Ushauri wa bure kwa tcra na makampuni ya simu za mikononi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa tcra na makampuni ya simu za mikononi

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by JF Marketer, Mar 13, 2012.

 1. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wimbi la wizi wa pesa kupita simu za mikononi linavuma kwa kasi. Mbinu zinabadilika kila uchao. La kustahajabisha ni kuwa wezi wanakwenda level nyingine kabla ya hata makampuni ya simu wala TCRA kudhibiti hatua ya nyuma.

  Nimesikitishwa sana na jinsi kampuni kama tiGO lilivyoshindwa kutoa ushirikiano kwa rafiki yangu Mashauri. Namba ya simu ya Bw. Mashauri ilikuwa swapped, akatoa taarifa tiGO kuwaomba waifunge. tiGO hawakufanya kama mteja alivyowaomba jambo ambalo limeacha mwanya na kuwawezesha wahalifu kusafisha salio lake pamoja na kuwaibia ndugu, jamaa na marafiki kwa kupitia line ya simu. Najua wahanga ni wengi. Na wengine maafa yamewapata kupitia line za simu ikihusisha na muhamala.

  Kwa kuwa haya makampuni hayaonyeshi nia ya dhati kutuhakikishia usalama wa data na pesa zetu. Na kwa kuwa TCRA wanayasikia haya na kubaki kimya, mimi kama mmoja wa wateja wao nashauri wafanye lifuatalo:

  • Watupe namba maalumu ya kufunga (block) line zetu wenyewe tunapopatwa na mashahiba kama haya.

  Serialization inaweza kuwa kama ifuatavyo:

  *NAMBA MAALUMU YA KUFUNGA LINE*NAMBA INAYOSTAHILI KUFUNGWA*NENO LA SIRI#KUTHIBITISHA (Mfano: 211*0655XXXXXX*PASSWORD#)

  TCRA wa-assign 211 kuwa permanent universal code for blocking hijacked SIM cards
   
 2. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dah! Ndugu yangu kwanza mpe pole sana rafiki yako kwa maswahibu yaliyo mpata..


  Tanzania ni nchi inayosemekana inaongozwa kwa mujibu wa sheria!


  Umetumia nguvu nyingi sana kujaribu kuwashauri mamlaka ya mawasiliano TCRA jinsi ya kujaribu kutatua kero zinazotukabili watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini


  Ukweli wanajua matatizo haya ya wizi na mbinu zote za uhalifu kwa kwenye mitandao na baadhi ya wahalifu ni wafanyakazi wa kampuni usika.


  Na makampuni yenyewe ya mawasiliano ndio wanaongoza kwa kuibia wateja wake na mara nyingi tume report kwa na hakuna hatua yoyote wanayochukua juu ya makampuni haya ya mawasiliano na ndio maana kila kukicha wanazidi kutuibia maana hakuna wakuwakaripia

  Hapo ndipo utajua sheria za nchi hii zinafanya kazi kwa baadhi ya watu....Tatizo kubwa ni kwamba mhe wetu wana_share zao kwenye haya makampuni ya mawsiliano ndio maana hii sekta ambayo ni muhimu sana kwa kushangia pato la taifa
  Nchi imekuwa hainufaiki na sekta hii ambayo imekuwa inakuwa kwa kiwango kikubwa kuliko sekta yoyote nchi kutokana na viongozi wetu kuwa na hisa zao hivyo hii sekta imekuwa ikitumiwa kumnyonya mkulima wa nchi ambaye kipato chake hakizidi dola moja kwa siku na wanayonufaika ni watu wa chache tu...


  Unaweza kuwasiliana na jamaa wa TCRA kwa E-mail:malalamiko@tcra.co.tz
   
 3. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uncle Rukus,

  Asante kwa mchango wako.
  Umesema kweli; Watumiaji wa Simu za Mikononi Tunaibiwa sana na tumeibiwa kwa muda mrefu. Mfano mdogo tu, jiulize lini umetangaziwa rasmi kuwa bei ya vocha imepanda? Kinachofanyika ni kupunguza muda wa maongezi katika vifurushi bila kukutaarifu wewe mtumiaji.

  Nimefahamishwa kuwa, hivi karibuni Voda wamemlipa Mhindi mmoja zaidi ya TZS 100M kwa kosa la kuwaibia wateja kupitia muda wa maongezi. Mhindi huyu alikusanya ushahidi wa ankara zake kuonyesha jinsi wanavyoiba kupitia muda wa maongezi, akamtafuta Mwanasheria na pamoja wakawaarifu voda kuhusu kusudiao lao la kufungua kesi. Voda wakamwita kwa mazungumzo na baada ya kujiridhisha kuwa kweli kuna watu wamefanya kazi kuweka wazi wizi wao, wakamwomba "wayamalize". Mhindi akalmba TZS 100M, akiuaga umaskini! Tunao Wanasheria wanaganga njaa, hizi ndizo kesi za kutokea.
   
Loading...