Mkuu kalamu 1 unaju maana ya kura za maruhani?.Waulize WazanzibariUnadhani nitakubishia kwa hili? Hapana.
Hili ndilo ninaloomba wapinzani wawaelimishe wananchi.
Watu pekee wanaoweza kukataa mipango hiyo ya 'uteuzi' wa mtu badala ya kura zao ni wananchi pekee. Wengi wa hawa wakikataa, hata huyo mwenye 'mabunduki' yake hatathubutu kuchezea kura zao.
Tatizo kubwa ni 'Wapinzani' na watu wengine wasiokubali mpango huo wa mtu mmoja kuharibu kura za watu wengi, watawezaje kuwafikishia elimu hiyo wananchi?
Sasa hivi mtu huyo anafanya hivyo kwa kujua watu (wapiga kura) hawazijali kura zao.
Wanakwenda kupiga kura, lakini hawataki kujua kama kura zao kweli ndio zinazowapatia viongozi wanaowataka wao.
Hapo ndipo penye tatizo. Na ndipo mchango wa kila mtu, hata hapa JF unapotakiwa. Jinsi ya kuliondoa tatizo hili.