Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,502
113,610
Wanabodi,
Shirika la Ndege Tanzania ATC ni shirika letu na Ndege za ATC ni Ndege zetu hivyo shime Watanzania Wenzangu tuonyeshe uzalendo kwa kupanda Ndege zetu, Penda Chako, Jenga Chako kwa Kutumia Chako.

Tangu ATC imenunua hizi Ndege mpya za Bombardier, leo ndio nimepata fursa ya kuzionja ila kwa kulazimisha.

Naomba nisitaje destination ili kuwalinda wafanyakazi walio nihudumia kwa nía njema nisije nikawaponza ila kwenye customer care ATC Needs to improve.

Nilifanya booking yangu jana kwa njia ya simu. Nikaelezwa hakuna nafasi kwenye Economy Ndege imejaa. Nikasisitiza naomba tuu booking hata kama ndege imejaa ila tiketi yangu iandikwe waiting list. Baada ya ku insist ndipo nikaelezwa kuwa kwenye Business Class kuna nafasi ila nauli ya ni TZS 478,000 kwa One Way. Economy nauli ni 180,000 kwa one way.

Kosa la kwanza: Kwanini nilijibiwa ndege imejaa bila kuelezwa bussiness class ina nafasi? . Nisinge insist nisinge jua. Jibu rasmi lingepaswa kuwa economy imejaa lakini tuna nafasi business class.

Baada ya kujua kuna nafasi business class nikaomba booking ya economy na kueleza there are always no shows. Nikasema nibookie wakija wote wenye bookings zao, then nita upgrade from economy to business class. Nikaombwa number ya simu, sikujibiwa chochote. Huku kutojibiwa ni kosa la pili.

Leo mapema kabisa nikajibeba hadi airport nikauliza Airport Office ya ATC, to my surprise nikaambiwa ATC hawana ofisi uwanjani hapo! . Uwanja huo ni wa tatu kwa ukubwa baada ya JNIA na KIA. Kosa la tatu kwa nini ATC haina ofisi viwanja vyote vikubwa? .

Nikapelekwa Check in counter ya ATC uwanjani hapo nikaeleza nimefanya booking jana, wakaniomba reference number nikasema sijapewa, nikaomba waniangalie kwenye system Wataniona, labda aliyenifanyia booking alipitiwa kutonitumia ref no. Dada akanijibu saa hizi tunafungua check in counter, nenda subiri hadi wenye tiketi zao waishe ndipo nitakuangalizia!. Nilisubiri hadi abría wa mwisho. Ndipo nikaitwa, kuangalia hakuna booking yoyote iliyofanywa! .

Nikaelezwa kuna no shows hivyo nafasi ipo economy malipo ni cash na bei ni TZS 300,000 na sio ile ya 180,000. Nikauliza why, hakuna jibu naelezwa ndio bei yake!. Nililipa nikapewa boarding pass nikaboard.

Kufika ndani ya ndege, kwanza hakuna hata abiria mmoja wa business class hivyo seats zote reserved for business class zimesafiri empty. Jee abiria wangapi walijibiwa ndege imejaa hivyo kutafuta ndege za mashirika mengine?.

Kule ndani nako kulikuwa na mapengo ya hapa na pale kuashiria no shows kwenye economy.

Ushauri.
1.Watanzania ni Waswahili, no show sio big deal, hivyo ATC waanzishe mtindo kama wa Fast Jet, no show imekula kwako,no change, no refund.
2.ATC waanzishe over booking ila hizo extra waambiwe ni waiting list nafasi ikipatikana watakwenda, ikikosekana wataondoka na next flight. Ili ikitokea there is no shows or hakuna mtu wa business class, wawafanyie upgrade baadhi ya abiria muhimu na kuwaweka business ndege iende imejaa.
Tena leo kulikuwa na abiria mmoja wa wheel chair anabebwa na kuwekwa kwenye mbanano wa vile viti vya economy wakati business class ni empty!.

3.Waanzishe Frequent Flyer Program ili watu wavutiwe kusafiria ATC.

Otherwise huduma ni nzuri, japo viti vya Bombardier ni vidogo na hakuna any in flight entertainment ila refreshments zikiwemo bia! .

Big Up ATC, ndege yetu tuipende.

Paskali.
 
kwa kweli inasikitisha sana kama kweli hali ndo hiyo...maana hivo vitu wanavoshindwa kuvifanya ni majukumu yao...yani kila kitu mpaka ukomae ndo upewe huduma inachosha
 
Wasipo overhaul huo uongozi wote na hao wafanyakazi waluokuwepo, na kuweka uongozi mpya unaoelewa unafanya nini ni ngumu sana kusurvive kwenye competition.

Wanatakiwa kuelewa biashara siyo siasa ni good service ndo yamvutia mteja. Wasijidinganye kwamba kuna sheria inayombana mtanzania atumie tu ATC. Zitatumika tu pale huduma itakapokuwa nzuri Ikiwa hovyo ndo hvyo tena
 
Mkuu Paschal, mimi sio mjuzi wa mambo ya kupaa, lakini katika pitapita zangu naelewa:-

Tiketi ya ndege iliyofanyiwa booking muda mrefu kabla ya safari bei yake huwa ni rahisi kuliko bei ya kukata tiketi masaa machache kabla ya safari.

Naelewa pia bei za tiketi hutofautiana na msimu na muda gani wa siku unaosafiri. Aidha alfajiri, asubuhi, mchana na usiku.

Lakini kama ulivyosema customer care huwa ni kioo cha kampuni.

Nadhani, labda wanaogopa kutumbuliwa. Labda supervisor wa kiwanja husika anashindwa kutoa good judgment kutokana na macho mengi kuitazama Air Tanzania.

Otherwise nimependa ulivyoona tatizo na uka ainisha mapendekezo ya nini kifanyike.
 
Unachanganya economy na business class au? Wengi tunapanda economy chache ndo bznes
Business Class seats, zinakwenda empty kwa sababu hakuna aliyelipia Business Class wakati economy watu wamenyimwa nafasi kwa sababu ndege imejaa.

Kinachofanyika ni kufanya over bookings ya economy ili kama hakuna abiria wa Business Class, frequent flyers Wana kuwa upgraded to business class kisha nafasi zao wanapewa hao kwenye waiting list ili ndege isiende tupu.

Paskali
 
He dose not deserve that, tuwe wastaarabu. Heshima ni kitu cha bure.
He deserve, thats the foolish thing i dont wanna see here in JF.
"Be first to reply" so what? Whats the point? Ok hes the first, whats does he get then?
Many likes?

Thats foolish or gayish.
Tell him to stop.
:Back to the topic.
 
Wanabodi,
Shirika la Ndege Tanzania ATC ni shirika letu na Ndege za ATC ni Ndege zetu hivyo shime Watanzania Wenzangu tuonyeshe uzalendo kwa kupanda Ndege zetu, Penda Chako, Jenga Chako kwa Kutumia Chako.

Tangu ATC imenunua hizi Ndege mpya za Bombardier, leo ndio nimepata fursa ya kuzionja ila kwa kulazimisha.

Naomba nisitaje destination ili kuwalinda wafanyakazi walio nihudumia kwa nía njema nisije nikawaponza ila kwenye customer care ATC Needs to improve.

Nilifanya booking yangu jana kwa njia ya simu. Nikaelezwa hakuna nafasi kwenye Economy Ndege imejaa. Nikasisitiza naomba tuu booking hata kama ndege imejaa ila tiketi yangu iandikwe waiting list. Baada ya ku insist ndipo nikaelezwa kuwa kwenye Business Class kuna nafasi ila nauli ya ni TZS 478,000 kwa One Way. Economy nauli ni 180,000 kwa one way.

Kosa la kwanza: Kwanini nilijibiwa ndege imejaa bila kuelezwa economy ina nafasi? . Nisinge insist nisinge jua.

Baada ya kujua kuna nafasi Economy nikaomba booking ya economy na kueleza there are always no show. Nikasema nibookie wakija wote wenye bookings zao, then nita upgrade from economy to business class. Nikaombwa number ya simu sikujibiwa chochote. Huku kutojibiwa ni kosa la pili.

Leo mapema kabisa nikajibeba hadi airport nikauliza Airport Office ya ATC, to my surprise nikaambiwa ATC hawana ofisi uwanjani hapo! . Uwanja huo ni wa tatu kwa ukubwa baada ya JNIA na KIA. Kosa la tatu kwa nini ATC haina ofisi viwanja vyote vikubwa? .

Nikapelekwa Check in counter ya ATC uwanjani hapo nikaeleza nimefanya booking jana, wakaniomba reference number nikasema sijapewa, nikaomba waniangalie kwenye system Wataniona, labda aliyenifanyia booking alipitiwa kutonitumia ref no. Dada akanijibu saa hizi tunafungua check in counter, nenda subiri hadi wenye tiketi zao waishe ndipo nitakuangalizia. Nilisubiri hadi abriría wa mwisho. Ndipo nikaitwa, kuangalia hakuna booking yoyote iliyofanywa! .

Nikaelezwa kuna no shows hivyo nafasi ipo malipo ni cash na bei ni TZS 300,000 na sio ilegal ya 180,000. Nikauliza why, hakuna jibu naelezwa ndio bei yake!. Nililipa nikapewa boarding pass nikaboard.

Kufika ndani ya ndege, kwanza hakuna hata abiria mmoja wa economy hivyo seats zote reserved for economy zimesafiri empty.

Kule ndani nako kulikuwa na mapengo ya hapa na pale kuahiria no shows.

Ushauri.
1.Watanzania ni Waswahili, no show sio big deal, hivyo ATC waanzishe mtindo kama wa Fast Jet, no show imekula kwako,no change, no refund.
2.ATC waanzishe over booking ila hizo extra waambiwe ni waiting list nafasi ikipatikana watakwenda, ikikosekana wataondoka na next flight. Ili ikitokea there is no shows or hakuna mtu wa business class, wawafanyie upgrade baadhi ya abiria muhimu na kuwaweka business ndege iende imejaa.
Tena leo kulikuwa na abiria wa wheel chair anabebwa na kuwekwa kwenye mbanano wakati business class ni empty.

3.Waanzishe Frequent Flyer Program ili watu wavutiwe kusafiria ATC.

Otherwise huduma ni nzuri, viti vya Bombardier ni vidogo na hakuna any in flight entertainment ila refreshments zikiwemo bia! .

Big Up ATC, ndege yetu tuipende.

Paskali.
Bado kazi tunayo JPM aangalie hayo ndio yaliyochangia ATC ya zamani kufa kama atawanunulia ndege na kuwaachia wafanye walivyozoea huko nyuma ataweza kutimiza ndoto zake wala kushindana na mashirika mengine yanayofanya safari chini na nje! Tutashindwa hata kuweka mafuta, kama nauli 180,000 unaambiwa 300,000 nani atapanda watayarusha hivyo hivyo bila abiria kwenda rudi mpaka yachakae.. Walikupa na efd receipt ya hizo 300,000?
 
Back
Top Bottom