Ushauri wa mh. Freeman mbowe kwa wanachama wa chadema

MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,480
944
"Hawa wanachama wa vyama vingine tusiwaone kama madui, bali tuwaone kama wenzetu ambao hatujafanya jukumu la msingi la kuwahamasisha na kuwaelimisha waweze kuunderstand umuhimu wa kujiunga na CHADEMA.

Tuone kama tunajukumu la ziada, tuna kazi ya ziada ambayo pengine hatujaitekeleza ya kuwashawishi na kuondoa kiza chochote ambacho kiko mbele yao ambacho kinawakwaza katika kujiunga na harakati za CHADEMA.

Tunahitaji kura ya kila mmoja wetu, tunahitaji busara ya kila mmoja wetu, bila kujali dini yake, bila kujali kabila lake,bila kujali itkadi yake ambayo siku zote alikuwa anaisimamia.

Basi niwaombe Watanzania wenzangu, endeleeni kuwaelimisha hawa wenzetu walio ktk vyama vingine,

endeleni kuwavumilia,

endeleeni kuzisikiliza hoja zao za msingi, yapo mambo mengine ya msingi wa hoja nayo,

pale wanapokosoa tuwaelewe,

tuwaelewe kuwa wanaweza
kuwa wanakosoa kwa nia njema, au wanaweza kuwa wanakosoa kwa misingi ya tumikia kafiri upate mradi wako.

Tukubali yote hayo ni sehemu ya siasa".

Tuzingatie hili wanaCHADEMA wenzangu ili kuzidi kuimarisha chama.
 
Ni ukweli usiopingika ingawa mnapaswa kuwa makini na nyemelezi na mapandikizi wanaotumwa kuwahujumu kwenye upinzani kama ilivyotokea kwa akina Mrema, Seif, Cheyo, Kaboro na wengine.
 
Hawa wanachama wangine sawa,lakini mtu kama Nape na jopo lake siwezi kuwasikiliza kabisaaaaaa!!!hata kwa dawa.
 
Maneno haya yako kwenye hotuba ya Mbowe kwa wanachama wa Marekani! Ni moja ya hotuba nzuri sana iliyojaa hekima za kiuingozi! Ndio maana nasema hapa kuwa Mbowe bado ni jiwe imara!

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Nawiwa kukushukuru tena Mohamed kwa ile clip.

Ile hotuba ya DMV ni hotuba makini kwa miaka 50 ijayo!

Kuna kitu kimoja ambacho Mh: Mbowe, Dr. Slaa, Mhe Mnyika na Mhe Lissu wanacho ambacho ni nadra sana. Wana kujitolea na kuipenda kwa dhati kabisa nchi hii. Kiwango chao cha uzalendo ni kikubwa mno na wana hekima sana. Wao sio viongozi kwa madaraka tu bali zaidi ni kwa utashi na upendo wao. They have won my approval, in short.
 
Tatizo la ndugu zangu WanaChadema hawana uvumilivu huo. Kila napowasoma ni kutangaza Uadui tu.. Hivi kweli mtu utaweza vipi kupata kura za Ushindi ikiwa unajenga uadui? Mheshimiwa Mbowe nakusifia kwa haya na hakika wewe kingozi kat ya viongozi walioshiba kisiasa. CHUKI za watu zitakibomoa chama hiki na wala haitatoka nje isipokuwa kuna hatari kubwa Uchadema utatumaliza wenyewe kufikia 2015.
 
mkandara wewe ni great thinker ,lakini nataka nikueleze jambo ,hapa jf kuna watu wako rasmi kama sio kikazi wanayumbisha wana mageuzi or say wanachadema ,kwa hiyo saidia kuona wana cdm .wanangamua hilo hapa jf,ikiwezekana kutochangia threads zinanzo anzishwa makusudi kuchanganya ili kupelekea kufikiwa lengo la mwanzisha hoja ,i mean inaitajika hekima na busara zaidi ,
 
Hakika freeman mbowe ana hekima sana!
Timesikia maneno yako na tutayafanyia kazi!
 
mkandara wewe ni great thinker ,lakini nataka nikueleze jambo ,hapa jf kuna watu wako rasmi kama sio kikazi wanayumbisha wana mageuzi or say wanachadema ,kwa hiyo saidia kuona wana cdm .wanangamua hilo hapa jf,ikiwezekana kutochangia threads zinanzo anzishwa makusudi kuchanganya ili kupelekea kufikiwa lengo la mwanzisha hoja ,i mean inaitajika hekima na busara zaidi ,
Mkuu nakuelewa sana unapotokea.. Kitu kimoja ambacho naomba sana mnielewe nacho ni hivi.. Kama kuna mtu wa CCM anakitukana chama chetu, hatuna sababu ya sisi pia kuweka chuki juu yake isipokuwa kumvuta kwa mazuri yetu sisi. Kama unamkumbuka kuna mada fulani alianzisha zomba akapigwa madongo kwa sababu yeye ni CCM lakini watu wakasahau kwamba hapa tunazungumzia haki ya utawala kwa wale waliofungwa jela kwa siku 8 pasipo kufunguliwa mashtaka. Kwa nini nasi tuwe kina Zomba wa Chadema?.. ndio tutapendewa zaidi? au tutawachosha watu watafikiri hata sisi ni sawa na kina Zomba tumejawa chuki mioyoni.

Hivyo huwa sioni sababu ya WanaChadema kujaribu kuwa kama wanaCCM, Sisi tuna katiba yetu, tuna kanuni zetu, tuna ilani zetu hivyo nfio mwanga wetu na sio kufuata wanayoyafanya CCM..CCM kazi kubwa walokuwa nayo ni kuivuruga Chadema nasi hatuwezi kupoteza dira yetu ktk kukijenga chama kwa ushindani w akijinga tugeuze kuwa vita yetu kuwa ya kuwavuruga CCM pia.. Hapana Chadema inatafuta kuchukua uongozi mwaka 2915 inatafuta kura za wananchi na hivyo hata wale walioko CCM, CUF na TLP tunahitaji ridhaa yao siku ya kura - Tuwavute kwetu badala ya kuwatosa.
 
Mwaka huo uliouandika nakubaliana na wewe lakini 2015 ni ndoto chadema kuchukuwa nchi.

Zomba hana chuki na chadema au mwana chadema isipokuwa Zomba hakubalini na namna chadema wanavyoendesha siasa zao. Kwa mtazamo wangu, viongozi wa chadema wapo ki maslahi yao zaidi ya kutaka maslahi ya wengi. Mifano ni mingi tu, msome TUNTEMEKE.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakuelewa sana
unapotokea.. Kitu kimoja ambacho naomba sana mnielewe nacho ni hivi..
Kama kuna mtu wa CCM anakitukana chama chetu, hatuna sababu ya sisi pia
kuweka chuki juu yake isipokuwa kumvuta kwa mazuri yetu sisi. Kama
unamkumbuka kuna mada fulani alianzisha
zomba
akapigwa madongo kwa sababu yeye ni CCM lakini watu wakasahau kwamba
hapa tunazungumzia haki ya utawala kwa wale waliofungwa jela kwa siku 8
pasipo kufunguliwa mashtaka. Kwa nini nasi tuwe kina Zomba wa Chadema?..
ndio tutapendewa zaidi? au tutawachosha watu watafikiri hata sisi ni
sawa na kina Zomba tumejawa chuki mioyoni.

Hivyo huwa sioni sababu ya WanaChadema kujaribu kuwa kama wanaCCM, Sisi
tuna katiba yetu, tuna kanuni zetu, tuna ilani zetu hivyo nfio mwanga
wetu na sio kufuata wanayoyafanya CCM..CCM kazi kubwa walokuwa nayo ni
kuivuruga Chadema nasi hatuwezi kupoteza dira yetu ktk kukijenga chama
kwa ushindani w akijinga tugeuze kuwa vita yetu kuwa ya kuwavuruga CCM
pia.. Hapana Chadema inatafuta kuchukua uongozi mwaka 2915 inatafuta
kura za wananchi na hivyo hata wale walioko CCM, CUF na TLP tunahitaji
ridhaa yao siku ya kura - Tuwavute kwetu badala ya kuwatosa.

Mkuu nadhani umemaanisha 2015 na sio 2915. Tusije kurudi nyuma Mkuu
 
"Hawa wanachama wa vyama vingine tusiwaone kama madui, bali tuwaone kama wenzetu ambao hatujafanya jukumu la msingi la kuwahamasisha na kuwaelimisha waweze kuunderstand umuhimu wa kujiunga na CHADEMA.

Tuone kama tunajukumu la ziada, tuna kazi ya ziada ambayo pengine hatujaitekeleza ya kuwashawishi na kuondoa kiza chochote ambacho kiko mbele yao ambacho kinawakwaza katika kujiunga na harakati za CHADEMA.

Tunahitaji kura ya kila mmoja wetu, tunahitaji busara ya kila mmoja wetu, bila kujali dini yake, bila kujali kabila lake,bila kujali itkadi yake ambayo siku zote alikuwa anaisimamia.

Basi niwaombe Watanzania wenzangu, endeleeni kuwaelimisha hawa wenzetu walio ktk vyama vingine,

endeleni kuwavumilia,

endeleeni kuzisikiliza hoja zao za msingi, yapo mambo mengine ya msingi wa hoja nayo,

pale wanapokosoa tuwaelewe,

tuwaelewe kuwa wanaweza
kuwa wanakosoa kwa nia njema, au wanaweza kuwa wanakosoa kwa misingi ya tumikia kafiri upate mradi wako.

Tukubali yote hayo ni sehemu ya siasa".

Tuzingatie hili wanaCHADEMA wenzangu ili kuzidi kuimarisha chama.

Very good and well delivered.
 
Back
Top Bottom