Ushauri wa kisheria kwa huyu rafiki yangu

Man Ngosha

JF-Expert Member
May 2, 2012
219
69
Habari ya kazi wana Jf, naombeni ushauri kuhusu suala ambalo linamkabili jamaa yangu, iko hivi; jamaa yangu ni mfanyakazi wa bank private, pale kazini kwao palitokea tatizo ambapo kuna mteja alikuja kulalamika kuwa account yake imetoa pesa kwa simbanking bila yeye kujua, walifuatilia ikabainika kuna namba imehusika kufungua account ya simbanking na ndio ilitumika kutoa pesa, na kuna namba zingine zilitumiwa hiyo pesa. Huyu jamaa yangu ni moja kati ya wanaosaini katika form za kufungua account. Issue ilikwenda polisi na hatimae mahakami wakati uchunguzi ukiendelea na kazini alikuwa amepewa administrative leave kupisha uchunguzi.

Sasa majuzi wamemwita ofisini wanampatia barua ya kurudi kazi,ambayo inasema investigation complete na anatakiwa arudi kazini.
Ushauri tunaoomba ni juu ya yeye kukubali kurudi kazini wakati kesi ikiendelea na pia hawajasema matokeo ya uchunguzi wao?
Pia, anahofia isiye kuwa wanamrudisha kazini ili wasimpe mkataba mpya maana mkataba wa sasa unakoma mwezi ujao.
Naombeni ushauri wa nini cha kufanya katika hili ili kulinda maslahi na haki yake,
Asanteni sana
 
Barua yake hiyo ni uthibitisho wa yeye kutokuwa na hatia, maana kama angekuwa na mshtakiwa asingerudishwa.
 
Arudi kazini hata wakiterminate contract kunasehemu ya kuwabana.. tu
 
Barua yake hiyo ni uthibitisho wa yeye kutokuwa na hatia, maana kama angekuwa na mshtakiwa asingerudishwa.
Ni kweli lakini anamashaka ya kutopewa mkataba mpya kwa kigezo hizo, maana tulidhan inapaswa kwanza kesi imalizike ndo wafanye maamuzi ya ndani, maana wao benki ndo walianzisha kesi
 
Back
Top Bottom