Ushauri wa bure kwa CCM

Ushauri wa bure kwa CCM

Ccm haitakiwi ife, ili waone jinsi cdm inavyotengeneza mazingira ya nchi yetu. Kisha watasema wenyewe kuwa wao walikuwa hawasitahili kutawala.
 
Kwa jinsi mambo yanavyo enda kombo,ni vyema chama cha mapinduzi kianze kujipanga kuwa chama imara cha upinzani.
Ushahidi u wazi,KANU ya kenya ilishindwa kuliona hili mapema na inawagharimu kwa sasa.
Ni ushauri tu,kwani kama mwana mageuzi,sipendi pindi upinzani utakapochukua nchi,kuwe na chama cha kusimamia serikali itimize kazi zake.
Naomba kuwasilisha.

Siku CCM itakapopokwa utawala itakuwa siku ya furaha sana kwangu kwani najua hawa MAKUWADI WA SOKO HURIA walioingia, wakapata uongozi wa chama na kubadilisha dira ya chama watakimbia na kukitelekeza. Hii itakipa fursa ya kuangalia upya misingi ya uanzishwaji wake kama chama chenye mrengo wa UJAMAA na KUJITEGEMEA kilichoundwa kulinda na kutetea maslahi ya wakulima na wafanyakazi kwa minajili ya kuleta usawa na haki kwa wananchi huku kikipinga ukoloni na kwa sura zake zote na kilichobeba matumaini ya wananchi wa kawaida.
 
Kutokana na chama chenu kukosa mvuto miongoni mwa wananchi na kutumia gharama kubwa kukaa vikao visivyo na mafanikio mlikofikia inatosha haiwezekani nyanyuka tena kutokana na udhaifu huu ndani ya chama
-Kina sera zisizotekelezeka
-Kina tumia defensive mechanism badala ya problem solving
-Kina walinda mafisadi waziwazi pasipo kuona aibu
-wamebadilisha maslahi ya taifa kuwa ya chama( yaani jambo la kitaifa linajadiliwa na chama)
-Kinaendeshwa kwa unafki wa hali ya juu kwa kuoneana aibu baina ya viongozi wa Juu
-Kila kiongozi ndani ya chama hicho analinda maslahi yake kwanza( matokeo ya makundi)
-chama kinamilikiwa na matajiri fulani ndani yake(wanatoa maamuzi kwa nguvu ya pesa)

maoni yangu
Kutokana na mambo yote hayo na mengine chama hakina uwezo wa kutokomeza matatizo hivyo basi uweni chama kiundwe chama kipya mbona ccm ni mazao ya tanu ,asp, zaidi ya kufa na kuundwa upya ilikutengeneza sera mpya, watu wapya na spirit mpya kwa wanachama wake mtapata kifo cha aibu na kusahaulika katika historia.
 
Unapoteza muda wako kuishauri ccm . Acha wajifie wamepora mno rasilimali za taifa
 
Four Wheel itayoiondoa CCM toka kwenye tope zito bado Mjapani hajagunduliwa mpaka leo. Chama kinazama mchana kweupe kabisa.
 
Huo muda wa kuwashauri magamba unaupata wapi?acha wajifie wenyewe, kwani wameiba hela za umma mara ngapi? Achana nao.
 
hehehe nimeamua kuwashauri ili kupunguza aibu kwa wazee wetu ambao wamekunywa maji ya bendera hawasiti kukuachia laana unapokipondea chama chao
 
CCM wanaelewa hali yao ni mbaya kisiasa, ndiyo maana wanafanya warm up ya kuwa chama rasmi cha upinzani Tanzania 2015
 
Tatizo la CCM hawaamni nguvu ya umma bado, wao wanadhani mbinu zao chafu bado zinaweza kufanaya kazi dhidi ya nguvu ya umma 2015.
 
Back
Top Bottom