Ushauri wa Harusi ya gharama ndogo

Mkuu, andaa unataka kufanya sherehe ya watu wangapi, na una sh ngapi?
 
Mkuu, andaa unataka kufanya sherehe ya watu wangapi, na una sh ngapi?
Huu uzi ni mwaka 2013 si ajabu hata wameshazaa watoto watatu. Angalia tarehe ya uzi umepostiwa lini.
 
watu wangapi?
Watu 20 , na ningependa nifanyie mahali popote kuanzia tabata Segerea kuja maeneo ya gongo la mboto mpaka chanika kama kuna garden au hotel nayoweza kuitumia kwa shughuli hiyo.
 
Watu 20 , na ningependa nifanyie mahali popote kuanzia tabata Segerea kuja maeneo ya gongo la mboto mpaka chanika kama kuna garden au hotel nayoweza kuitumia kwa shughuli hiyo.
Inatosha mbona, niliwah kufanya kama hiyo, basi ukumbi hautahitaji mapambo. Na hauna ndugu yako mwenye uwanja au garden nzuri ukafanyie kwake?, then chakula utafute mtu wa kawaida uumpe hela kama laki tatu anunue vitu akupigie menu ya maana.
 
Inatosha mbona, niliwah kufanya kama hiyo, basi ukumbi hautahitaji mapambo. Na hauna ndugu yako mwenye uwanja au garden nzuri ukafanyie kwake?, then chakula utafute mtu wa kawaida uumpe hela kama laki tatu anunue vitu akupigie menu ya maana.
Nafikiri nikipata Garden , au Resort yenye garden mimi nikanunua vyakula toka kwao ndiyo ingenipendeza zaidi , maana natumia mfuko wangu mwenyewe.
Yaani , zaidi nahitaji kujua wapi naweza kupata huduma ya vyakula vizuri na vinywaji wageni wangu wakafurahi na sisi siku hiyo, iwe hotel au hotel yenye garden ambayo gharama itakuwa kwenye vyakula na vinywaji tu.
 
SMAAAARTTTT
 
Andaa kama mil 3.5
Na hakikikisha watu hawazidi kwel hamsini utafanikiwa

Binafsi tulifanya watu 100(nusu walichanga)
Tukapiga sherehe kali sana temboni garden
Bajet kama 4mil ilifika
-picha video 350k
-garden na viti kupambiwa na meza 400k
-stage ya maharusi 150k
-chakula nakumbuka ilikua 750k(meza moja tu ilikosa msos watu kama 10 ndo walikosa unfortunate)
-mc na mziki 500k
Iliyobaki tulielekeza kwenye vinywaji
(Kumbuka hii ni 4yrs back alafu wengi hapo walikuwa jamaa zangu so walinifanyia fair sana
Jitahid upate watu wako ambao wanautundu na field za mapambo mc nk)
 
Truelove, nikutie moyo juu ya mpango wenu na mumeo mtarajiwa. Ni kwamba inawezekana sana tena vizuri mkafanya sherehe ndogo kwa macho lakini kubwa ndani ya mioyo yenu wewe na mumeo na wageni wenu wachache kama 40 au 50 tu hapo unawaalika wageni wa upande wa mume 25 na upande wa mke 20 na watano ni mpiga picha na nk.
Na pia kupunguza gharama msitake kufanyia kwenye ukumbi , bali mfanyie hiyo sherehe nyumbani kama ni mzazi wa kiume basi ni vizuri au mnaweza kufanyia hata kwa rafiki yako mkubwa kama ananyumba yenye eneo kubwa au ndugu wa karibu, alafu mkatafuta mpambaji mzuri akapapamba na kulipendezesha hilo eneo kwa 500k.
Chakula mkamtafuta mpishi mzuri kwa gharama ya kati.
Viti 50 vya kukodi gharama ni ndogo.
Mimi nilifanya ya 3.5 ya wageni 45 tu na ilikuwa ni nzuri sana mpaka kesho nikiangalia picha siamini kama nilifanikiwa kufanya kwa staili ile.
Nakutakia ndoa njema.
 
Huo ndo ujinga wa vijana wengi ulipo, maisha ni yako eti sherehe ni yandugu na marafiki, shubamitiiiii!!!! kwanini bwana harusi/bibi harusi uhangaike na michango? kiufupi swala la kuchangishana limeshapita na wakati, andaa sherehe kadri ya uwezo wako lakini fikiria na kesho yako pia. Unakuta umeajiliwa unalipwa mshahara 800k ila harusi unafanya ya zaidi ya Milioni 20 na hapo umepanga chumba kimoja, si ujinga huo.
 
Tutor B unatumia kinywaji gani ukute unaendlea nakuja kulipa,safi sana aisee
 
Wahenga wahuu uzi jamani mjage vijana tunataka kujua gharama nizilezile au zimebadilika
 
Mie kipindi naoa nilifunga ndoa ya kiserikali hivyo sina ujuzi sana na mambo ya harusi.
Nina mdogo wangu anaishi mjini Dodoma ila ndoa atafungia kijijini.
Kijijini kwetu ni nje kidogo ya mji wa Misungwi.

Kwa watalaamu au wazoefu wa masuala ya harusi na gharama zake. Makadirio ya gharama za kufungia ndoa huko kwetu zinaweza kuwa kiasi gani?.
Zikiwemo gharama za kumleta mpambaji toka mjini na mapambo yake kuja kupamba ukumbi kijijini, kukodi viti toka mjini, mziki, keki, usafiri na mengineyo ambayo yanahitajika ili kukamilisha zoezi hili?
Idadi ya watu makadirio 150

Note: Mchele upo wa bure na nyama pia ni ya bure.
Wapishi ni watu wa kijijini hapo wakiongozwa na expert wawili tu walio na utaalamu katika mapishi, hawa expert wa upishi nao watakuwa wa bure pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…