Ushauri wa Bure kwa Wazazi wenye Wanafunzi Primary School

iQ255

Member
May 28, 2017
7
9
Ili kuongeza Ufaulu wa Mwanao kwenye Somo la Hisabati (Mathematics) kwa aliyeko shule za Msingi fanya mambo yafuatayo:

1. Hakikisha unamsimamia vizuri mtoto wako afahamu kwa kuzishika kichwani Table zote kuanzia Table namba 2-12. Kwa mwanafunzi wa darasa la 3 hadi 4 table namba 2-6, kwa mwanafunzi wa darasa la 5-7 Table namba 2-12.

2. Hakikisha mwanao anafanya zoezi la Hisabati (Mathematics) kila siku kabla ya Kula Chakula cha jioni/usiku.

3. Hakikisha mwanao anafanya mazoezi ya somo aliyofundishwa siku hiyo hiyo bila kulaza Home work.

4. Hakikisha unafuatilia maendeleo ya Mwanao kwa Mwalimu wa Hisabati (Mathematics) Mara kwa mara, ili kujua mapungufu ya mwanao.

5. Hakikisha mwanao anatumia vitabu vilivyosahihi katika kujifunza.

Kwa maelezo ya vitabu vizuri na vilivyosahihi kwa Wanafunzi njoo inbox.
 
Ungetoa kila kitu hapa pm yanini kama unataka utuuzie vitabu si ungesema hapahapa tu mkuu hata nikushukuru kwa ushauri.kuhusu tebo nashauri mtoto afahamu tebo yote darasa la nne
 
Hiyo ya kwanza sijakuelewa vizuri
Mtoto kabla hajavuka darasa la pili inabidi ajue table yote ya 1 mpaka 12 kwa sababu darasa la tatu ataanza hesabu za kugawanya kama hajui table ndio mwanzo wa kuichukia hesabu
 
Back
Top Bottom