUMA NYINGINE ZA KIJAMII!
 
Back
Top Bottom