Mnabagua Watanzania kisiasa mnawanyima umeme wapinzani mnadhani mtakaa madarakani milele?

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Hili shirika linaendeshwa kisiasa hali inayopelekea tulione genge la CCM.
Tangu 2004 mpaka sasa ni miaka 19 inakaribia 20 bado kuna vijiji havina umeme kabisa sasa mtaanzaje vitongoji wakati vijiji vingine havijawahi kufikiwa na umeme? Mmebuni teknolojia gani ya kufikisha umeme kwenye Vitongoji uku kwenye Vijiji hakuna umeme?
Natoa KIJIJI chenye Vitongoji 10 kama nilivyovipokea kutoka kwa watu walionyimwa umeme mbali ya kuwa na uwezo wao wa kulipia ghalama yoyote ila kwakuwakomoa tu TANESCO kwa kushirikiana na wenyeviti wa Vijiji na Kata waliwanyima umeme kisa WAPINZANI wa CCCM.

VITONGOJI vya Kijiji KAISHO kama ifuatavyo:
*Charuhuza
*Chabojo A
*Chabojo B
*Kitembe (nusu)
*Rwagabo
*Omukigando
*Kigarama
*Nyaruhanga
*Nyakanyasi A
*Nyakanyasi B
Chanyamwilika
Kwa kifupi Kijiji kizima hakikuwahi kupata umeme tangu kuumbwa kwa dunia ie REA walipoingia Kata za Kaisho na Isingiro 2004.

Mnaweza kuchukulia kawaida ila ninaamini vipo vijiji vingi vimefanyiwa mtima nyongo na TANESCO wakajikwaa kwenye ujinga wa watendaji awa wasio na akili.

Jambo la ajabu ata Naibu Waziri Nishati kajikuta kadumbukia umo licha ya kupewa malalamiko aya yeye binafsi, Mbaya zaidi ata Waziri mwenyewe aliahidi tangia mwaka jana kushughlikia tatizo ili lililoasisiwa na CCM lakini mpaka leo hajatekeleza.
Ifike maala ninyi CCM mnaojimilkisha nchi hii ivi mkitolewa madarakani mtakuwa wageni wa nani? Hamjui muda wenu wa kutawala umeisha? Kwanini hamsomi alama za nyakati?
Maeneo niliyotaja apo juu ni Watanzania wanastahili kuheshimiwa acheni ubaguzi mnapanda mbegu mbovu ila ikikuwa mtakimbia mavuno. Ebu pitia Katiba ya nchi yetu uenda hamkuwahi kusoma eneo hili Katiba inazuia UBAGUZI


bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya
watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa
mujibu wa sheria.

Inaendelea kusema

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
17
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria
yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya
Mamlaka ya Nchi.

Sasa ubaguzi huu unaoendeshwa na awa wenyeviti wa vijiji na watendaji kata mpaka madiwani na wabunge wanajua wanavyovunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Je Tanesco mnatambua jambo hilo?

Ushauri kwa ufupi TANESCO acheni kutumika kisiasa hizi ni kodi za Watanzania wote ni vyema mkasimamia sheria na taratibu za nchi sio wanasiasa waliopo leo kesho hawapo.
Tanzania_Electric_Supply_Company(TANESCO)_logo%20(2).jpg
 
Back
Top Bottom