Ushauri wa bure kwa Waziri Kairuki

che wa Tz

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
277
71
Siku kadhaa zilizopita, nilijaribu kutoa ushauri wa bure hapa hapa kwa waziri wa nchi, ofisi ya raisi, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora juu ya hili zoezi la uhakiki linaloendelea, na ninamkumbusha tena kama uhakiki huu usipochukuliwa kwa umakini basi madhara kama ya haya ya kifo cha yule muuguzi kule Bahi yanaweza kuwa mengi, sitaki kulihusisha moja kwa moja tukio hilo na hili zoezi lakini kwa ushahidi wa kimazingira inaonekana sababu ni hilo.

Kama itafika mahali makosa ya kiuandishi haswa ya majina katika nyaraka mbalimbali ambapo ni makosa ya kikawaida sana yatatumika kama ni sababu ya kumuondoa mtumishi katika utumishi wa umma, basi ama kwa hakika hakuna mahali kutaonekana kwa hovyo kabisa kama Tanzania na ule utabiri wa kuuvuruga utumishi wa umma basi utakuwa umetimia.

Mheshimiwa waziri, ukiachia na hilo, hebu tujifunze napo kusoma alama za nyakati, naamini hakuna mwajiri yyte duniani ambae ameajiri na hataki kuona ufanisi ukitokea katika ile sekta aliyoajiri, lakini kwa hali hii ya hofu waliyonayo watumishi wa umma ambapo wengi wamekuwa kama hawaijui kesho yake, sidhani kama kutakuwa na ufanisi katika utendaji wao na ubunifu, most of them wamekata tamaa na hofu zimewajaa. Tuwe makini katika haya mazoezi.

Shahidi ni huu wingi wa post humu kwenye haya majukwaa y kijamii na maoni ya wafanyakazi wenyewe.

Muuguzi afariki baada ya kuhakiki taarifa za utumishi wa umma
 
Wanajipa moyo kwamba kuna watu maelfu na malaki hawana ajira...kwahiyo wakifa..wakifukuzwa...kuna wataoreplace nafasi zao...which is NON SENSE.....wanasahau kwamba wenye uzoefu ndio watakaowapa training wenzao wakiw kazini...
Tena katika sekta ya afya hutakiwi kumdharau uliyemkuta kwasababu unatoka na kielimu chako cha darasan..ukipewa mgonjwa unatoa macho...
 
Siku kadhaa zilizopita, nilijaribu kutoa ushauri wa bure hapa hapa kwa waziri wa nchi, ofisi ya raisi, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora juu ya hili zoezi la uhakiki linaloendelea, na ninamkumbusha tena kama uhakiki huu usipochukuliwa kwa umakini basi madhara kama ya haya ya kifo cha yule muuguzi kule Bahi yanaweza kuwa mengi, sitaki kulihusisha moja kwa moja tukio hilo na hili zoezi lakini kwa ushahidi wa kimazingira inaonekana sababu ni hilo.

Kama itafika mahali makosa ya kiuandishi haswa ya majina katika nyaraka mbalimbali ambapo ni makosa ya kikawaida sana yatatumika kama ni sababu ya kumuondoa mtumishi katika utumishi wa umma, basi ama kwa hakika hakuna mahali kutaonekana kwa hovyo kabisa kama Tanzania na ule utabiri wa kuuvuruga utumishi wa umma basi utakuwa umetimia.

Mheshimiwa waziri, ukiachia na hilo, hebu tujifunze napo kusoma alama za nyakati, naamini hakuna mwajiri yyte duniani ambae ameajiri na hataki kuona ufanisi ukitokea katika ile sekta aliyoajiri, lakini kwa hali hii ya hofu waliyonayo watumishi wa umma ambapo wengi wamekuwa kama hawaijui kesho yake, sidhani kama kutakuwa na ufanisi katika utendaji wao na ubunifu, most of them wamekata tamaa na hofu zimewajaa. Tuwe makini katika haya mazoezi.

Shahidi ni huu wingi wa post humu kwenye haya majukwaa y kijamii na maoni ya wafanyakazi wenyewe.

Muuguzi afariki baada ya kuhakiki taarifa za utumishi wa umma
Mwezi July 2017 mishahara inatoka kwa mafungu. Hadi mda huu wengine hawajapata na hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa na wahusika tatizo ni nini.
 
Back
Top Bottom