Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nadhani kwenye suala la kuvutia wawekezaji tumelala sana. Tunaimba kuvutia wawekezaji lakini ukiuliza tunafanya nini kuwavutia hupati majibu yanayoeleweka. Sana sana tunajikuta tukiwazuia na kuwafukuza kwa kuanzisha sera zinazowakimbiza hata wale ambao tayari wapo nchini, tukisingizia uzalendo na kulinda maliasili.
Hata kutoa work permit kwa wawekezaji wanaostahili ni shida sana hapa Tanzania! Kuna wawekezaji ambao wamekaa zaidi ya miaka kumi nchini na wanaajili Watanzania, na bado wananyimwa permanent residence, zaidi ya kusumbuliwa sana wanapotaka ku-renew vibali vyao vya kuishi nchini.
Sasa ushauri wangu kwa Magufuli ni kwamba achana na kuishi zama za miaka ya 47 katika enzi hizi za globalization. Usiifanye Tanzania kuwa kisiwa kwa kisingizio cha uzalendo na kulinda maliasili. Kuwa mkali kwa wazamiaji wasioleta faida, lakini pale ambapo tuna wawekezaji genuine wafungulie milango na madirisha ya kuwekeza nchini. Acha kufanya "impulsive decisions" kwenye haya mambo. Tafakari faida na hasara kabla ya kufanya uamuzi.
Kwa Prof Kabudi, ambaye ni guru wa sheria za kimataifa, ushauri wangu ni kwamba ongeza wigo wa nchi ambazo wana potential kubwa ya kuwekeza kwa kuanzisha nao mikataba (bilateral agreements) ya kutokuwa na visa kwa siku 30, 60 au 90. Hiyo itafungua milango si tu ya kuleta watalii kwa wingi, bali pia kurahisisha wawekezaji kutembelea nchi yetu kuangalia fursa za kuwekeza bila kuwa na usumbufu. Usidanganyike na vijisenti tunavyopata vya kuombea visa ya Tanzania, faida ya kutokuwa na visa na hizi nchi itakuwa kubwa kuliko hizo visa fees wanazolipa.