Masuala ya uchafu wa ndoa muulize Kikwete kama yuko tayari kujadiliwa kwa hilo. Hapa unaandikia watu wenye kujua mengi, sioni hekima ya kujadili haya, kama ungekuwa mtu wake wa karibu usingejaribu hili..
Kuhusu kuchomekewa, naona kuna 'research' unaifanya hapa hivyo sikupi faida.
Kuhusu kuheshimu maamuzi ya 1995. Hayo ni mambo ya CCM kwamba kuna mtu au kikundi cha watu wachache kinaamua nani awe kiongozi. Maana ukweli ni kuwa Kikwete aliwabwaga Msuya na Mkapa mwaka ule. Uamuzi wa CCM kuongozwa na matakwa ya dikteta fulani au kikundi fulani cha kisultani isiwe ndio msaafu kwamba hata Dr. Slaa afuate nyayo za nyoka.
Ukiondoa Mandela ambaye anaheshimu watanzania wote hata kama ingekuwa Zuzu kawa Rais wa Tanzania, na sababu ya Mandela kufanya hivyo unaijua fika.
Hao wengine unajua fika wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi. Pia sioni kama ni vema kuorodhesha hapa makampuni makubwa ya uchimbaji madini, utafiti madini, ushauri na maeneo mengine ambapo nchi zao zinafaidika kwa kiasi kikubwa.
Kama kweli Kikwete amefanya kazi nzuri miaka mitano iliyopita, kwa nini pamoja na kuiba kura ameshuka kutoka zaidi ya 80% hadi 61%???
Utetezi wako unafaa ndani ya CCM peke yake. Upeleke huko wakupigie makofi, lakini fanya haraka kabla ya wiki ijayo maana utakosa washabiki. Wengi wanakenua na kupiga makofi saa hizi kwa ajili ya uwaziri, ubunge viti maalum, ukuu wa wilaya na mengineyo mengi. Maana mnadai CCM kazi nyingi....au kupeana kwingi???? kwa manufaa ya nani?????
Makame hujafanya utafiti wa kutosha wazungu si watu wazuri wote wanaosema wanamwaminia kikwete ni wazungu na wote waliomheshimu kwa kuwa mwana democrasia ni madikteta ndugu yangu fanya utafiti wako vizuri- anayekutumia na kunufaika na ulimbukeni wako lazima awe ananufaika na hali uliyo nayo na ni lazima akuheshimu na kukutetea ili azidi kunufaika na ulimbukeni wako? Hata yeye mwenyewe anajua wanamtumia lakini ameshindwa kujitoa huko "obama akisema you are a good anamaanisha" does any body need to tell you, " your are a good man" find out! kumbuka hiyo ni statement ya rais wako katika kampeni za kwenda ikulu "IKULU ambayo NYERERE anasema ni mahali patatatifu, kama wazungu wanakutumia kwa maana hiyo panaweza tena kuwa patakatifu....... makame ndugu yangu vipi?
hahaha.. ndugu yangu kwani akili hiyo anayo??? alishalewa madaraka huyo hasikii ushauri wowote. labda ungemshauri atafaidika nini na mafisadi wenzake. lakini dawa yake itapatikana siku moja.. kwani kuna mtu aliye ota hata siku moja dola ya rumi inge anguka?
atakuja juta. mungu mkuu
Ndugu yangu
Dola nyingi zilianguka, siyo ya KIRUMI peke yake.
Mie nashangaa; hivi kweli mnataka tufanye USHABIKI wa Kumshangilia SLAA hata kama KACHEMKA? Perhaps JK na CCM sio The Best; lakini SLAA na CHADEMA SIO ALTERNATIVE.
Think Critically
Think Loudly
Think clearly
Think Analitically
Think Positively
THIS IS SAID TO BE A PLACE OF GREAT THINKERS, THINK NOW!!
NDUGU YANGU
DUNIA NZIMA IMEKUBALI USHINDI WA JK.
Salamu zimetinga kutoka Kila Capital.
Observers from all over the world wametoa POSITIVE REPORTS.
Usikurupuke na Majibu kama SLAA.
USHASOMA KITABU CHA ABDULRAHMAN MOHAMMED BABU - cha Siku Mia Baada ya Mapinduzi? Kakisome kile ujuwe mengi na uweze kupata ya kuchangia humu.
Nimezungumza hapa KUCHAKACHUA NDOA.
A) DKT SLAA ametengana na Mke wake
B) DKT SLAA AMETWAA MKE WA MTU.
C) DKT Slaa ametuambia kuwa MKE WA MTU ni MKE WAKE.
Kuhusu Kuchomekewa; wala sifanyi RESEARCH, Nakupa kitu affirmative. Watanzania Wote wenye kudadisi mambo na kuwa na ufuatiliaji wanajua kuwa Slaa AMECHOMEKEWA; ndio maana ukazuka Usemi mpya Mjini usemao, 'PAPARA KAMA SLAA'. Akipewa kitu, hata kama ni dhahiri kuwa sio cha ukweli; anakurupuka na kunadi kuwa ana ushahidi. Kinyume na yeye, watu waliokuwa MAKINI kwenye kazi zao, hawachomekewi kirahisi rahisi namna hiyo. Ana Kurupuka wala hajapata majukumu ya kuendesha dola; akipewa WILAYA TU si atatoka POVU huyo?
Inaelekea hujui kuwa MSUYA alishabwagwa awali?
demokrasia; za kukubali matokeo kama anavyofuata Kikwete. Sio mtu ukubali matokeo ukishinda tu; hayo ni mmatatizo ya Waungu WATU.
HOJA YA KUSEMA JK ANAKUBALIKA na INTERNATIONAL FIGURES, hao niliowataja HAPO ni wachache tu. Anakubalika Globally; Tena WATANZANIA DUNIA NZIMA WAMESHEHEREKEA USHINDI WA JK. Unatembelea Blog nyengine? Diaspora ya France, Italy, UK, Arabuni ETC wamefanya sherehe za kumuunga Mkono JK.
Aidha, unaposema kuwa hao viongozi wengine wa West Wananufaika, hapo sikuelewi kabisa.
Kuhusu KURA kupungua from 80% to 61%.
1. More than 50% of registered voters did not vote, hao wangepiga kura; tungeona victory ya JK ikizidi 80%.
2. CAMPAIGN ZA SLAA ZILIMUOKOA KUPATA KURA, kwa sababu ya mianya aliyokuwa akiitumia. WEWE UNAFAHAMU, sihitaji kutaja humu.
MWISHO KABISA, mimi sifanyi UTETEZI na wala sitegemei UKUU WA WILAYA WALA MKOA.
WADAU MIMI NIKO TANZANIA, tatizo ni kuwa OBJECTIVE.
Kama ni ishu ya kutetea UTAIFA, basi la kwanza kabisa ni kulinda amani tuliyo nayo; sio kuleta chokochoko. Zoezi la kupiga kura lishapita, na Watanzania Walio wengi wamempatioa KURA JK; hivyo; tuheshimu chaguo lao.
Aidha, nilitakiwa nitoe evidence, nimetoa report ya SADC, sasa kituu gani tena?
Penye amani, ndipo inapopatikana NEEMA na MAENDELEO.
Wadau, maisha baada ya Uchaguzi yashaanza. JK anaapa kesho tukijaaliwa, ataunda Baraza jipya, ambapo kutakuwa na sura mpya. Idadi ya wapinzani Bungeni imeongezeka, hivyo Bunge linatazamiwa kuwa lenye tija zaidi kuliko lililotangulia; na hiyo ni +ve achievement kwa Taifa letu.
TANZANIA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!
Dunia nzima ndio kitu gani makame? Hivi wewe unadhani marekani ndio dunia nzima? Na hao observers wangekuwa 'from all the world' wangeweza kufanya kazi kweli???
How big is your world makame?
Hivi kusoma hicho kitabu kimoja ndio kumpe mtu cha kuandika. Huwezi kusoma kitabu cha kibinadamu kimoja ukakamilika kimtazamo, huo utakuwa mtazamo wa A.M. Babu ambao ni wa kibinadamu, wenye mapungufu yake na 'angle' yake.
Kihistoria kuna wakati binadamu walijiona wamefika mbali sana baada ya kugundua jiwe la kutwangia nafaka. Mpaka sasa Makame unaniambia nisome kitabu chenye mbinu za kutwanga kwa jiwe hilo. Heshima sana kwa babu...lakini ujue dunia inabadilika sana tena kwa kasi sana.
Anyway endelea na huo msahafu wako.
Hapa wanasiasa unaowatetea watakukana, maana kwanza huu ni uzushi mtupu lakini pili wao ni hatari eneo hilo, nimekuonya sana usiwaponze, tutaandika hapa na kutoa picha za ushahidi...shauri yako.
Usemi mpya ukazuka wapi??? au ndani ya CCM ili kujipendekeza kwa ajili ya viti maalum. Suala la kupewa wilaya...hivi Dr. Slaa unamfananisha na Nape????You must be out of your skull.
Hapa ndo umeonyesha kuwa wewe ni mtoto wa juzi. Awali ipi hiyo...kilichofanya uchaguzi urudiwe tena baada ya JK kushinda mwanzoni na Benja kuwa wa pili kisha Cleopa wa tatu ni nini? Acha kuanguka kifafa kama Kikwete.
Hakuna chama tawala duniani kingetoka madarakani kama watu wangekuwa wanakubali matokeo kipumbavu kama wana CCM kwenye kura za maoni.
Unatembelea blog nyingine! Sikutegemea kama hoja ya kichovu hivi ingeletwa hapa. Unamwongelea nani maana hizo blog ni watu na sio pipi. Unaongelea watoto wao na vibaraka wao na vimada wao kwamba wamefanya sherehe za kuwaunga mkono???.naomba niishie hapo tafadhali. Unanitafutia kufungiwa wewe.
Huwezi kuelewa....wewe huna uwezo wa kuona nchi yako inavyobakwa. Naomba niishie hapo pia.
Acha pumba wewe...watu waliozuiwa na NEC kwa makusudi wasipige kura ili wasiipigie CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wangeipigia CCM au unasema mmekosa kura za kutosha za kuchakachua????
Taja tu...kwamba kwa sababu JK alitetea mafisadi walioiba pesa za wapiga kura na kutumia kumweka madarakani na kisha kuzifuja zilizobaki kwa safari za anasa ulaya.
Unapoteza muda wewe. Kwa pumba zako hata ukuu wa nyumbani kwako haukufai. Bora watoto wako wakuongoze.
Wewe si fisadi nani hakujui wewe? Toka zako hapa watu hatujui tutakula nini leo wewe na mafisadi wenzako mnakula tu huko kwenu Oysterbayacha watanzania wenye machungu tulalamike bwana..tunajua nini tunalalamikia wewe...
Kikubwa katika vitu mnavyolalamikia ni kwamba KAMPENI ZILIPIGWA PIA KATIKA MISINGI YA UDINI, unafikiri nani hajui hilo?
It was a Crusade; SASA waheshimiwa. Hili TAIFA tukianza UDINI tutafika? we are more united as TANZANIANS than as Waislamu au Wakristu.
Tukileta hizo tu
Tutafikia
Waroma, SDA, KKKT nk
Tunaenda wapi?
TUHESHIMU MATOKEO
TUWACHE MISINGI YA KISENGE YA UBAGUZI
TUTUMIE UMOJA WETU KAMA NGAO YETU
6. Ni kweli, kwani mimi uelewa wangu wa awali unaniambia kuwa ADUI namba moja wa TAIFA hili ni yule asiyeheshimu uamuzi wa KIDEMOKRASIA Wa WATANZANIA. Una bahati hii ni Tanzania, ingekuwa CHINA, watu kama wewe unajuwa wanapotunziwa.
Duh! Hiyo red hapo nimenyoosha mikono. Kwa hiyo kumbe tofauti kubwa kimsingi kati yetu ni CHADEMA (Dk Slaa) na CCM ( J. Kikwete). Mengine yote yanasomeka na mwenye akili anaona kipi ni kipi.
Kama unachukia ubaguzi kwa kiwango hicho, basi wewe na mimi kwenye hilo tuko pamoja na hii inaonyesha unaelewa unachoandika na unaelewa fika unachotetea hivyo tunatofautiana mitazamo ya kiitikadi, jambo ambalo si dhambi.
Endelea kuamini kuwa una ushahidi wa kutosha kuwa CCM ni bora, na mimi nitaendelea daima kuamini kuwa CCM imeoza na inahitaji kuwapisha CHADEMA na CUF waongoze Tanzania. Naendelea kuamini kuwa tumepoteza nafasi ya kuongozwa na kiongozi mwenye 'vision' Dr. Slaa au pengine Prof. Lipumba. Jakaya simkubali hata kidogo.....miaka mitano ya 2005 - 2010 ameboronga sana.
Nitafurahi kuendelea kuacha mambo ya 'private' mbali na 'public', hasa yanayohusu viongozi wa nchi.
Lakini bado sielewi Makame...kwa mtu anayechukia ubaguzi kiasi ulichoonyesha kwenye maandishi yako inawezekanaje ukafumba macho kiasi cha kutoona machafu ya CCM. Au wewe ni muumini wa 'scientology'? Kwamba huwezi kuamini kwamba mtu amekufa kwa kusikia tu au kuudhuria mazishi, mpaka uage kikristo...uone kabisa jamaa kwenye jeneza, wengine hujifanya wana huzuni sana kiasi cha kuigusa maiti na kuilalia huku wakitoa mayowe na kuangukia juu ya jeneza kumbe wanapima kama kuna dalili za uhai au ndo ameondoka kweli kweli.
Makame 'patriotism' unayoionyesha kwenye maandishi niliyoyanukuu hapo juu na jinsi unavyopinga wanamageuzi walioleta changamoto zenye manufaa kwa nchi yetu...ni mambo ambayo nakiri kuwa yananichanganya ubongo. 'how possible?'
Pengine ni ule msemo wa kifalsafa...'if you knew what i know....'
Umesahau ulidai kuwa siwezi kuhatarisha maisha yangu kwa kuandika kwenye 'blog'. Sasa watu kama mimi maana yake ni nini...in the absence of the so called 'blog' how would you categorize me as 'watu kama...'????? wakati huo ukidai wewe uko tayari kufa kwa ajili ya nchi hii....kufa kwenye maandishi ya kuitetea CCM au kufaje??? sasa unadai ingekuwa CHINA...???? unaonyesha tabia za kuwa mbishi na sina tabia ya kujadiliana na wabishi na endapo nitathibitisha hilo sitakujibu popote pale.
Pia ujue kuwa hiyo unayotaka wewe iheshimiwe siyo demokrasia ni domokrasia. kwamba watu wawe wananajisi kura za wananchi wakijua baada ya uchaguzi watasema uchaguzi umeisha tusonge mbele.....namna hiyo hatutafika.
Ukweli ukifukiwa kwa muda mrefu huzaa moto usiozimika...kama unafahamu historia unalifahamu hilo. Kama tunaipenda nchi yetu kweli kweli basi tuungane kupinga wizi wa kura...tusifukie fukie tu mashimo bila kutoa mabomu yaliyoko ndani yake...baadaye yatatulipukia wenyewe!!!!!!!!!!!!!!
AKASHUBE
Hadithi ya Doubting Thomas nina imani unaijuwa.
Sasa katika Riwaya hiyo, Tomaso aliendelea kukataa kwamba aliyesulubiwa amefufuka. Akazidi kukataa ndio mwenyewe hata baada ya kumuona na akaendelea hata baada ya kuona majeraha ya misumari. Mimi nimejifunza kuwa kuna akina Tomaso wengi katika mazingira tofauti, ikiwemo hili la kura.
Ni nini matokeo ya KURA?
1. CCM imepoteza viti vingi kwa wapinzani; Ishara ya mambo mawili:-
(i) Upinzani unaimarika na kukua
(ii) CCM imepuza umaarufu.
2. Kwenye kura za URAIS , CCM imepoteza takriban 20%, ikimaanisha kuwa Wananchi wametuma MESSAGE kuwa expectations zao hazijawa attained.
3. OVERALL Results ni kwamba CCM imeshinda uchaguzi wa Rais na imebata viti vingi Bungeni. Observers wamesema hivyo na Taasisi za uchaguzi pia.
Sisemi hapakuwa na Tatizo hata moja; na the best way ni ku pursue through mahakama.
Na la muhimu zaidi, ni kwamba RAIS AKISHATANGAZWA, huwa RAIS MPAKA MANDATE YAKEITAKAPOMALIZA
AKASHUBE,
kwangu mimi ulisha PROVE KUWA UELEWA WAKO WA MAMBO NI HABA AU DUNI KABISA. Sasa naona unakazana kuwathibitishia wana JF hilo.
Nafahamu fika kuwa Darasani ulienda kukariri, basi walau STATISTICAL PROCEDURES? You make Inferences using a REPRESENTATIVE SAMPLE. :tape:
Wewe Makame usituletee hapa, who told you of the representative sample existence? You should have known the so called representative sample is reductionist. Continue fooling your fellows people who are smelling corruption, Peleka huko your awkward arguements. Many good Tanzanians and decent people from other Nations globaly know exactly CCM have rigged presidential and parliamentary eletions. Does your selfish and narrow thinking represent the whole world? Come on, think loudly, there is never a representative sample.