Najua nimeanza na kuelezea valentine spesho sehemu ya 1 ...
Naingia ndani zaidi kuwasaidia vijana na walipuaji wa mapenzi na majambazi ya mapenzi waliopo humu:
Mapenzi si kazi, kama ajira zingine, kama umeamua kuwa na dada/kaka huyu kubali kuwekeza kwenye hayo mapenzi yenu, Mapenzi ni ajira kama ajira zingine! ila kwasababu watu wengi kukaa kazini hawawezi ndio tunaona vilio viiingii vinatembea leo duniani kama wanaume waongo, wahuni, matapeli, wajinga, na maneno mengi mengi
My dia kama hauiwezi KAZI ya mapenzi usiingie kabisa ndio maana Mapenzi ni ya watu wazima wenye akili zao timamu sio uwanja wa maigizo!
Valentines Day sio siku na sehemu ya kupaua penzi, bali kuendeleza kilichopo kwa undani zaidi... lakini sasa wabongo wa vizazi vya 4G wanataka Mapenzi show za fasta fasta, aingize chuma cha moto atembee ndio anajiona kidumeee hapanaaa;
Ngoja nikusaidie kitu kimoja!
Kama kweli unampenda huyo mpenzi wako ushawahi kujiuliza ni kwa namna gani unamfahamu mpenzi wako?:
Labda tuangalie mambo mawili kwa sasa:
1. HISIA ZENU ZA NDANI (MOYO)
Vile ambavyo mpenzi wako anavyojiskia na kumruhusu mpenzi wako kuona yaliopo ndani yako!
MFANO: Mpenzi wangu anafurahishwa/kuumizwa na nini?
Ulkishawahi kujiuliza na kutaka kujua furaha au kilio cha mpenzi wako kinaletwa na nini? ili uendeleze furaha na kuondoa kilio... nini kinakutafuna ndani ambacho huwezi kusema kwa mwingine zaidi ya mpenzi wako!
Ukiweza kugusa hisia za mpenzi wako ndipo mafanikio ya mapenzi yenu yanapoimarika
hapo ndipo unaskia watu wanasema huyu mpenzi wangu ananijua nami namjua zaidi, kifupi tunajuana!
Je wewe na mpenzi wako mmefikia level hii au mnalipua tu?!
Kama mpenzi wako hana hisia na wewe, bro/sistaa kimbiaa! acha na viatu watakuletea majirani! Mapenzi sio kidali po, huyu anazinga huyu anajificha
Mapenzi ya kweli na kama ulishawahi kukutana na watu wanaopendana (True Love) hujali hisia za kila mwenzake!
Mahusiano yalio na hisia za kweli za ndani huleta kitu tunachokiona kwa wengine wengi duniani kinachoitwa TRUE LOVE
nataka kumwona mpenzi wangu aliekuwa na furaha, tukiwa tunataniani wakati tulipokutana mara ya kwanza, kwanini sasa amebadilika? imekuwaje?
Kitu gani kinamwumiza au kumliza mpenzi wangu?
Kwanini nikimpeleka mpenzi wangu kwa wazazi wangu hana furaha kuna nini? mtu unakuwa buzy ku invest (kuwekeza) kumfahamu mpenzi wako,
Lakini sikuhizi walaaa hamna mtu anahangaika kuwekeza kwenye hisia za mpenzi wake
Kazi, biashara kisifanye kukuzuia kumjua mpenzi wako alivyo hasa hisia zake
Kazi za ofisini au Biashara zako usilete nyumbani, cheo chako kiache ofisini ukiingia nyumbani kwenu, sio unaleta u director sijui ukurugenzi, mimi mme wangu namwambia ukurugenzi mwisho pale nje ya geti ukiingia ndani wewe ni mume....baba wa watoto wangu
Kama ni Baba/ Mama ukifika nyumbani itumie nafasi yako kama baba/mama kwenye familia... kama mume kwenye ndoa, usipoitumia nafasi yako vizuri wenzio watakusaidia nje! ndio maana michepuko haiiishi!
Hapa kwenye kuzijua hisia za mpenzi wako aliyefaulu so far alikuwa ni YESU KRISTO wa Mbinguni na akina Romeo & Julieth walifaulu hii show!
2. MAWASILIANO YAKO NA MPENZI WAKO YAKOJE?
Unavyowasiliana na mpenzi wako mpo kwenye level (ngazi gani)?
Kila mahusiano yana ngazi tofauti tofauti... kuna wale wanaoanza mahusiano tunawahita honey mooners, kuna wale waliokatikati na wale waliokubuhu...
Regardless ya ngazi lakini katika kupanga mambo ya kila siku, kifamilia (mipango ya sasa na baadae) je mawasiliano yenu yanakuwaje?
au ndio mnapeana habari za juu juu za kimjini kimjini mambo ya kibishoo ah me nishampa taarifa mpenzi wangu kwa juu juu kuwa leo au wiki ijayo nitakuwa safari au mwezi huu sina hela kwahiyo tutakula majani ... ada nimeshalipa, vocha nimeshamnunulia ya mwezi atanipigia mwenyewe
Mahusiano yasio na mawasiliano mazuri, hata kama mimi nakaa kufanya nini labda? mambo ya kuzeeshana kwenye mahusiano yenye mawasiliano mabovu, especially pale mpenzi wako hataki kufanya jitihada kwa upande wake.. mpendwa kimbiaaa!
Kila mwenzi akifanya majukumumu yake vizuri ataleta mawasiliano mazuri kwenye ndoa, mahusiano na familia yake!
Katika ndoa kila mtu ana majukumu yake... mke/mume ana majukumu yake tusiingiliane, ndio maana kila mtu akienda kazini anapewa majuku yake
Mafanikio ya Mwanaume yanategemea aina ya mwanamke aliyenae, Mafanikio ya Mwanamke hayategemei aina ya mwanaume alienae!
Mfano:
1. Ukiona mwanaume amekaa kaa ki-hasara hasara amekondeana yupo rafu, atakaeulizwa ni mwanamke sio mwanaume!
2. House girl anafanya kazi zote za mpenzi wako! mpaka kumsugua mgongo mpenzi wako, anafua nguo za mumeo, anampikia mumeo
Mapenzi sio tamthilia za kichina au soap babra za North America, Mapenzi ni realistic kama utachukua muda wa kuwekeza kwenye hicho kitu kinachoitwa mapenzi.
Vinginevyo utakuwa unaona wenzio wanaenda vizuri kwako kumenuna, ndio mnaaza kuibiana mabwana, kulogana ushenzi mtupu!
Mahusiano yalio na mawasiliano mazuri huleta kitu tunachokiona kwa wengine wengi duniani kinachoitwa TRUE LOVE
Ukitaka TRUE LOVE wekeza kwenye hisia na mawasiliano yenu
Alicia Keys na Mumewe Producer walishapata True Love!
Wishing you a Blessed Valentine for those who had/have found true love like me