Ushauri wa bure kwa Wizara ya Afya na NHIF

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
814
1,545
Hii huduma ya toto afya NHIF wamefeli kwenye Promotion sasa wanaamua kuwafanyia ukatili watoto mfano leo hii makampuni makubwa tunaona Kila siku matangazo yao wakijitangaza tuchukulie Mfano Kama makampuni ya Simu ukiwasha radio/Tv haipiti dk 30 hujaona tangazo la Eidha voda tigo au Airtel,leo hii nani asie ijua kampuni ya Coca ila kila siku wanatangaza ukija taasisi za Fedha kama Mabanki ndo hadi yanaamua kwa sasa kuingia kwenye soka ili kuendelea kujipatia wateja.

unaweza kaa wiki nzima usisikie Tangazo la Bima unaweza katiza mji mkubwa usikutane na bango lolote la BIMA.....mfano leo mtu wa Kijijini ndani akihitaji Laini ya Simu msajili anakuja hadi mlangoni ila Bima lazima atasafiri si ajabu km zaidi ya 100 na anaweza fika akashinzdwa kamilisha mchakato siku hiyo hiyo ikambidi alale tena bado siku bima ikitoka inabidi asafiri tenaa..na hii elimu ya Bima Watanzania wengi mno hawana.

Tatizo ni kuwa NHIF wanachukulia Bima kama msaada na Si Biashara wangeichukulia Kibiashara ingeenda...mimi nashauri kabla MAMA UMMY na anaejua Uchungu wa Mtoto hajafuta zilizopo na kuleta mfumo mpya Angeweka Benchi watu wa masoko walete ambao wataweza piga Promo na watakuja na mbinu mpya za usajili kama ilivo makampuni ya Simu. Unasajiliwa popote sio hadi ofisini maana hata hii wanasema ya mashuleni mimi nina watoto wawili na wana Toto afya card zinaisha Mwezi wa 10 ambapo ndo nilipaswa kulipa tena ila shule wanazo soma nauliza Mwalimu mkuu anasema hajapokea mwongozo wowote na shule baadhi nimeuliza jibu ni hilo hilo hakuna mwongozo wowote kwahiyo bado tu watafeli tena.

nashauri wale watoto wenye BIMA waendelee kuzitumia BIMA zao alafu wizara ya Afya na NHIF waje na promo wapite kila kijiji kusajili watoto watumie watendaji wa vijiji,Mitaa,walimu, vituo vya afya ambapo kuna kliniki yani mama ikibidi pale mama tu anapojifungua anapewa na Fomu ya BIMA ajaze pia wawe na Freelencers kama Mitandao ya Simu,,mbona kwenye kusambaza condom za bure inawezakana kufika pote au kwennye chanjo kama za Surua inawezekana Nchi nzima why NHIF washindwe??

Zile TAASISI zinazotetea Haki Za Watoto Hazioni Katika hili kuna ukiukwaji,na Unyanyasaji wa watoto??? Viongozi wa Dini hawaoni huku ni kunyanyapaa watoto ambao hata Yesu alise WAACHENO WATOTO WADOGO WAJE KWANGU MAANA UFALME WA MBINGU NI WAO.

Nawasilisha
 
Hili suala linaumiza sana, hata wale ambao Tayari Wana Toto Afya Card, hawawezi kulipia Tena huduma.
 
Back
Top Bottom