Ushauri wa bwerere kwa Anko Mrisho Ngassa

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
NIMEONA andiko la Mrisho Khalfan Ngassa mitandaoni. Ni andiko flan hivi ambalo lina vimelea vya kujitilisha huruma. Alichofanya huo ndo uzalendo mkubwa kwa timu yake. Wachezaji wote wangekuwa hivi naamini ingekuwa safi sana. Maana vijana wametawanyika kwama Wayahudi wa kale.

Msuva yuko Morocco huko. Hivi anadhani zile chips za washikaji mitaani atakuwa anakula nani?
Hana uzalendo wowote kaamua kwenda kuishi na mabeberu wa Kiarabu. Ndivyo ilivyo na kwa Mbwana Samtta na wengine. Kawaacha masela wa Mbagala huko kaenda kukaa na wazungu.
Lakini Mwamba wa Kanda ya Ziwa Mrisho Ngassa. Yeye anazunguka tu kwenye vitimu vya hapa hapa Bongo. Hana makuu mshikaji. Wala hataki kuwaacha ndugu jamaa na marafiki. Anachopata anapata kugawana na ndugu jamaa na marafiki wa hapa hapa Bongo. Huu ndo uzalendo.

Himid Mao kama ilivyo kwa Abdi Banda na wengineo. Hawana utu kwa Watanzania. Wanaacha kuwaburudisha wakazi wa Turiani na Chamazi. Yeye kaenda kwa wajukuu wa Farao. Anaona sifa sana na kudhani kubaki Bongo watu wangefaidi sana. Ngassa hana makuu.
Yeye katoka Kagera, Yanga, Azam, Simba, Mbeya City, Ndanda kisha karudi zake Yanga. Huyu jamaa ana upendo na nchi yake. Ana upendo na timu za Bongo hasa Yanga na mashabiki wake. Muungwana ni vitendo na Ngassa anatenda vitendo vya kiungwana hasa. Kwanza alikubali kufanya kazi kwa mkopo. Yaani alisajiliwa kama laini za simu kwa alama tu za vidole. Akaambiwa fanya kaza malipo ya usajili yanakuja. Hii ni akili ya kizalendo kwa timu yenye hali duni. Inadaiwa nchi itakuwa klabu ya mpira bana. Na sasa Ngassa anadai pesa yake kwa mafumbo mafumbo.

Hataki kuwakera viongozi na mashabiki. Huu ndo uzalendo hakuna sababu ya kwenda kucheza kwa mabeberu. Mpira ni mchezo wa watu masikini, kwanini utake mamilioni ya pesa? Manaake ni kwamba mpira siyo kazi. Ndo maana wanauchezea watu 22 katika dakika 90. Siyo kazi ile ni burudani.
Ngassa huu ushauri kwako wa bure bin bila senti.
Kwamba acha kuwadai Yanga hizo pesa ili uendelee kuwa mtu wa mfano kwa uzalendo. Usiwaige kina Msuva na Samatta. Waambue ndo maana ukikataa kwenda nje wakati ule ili ubaki Yanga. Siyi West Ham wala El-Merekh. Wote hao uliwakataa.
Ukabaki Bongo ili kuburudisha watu bila malipo ya kueleweka.

Ubarikiwe sana kwa moyo huo na zaidi endelea kucheza bure. Maana Yanga ndo wataleta ada za shule kwa watoto wako. Kama wanavyopeleka kwa Lunyamila, Mmachinga, Sekilojo Chambua na Fred Felix Katariya Baba Isaya Minziro Majeshi.

Credit: Mwanaspoti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkia wa mbuzi wewe

Huo alioufanya Ngasa ni ujinga mkubwa na umaskini wa kujitakia. Sio kitu cha kujivunia hata kidogo.
 
Nilisikia huyu mjomba alioa wake wawili? Sasa anatia huruma vipi? Mi namuonea jealous mwenzetu anafaidi,
 
Haahaa! acha kumzidishia hasira mwenzake, hukumbuki alivyopata chance ya majaribio huko kwa mabeberu, alikimbia tu uwanjani hata hakugusa mpira, karudi kaongeza mke ndio nguvu zikapotea akaenda kuamkia ndanda. Kma anadai alipwe tu maana ni deni.
 
Hahah Uncle mtu safiii sanaa ujue ni kama Ali kiba tu hawana makuu.
 
Back
Top Bottom