Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,301
- 33,920
Kihistoria Lipumba hakuwahi kuwa mwanasiasa bali alikuwa anatumiwa na chama cha siasa kufanikisha malengo yake ya kisiasa. Lakini kwa bahati mbaya sana chama kilichokuwa kinamtumia kwa mambo ya siasa kilidharau kumshughulikia kisiasa pale alipoonekana mwaka 2015 anataka kutumiwa kisiasa na CCM.
Leo Lipumba ni kikwazo kikubwa sana ndani ya CUF si kwa sababu ana nguvu za kisiasa (hajawahi kuwa nazo) bali ni kutokana na mwendelezo wake wa kutumika kisiasa dhidi ya CUF.Kwenye uchaguzi wa 2010 Lipumba alitumika kisiasa dhidi ya CHADEMA na kwa maneno yake mwenyewe ilikuwa ni "kuokoa jahazi lisizame". Leo ni zamu ya Lipumba kutumiwa na CCM dhidi ya CHADEMA.
Lakini la kujiuliza ni kwa nini siku zote hizo CUF walivumilia Lipumba kutumiwa kisiasa na CCM dhidi ya vyama vingine pinzani kwa CCM? Tangu Uchaguzi wa mwaka 1995 Lipumba alikuwa anapambana kugawa kura za wapinzani dhidi ya CCM. Inavoonekana Lipumba ana "kazi maalum" ya kuhahakikisha kwamba kura za wapinzani wa CCM haziunganiki kwa hali ama njia yoyote ile.
Ushauri wangu kwa vyama vya Upinzani hasa chama cha CUF na CHADEMA ambavyo ndiyo vinalengwa na CCM, kwa sasa vibadili mbinu za kupambana na Lipumba. Watendaji wa Serikali wanaomuunga mkono Lipumba hawafanyi hivyo kwa kuwa wanaamini kwamba Lipumba yuko sahihi, bali wanafanya hivo kwa kuwa hawana kingine cha kufanya kubakia kwenye ajira zao.
Kwanza kuwe na Mkakati wa pamoja tena yakinifu wa kupambana na wanaomtumia Lipumba na wanaosaidia CCM kumtumia Lipumba. Lipumba anapowafukuza wabunge anaamini kwamba CUF haitashinda uchaguzi ukirudiwa na CCM ndilo walitakalo. Lazima UKAWA wawe wamoja bila ya hivyo watapigwa!