Ushauri wa kisheria

ilisha juniour

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
714
217
Naandika kwa masikitiko makubwa Sana, nlitokea kuwa na mahusiano na binti wa kiislam kwa muda wa miezi sita nikampenda Sana, mimi ni mkristo, yeye hakuwa na msimamo mkali sana kwenye dini kwaio alibatizwa na akabadiri dini na kuwa mkristo wakati huo yeye ni mtumishi na mpaka anafikia maamuzi ya kuniacha vyeti vyake vyote mpaka faili lake la utumishi vinasoma jina la kwanza la kiislamu, nimemuoa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana,mara kwa mara tumekuwa na mikwaruzano ya kawaida ambayo yapo katika mahusiano na toka nimemuoa mpaka sasa kila tukihitilafiana anataka tuachane swala hili limejirudia kwa sasa ni mara ya tatu Mimi sikatai nina mapungufu lakini nae pia ana ya kwake, nilipomuoa vyeti vya ndoa vina jina la kikristo pamoja na cheti cha ubatizo, kwakuwa kwa sasa amekataa kabisa kuendelea kuishi tena na mimi na pia amekataa vikao vya usuluhishi imefika mahali nimehisi nikiendelea kukaza uzi maisha yetu ya baadae hayatakuwa na furaha na mbaya zaidi ni yeye amenikataa sio Mimi, nataka nimruhusu aende Kwa masikitiko makubwa kwakuwa ndoa yetu ina mwezi mmoja you Msaada wa kisheria ninaoomba je itakuwa na athari gani kisheria kwangu Kama nitaendelea na maisha Mengine kwa maana siko tyari kuoa tena kulingana na miiko ya dini yangu lakini nahitaji kutengeneza mali za kutosha na maisha ya baadae(future)
 
Ndoa ina mwezi mmoja???????.. Ongeza juhudi kujaribu kuyamaliza katika ngazi za familia kwanza kabla ya ku-opt kwenda katika vyombo vya sheria .....
 
Ndoa ina mwezi mmoja???????.. Ongeza juhudi kujaribu kuyamaliza katika ngazi za familia kwanza kabla ya ku-opt kwenda katika vyombo vya sheria .....
Niliyemuoa kanikataa kabisa na hataki kikao chochote kile na mimi sijamkataa na wala haipo dhamira kwangu kwenda kwenye vyombo vya sheria nataka ushauri kwa maana ya maisha ya baadae swala la kisheria kwangu litakuwaje?
 
Kisheria mahakama haiwezi kuvunja ndoa yoyote ile ambayo haijafikisha miaka miwili, hakuna sheria itakayotumika kwa sasa ktk tatizo lako hili, kwa sasa tenganeni tu kila mtu aishi kivyake, ila nakusihi uanzie kwanza kwenye baraza la kata la usuluhishi wa ndoa ulipeleke hili swala.
 
asante sana swali lingine naomba nikuongezee, ndoa nilifungia mbezi halafu mimi nakaa kigamboni kata inaitwa tungi sasa Shauri hili naweza kulipeleka kwenye kata hii ninayoishi?
 
asante sana swali lingine naomba nikuongezee, ndoa nilifungia mbezi halafu mimi nakaa kigamboni kata inaitwa tungi sasa Shauri hili naweza kulipeleka kwenye kata hii ninayoishi?
Ndio, kwenye hio kata ambayo mna makazi ya kudumu au mmeishi wote pamoja hapo kwa wakati flani.
 
Back
Top Bottom