Ushauri wa Kipuuzi kwenu Wapinzani: Mpeni Kamba Magufuli ajinyonge mwenyewe

Wewe hutaki kuelewa ninachoandika au unapindisha tu maksudi na kujifanya huelewi.

Ni wapi nilipoandika kuwa 'ninaamini kuwa kupiga kura na kuishia hapo' ndio itakuwa njia ya kuwaondoa CCM?
Huwezi kuwa mtu 'unayejitambua' halafu ukaacha kupigania haki yako. Huenda huelewi maana ya "kujitambua."
 

Unapigania haki yako kwa box la kura njia ambayo imeshaonyesha wazi kufeli? Njia ya kura haitowatoa ccm zaidi ya machafuko. Tawala nyingi za kiafrika huwa hazijeshimu demokrasia ya kura, bali machafuko pekee ndio huleta mabadiliko na haki. Kama una ndugu na jamaa wenye muda wa kupoteza kapangeni mstari kwenye box la kura muwatoe ccm.
 
Wewe "usiekuwa na muda wakupoteza" usitupotezee muda na kutuwekea visingizio vya kuwalinda hao usiotaka tuwatoe madarakani. Ni lazima tuwe na mahali pa kuanzia, na kwenda kupiga kura ni sehemu mhimu ya kianzio cha mengine inapolazimu.
Watu kama nyinyi wanawapenda sana.
 

Sio mimi, sema sisi maana tuko wengi, ndio maana nakuambia subiri siku ya kura uone idadi itakavyokuwa ndogo. Ww utapaswa kuniprove wrong kwa idadi kubwa ya wapiga Kura. Wajinga wa kwenda kusimamishwa kwenye mstari kwa kura za kiini macho hawapo tena zama hizi.
 
Wajinga wa kwenda kusimamishwa kwenye mstari kwa kura za kiini macho hawapo tena zama hizi.
"Wajinga" ni wasiotambua wajibu wao katika taifa lao na ndio inaowahitaji sana CCM. Watu ambao hawjui kwamba kura zao zina thamani kubwa na zinatakiwa ziwe ndizo mwamuzi wa mtu anayetakiwa kuwaongoza.

Siku zote CCM inawataka sana watu hao. Na ndio maana wanasema 'CCM itatawala milele', kwa sababu inajua wajinga hao wapo wengi nchi hii.
 

Hao wapinzani tuliokuwa tunawapambania si ndio hao hao walituletea Lowassa toka ccm na sasa karudi tena ccm? Hao wapinzani si ndio hao tulipambana kupiga kura na kuzilinda kisha wakaenda kuunga mkono juhudi? Sasa kama tunatake risk na bado wapinzani wanatuletea wanaccm na wengine wanarudi ccm kuunga mkono juhudi, tupige kura ili iweje kwa mfano.
 

Sasa unaingiza mjadala mwingine ambao pengine ninaweza kukubaliana na wewe.

Ndiyo maana nimeandika mara kadhaa katika majibishano nawe humu kuhusu umhimu wa uongozi wa kuwaongoza hawa wananchi ambao wako tayari kupiga kura kwa wingi na kuhakikisha kura hizo zinahesabika na hazichezewi na mtu yeyote awaye.

CCM wamekwishafanikiwa kuwatia woga upinzani. Na wananchi hawaoni kiongozi wanayeweza kumwamini kuwaongoza ili wajikomboe kutokana na kunyimwa haki za kupiga kura zao huru na kuzihesabu kura zote bila mizengwe.
 
Huu ni ushauri konki kabisa wala si wakipuuzi!

Wapinzani ambao sio mapandikizi wasipoteze hela za kugombea na kufanya kampeni. Wakishachukua kiinua mgongo watafute shughuli nyingine za kufanya, wakae pembeni wamuachie chama chake na Bunge lake. Halafu tuone atakapotufikisha kimaendeleo
 
Walikuwa wananikashifu kwa huu ushauri toka mwanzo.leo wamefanya yale yale nliyoyasema.

 
Walikuwa wananikashifu kwa huu ushauri toka mwanzo.leo wamefanya yale yale nliyoyasema.
Mkuu labda wewe ndiye mkono wa kushoto wa Mh.Mbowe na kamati yake.


Sema ulikuja kupima upepo baadaye leo mmelizia kiulaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…