Ushauri wa kwa Serikali namna bora ya kuboresha elimu

Ushauri wa kwa Serikali namna bora ya kuboresha elimu

Joined
Jun 3, 2014
Posts
63
Reaction score
68
Kwanza nipende kuwapa pole na shughuli mbalimbali, na hongereni wananchi wote kwa mafanikio ya mwaka huu.

Najua Tunamuomba Mungu ili aendelee kutulinda na kututunza kila iitwapo leo, pia tunamuomba atufikishe salama mwaka unaokuja wa 2018.

Lakini ushauri wngu mfupi kwa serikali yetu kuhusu mambo mbalimbali.

1. ELIMU. Elimu yetu ya Tanzania ni nzuri sana, na inaendelea kua nzuri, lakini najiuliza sana kwa nn shule za serikali zimedorola mwaka huu? Je waalimu hakuna? Je mazingira ya kujifunzia hakuna?

Je vitendea kazi hakuna? Je waalimu wana uwezo mdogo wa kufundisha, je wanafunzi wenyewe ndo wagumu wa kuelewa?

Ni maswali tu najiuliza maana Elimu bure imewakomboa wa Serikalini cha kushangaza Shule za Binafsi zinafanya bizuri zaidi kuliko za serikalini. Pendekezo langu ni kua waalimu wasiachishwe kwenye shule moja zaidi ya miaka 10, kuna waalimu wapo vijijini huko, wengine mijin, ni vyema wakawa wanabadilishana vituo ili wabadilishe hata mazingira, pili mitaala ya kufundishia iwekwe wazi, mfano vitabu vingine vya zamani virudi vya shule ya msingi, masomo yasiongezwe zaidi ya hapo, ndani ya somo fulani waingize topic ya Rushwa athali zake, waalimu wapelekwe vijijini maana waalimu wengi wamejazwa mijini ila vijijini hakuna waalimu, idadi ya kudahili waalimu wasiona ajira ipungue, maana ajira imekua ni shida, hivo kama chuo kilikua kidahili wanafunzi 3000 basi kipunguze wafike hadi 1500 ili kuondokana na tatizo la ajira.
 
mie nadhani serikali ianzie na vijijini huko kuna mabalaa ya kila aina lolz
 
Du ushauri kiboko huu! Mbona unawandama tu walimu kana kwamba wao ndo tatizo tu, ukisema vyuo vipunguze udahili kwani lazima wote waajiriwe?? Hata kwani idadi ya walimu inajitoshereza?? Nani kasema siasa tu!
 
ushauri mzuri,na kwa sisi tulioishi wakati nchi ina adabu,kuliundwa tume ya MAKWETA(rip) mapendekezo ya ile tume yakifanyiwa kazi hata nusu yake kiwango chetu cha elimu kitakuwa bora kulingana na cha sasa,elewa Zimbabwe pamoja na mchoko waliokuwa nao elimu yao ni best ukilinganisha na nchi za SADCC,mfumo wao wa elimu hawakuuchezea kama tulivyofanya sisi.itafutwe ile ripoti ya tume ya Makweta na ifanyiwe kazi.
 
Back
Top Bottom